STORI KUHUSU MWANAMKE ANAYE CHUKUA WALEMAVU TANZANIA NA KWENDA KUWAFANYISHA BIASHARA YA OMBA OMBA MOMBASA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Citizen TV Kenya wanaripoti kwamba huko Mombasa wamekamatwa watu 26 wenye ulemavu ambao walichukuliwa kutoka Tanzania na Mwanamke Mtanzania ili kwenda kufanya biashara ya kuomba pesa na baadae jioni Mwanamke huyo anapitia mahesabu huku akiwa amewaweka walemavu hawa kuishi kwenye nyumba moja huko Mwembe tayari.
Mwanamke huyu nadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza Walemavu kuchukuliwa Tanzania na kuingizwa Kenya kupitia Taveta na Lungalunga ambapo anawatumia kibiashara yeye na washirika wake ambapo mpaka sasa washukiwa saba wametiwa mbaroni kutokana na hii ishu.
Taarifa inasema ombaomba hawa ambao wanatoka Shinyanga, Mwanza, Musoma na Bukoba wakiwa mitaani kuomba, wakipata shilingi mia tano ya Kenya tajiri anachukua shilingi 300 na anamuachia shilingi 200.
Mmoja wa Walemavu hao anasema ‘kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa Baiskeli lakini kinachotokea sasa hivi ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, Mwanamke huyu ndio anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya’

Angalia video:
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watanzania tuwe makini sana kuangalia wenzetu wanapelekwa wapi? na pia kujenga tabia ya kuwatembelea wenzetu hata km wako mikoani ilikujifunza upande wapili wanafanyaje wenzetu ni vema tukawa na tabia ya kuangalia usalama hata wa wanafunzi wetu mashuleni na vyuoni sio kuwa acha km vile wanajua kila kitu.

    ReplyDelete
  2. wonder shall never end

    ReplyDelete
  3. Tanzanians this is a shame to you all.

    ReplyDelete

Top Post Ad