UVCCM WAZIKANA PICHA ZA UCHI ZA GODBLESS LEMA....WADAI KUWA MWENYEKITI WAO HAJAHUSIKA KUZITENGENEZA NA KUZISAMBAZA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa ya kifo cha mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr Sengoondo Mvungi ambacho kimetokea katika hospitali ya Millpark nchini Afrika kusini.

Uongozi wa UVCCM Taifa unatoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu, pia UVCCM inatoa pole kwa uongozi wa NCCR- Mageuzi na kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Warioba pamoja na Vijana nchini kote ambao wamenufaika na Utaalamu na mafunzo.
  
Kama vijana tulihitaji sana mchango wa mawazo, hekima na utaalamu kutoka kwake, hakika tumepoteza kiongozi shupavu, muadilifu na mzalendo ambao  ni mfano wa kuigwa kwa Vijana wa Taifa hili.

Kadhalika, UVCCM inatoa pongezi za dhati kwa hotuba makini iliyojaa hekima, busara na ushupavu wa Uongozi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Pia, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesikitishwa na tuhuma ambazo zimeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kutoka kwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mheshimiwa Godbless Lema ambazo amezielekeza kwa baadhi ya Viongozi wa Jumuiya akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM Ndugu Sadifah Juma kuwa amehusika na usambazaji wa Picha chafu za  uchi mitandaoni. 

Pamoja na kusikitishwa, UVCCM inazo taarifa juu ya mgogoro unaoendelea katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kwamba inamtaka Lema kutoelekeza tuhuma kwa UVCCM na viongozi wake bali waangalie namna bora ya kushughulikia na kutatua migogoro yao ya ndani ambayo imesababisha kuzushiana, kuchafuana na kuvujishiana siri katika mitandao ya kijamii. 

UVCCM na Viongozi wake inakana kwa namna yeyote ile kuhusika na usambazaji huo na kwamba Jumuiya hii ni ya Vijana makini na wanaojitambua na inajielekeza katika kufanikisha malengo ya kuundwa kwake ya kukisaidia Chama kushika dola mwaka 2015.

Na kwamba UVCCM inalaani tabia ambayo imeasisiwa na Vijana wa CHADEMA ya kukashifu, kuzomea na hata kutukana Viongozi wa CCM na Serikali yake na kwamba yaliyomkuta Mhe Lema ni matunda ya kazi waliyoiasisi wenyewe.

Imetolewa na:

PAUL MAKONDA

KATIBU WA IDARA YA HAMASA NA CHIPUKIZI

UVCCM

13/11/2013
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MakondA umekonda hata ubongo wa kufikiri? Kashfa zenu kwa kamanda lema ni sawa na ukichaa wa kujaribu kupunga ili kusimamisha ndege inayopasua anga! Mnamuongezea umaarufu bure.

    ReplyDelete
  2. Hkuna mbinu yoyo itkayofanikiwa kuzuia utawaka wa haki kuongoza tz..

    ReplyDelete
  3. Poor Makonda, sikutegemea msomi kama wewe kuandika taarifa mbovu isiyo na dhima kama hii. Unazidiwa hata na bwana Msungu mwenyekiti wangu wa kitongoji. Poor Makonda ungeweza kuwaomba hata wenzako wakusaidie, achana na upowermonger wakati kichwa chako cha kukariri tu!

    ReplyDelete

Top Post Ad