TAARIFA YA POLISI NA PICHA 7 ZA MGANGA WA KIENYEJI ALIYEKAMATWA NA KIGANJA CHA BINADAMU KIKIVUJA DAMU....PICHA ZINATISHA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAGANGA wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu ambapo walikamatwa kwenye eneo la ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.





Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.


Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.


Taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.


 kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbona picha ziko mbili tu mdaku?

    ReplyDelete
  2. Jaman, hatar dunia sasa inatsha...!!

    ReplyDelete
  3. ee mungu tunusur

    ReplyDelete
  4. waungwana dunia inakwishi turudi kwa m/mungu wetu! kwani m/mungu alisema dalili ya kumalizika kwa dunia kutatokea kila aina ya viroja!

    ReplyDelete
  5. polisi msikubali kuchukua rushwa ya mfanyabiashara huyo baadae kesi iharibike

    ReplyDelete
  6. Mbona they got the middle finger up?

    ReplyDelete

Top Post Ad