March 2013


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) amesema haungi mkono pendekezo la Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema mapendekezo hayo yametolewa na watu wenye kutaka kujipendekeza kwa mkuu wa nchi badala ya kufikiria kuutangaza Mkoa wa Mbeya katika nyanja ya kimataifa.
Alisema Mbeya ina historia ya kutaka kujitangaza kimataifa na uwanja huo ni fursa pekee ya kufikia malengo hayo aliyoeleza kuwa yanataka kufifishwa na wateule wa rais.
“Siungi mkono uwanja kuitwa kwa jina la JK, tunataka jina litakaloasisi uhalisia wa Mbeya nasi tufahamike kimataifa, kamati ya ushauri ya mkoa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Norman Sigala ilikurupuka kuleta wazo hilo kabla ya kuwasiliana na wabunge,” alisema.
Alisema hatua hiyo ya Sigala haiwakilishi mawazo ya wananchi bali inawakilisha mawazo ya mtu aliyeteuliwa na kwamba wao wakiwa wawakilishi wa Mkoa wa Mbeya kwa ridhaa ya wananchi hawawezi kukubaliana na suala hilo.
Kauli ya Sugu iliungwa mkono na wabunge wengine wa Mkoa wa Mbeya, ambapo Mchungaji Lukson Mwanjale wa Mbeya Vijijini (CCM) alisema anasikitishwa na hatua hiyo ya kuliwasilisha wazo hilo bila ya kuwashirikisha wabunge.
Alisema wakati wa kikao cha kamati ya ushauri wabunge wengi hawakuwepo na taarifa hizo walizisikia baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo ambaye pia ni mbunge wa Songwe, aliomba apewe muda wa kutaka kujua sababu zilizoibua wazo hilo.
Wazo la kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete linazidi kupata upinzani ambapo awali chama cha NCCR-Mageuzi na kile cha PPT Maendeleo kupitia kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya vilipinga wazo hilo.Mwanadada Vanity Wonder ameamua kuandika kitabu kusimulia kwa nini aliamua kutumia kiasi cha dola 15,000 kuchoma sindano za kukuza makalio.

Vanity mwenye miaka 30 mama wa watoto wa wawili wa nchini Marekani kabla alikuwa mwembamba tu hana makalio.

Anasema wanawake wengi hufikia hatua hiyo sio kwa lengo la kuwavutia wanaume bali kutoridhika na anachokiona kila anapojiangalia kwenye kioo.

Vanity anavyoonekana sasa baada ya kukuza hips na makalio.Anasema ameamua kuandika kitabu kuelezea ukweli kwa nini aliamua kufanya hivyo.

Anasema kuwa kwenye process wanawake wengi hupoteza maisha,hupata ulemavu wa kudumu na matatizo mengi tu hutokea.Wanawake wengi kisa kamuona mtu fulani kafanikiwa kukuza makalio hupata tamaa matokeo yake huenda kwa wataalam wa vichochoroni kukwepa gharama.Matokeo ndio huwa vifo na ulemavu


Hi Admin..Hide My Name ....
Wadau embu nishaurini, nina Girlfriend wangu ambae ni mke wa mtu, huyu mwana dada ni mama wa watoto wawili, ebana kila nikikutana nae kwa siri kubwa katika suala la mapenzi anasema anafaidi sana mapenz yangu kuliko ya mume wake, sasa juzi kaniambia kipindi yupo chuoni alikuwa na boyfriend wake aliyeanza kumchezea sehemu za kinyume na maumbele, ameniomba sana nimkumbushie sababu ameshindwa kuvumilia kuishi na mume wake bila kumla tigo, na kumwambia mume wake amchezee sehemu ya tigo hadhubutu sababu anamheshimu, sasa kanipa iyo kazi mimi, kwa kweli cjawai kupiga iyo kitu jamani, jana kanilazimisha sana ila cjafanya ivyo, kwa kweli ananitoa sana kwenye mambo flani ya umatemate, sasa nipo njia panda wadau, nikiachana nae na misaada yake kwangu itakuwa ndo mwisho, ushauri wenu Tafadhali....


Baada ya kusoma maudhui yaliyomo kwenye taarifa hii ya NHC, nashawishika kusema uongozi wa sasa chini ya DG Mchechu haustahili chembe ya lawama.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUANGUKA KWA JENGO LA UBIA KATI YA NHC NA M/S LADHA CONSTRUCTION LIMITED LILILOKUWA LINALOJENGWA KATIKA MTAA WA INDIRA GANDHI JIJINI DAR ES SALAAM

Leo tarehe 29 Machi 2013, mnamo saa mbili na nusu asubuhi jengo linalojengwa kwenye kiwanja namba 2032/73 Mtaa wa Indira Gandhi lilianguka kutokana na sababu ambazo bado hazijathibitishwa kitaalam na mamlaka husika. Shirika la Nyumba la Taifa linasikitika sana kutokana na kuanguka kwa jengo hilo pamoja na maafa yaliyotokana na tukio hilo la kusikitisha. Pia Shirika linatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba uliotokana na ajali hii.

Mradi huu wa ubia kati ya NHC na M/s Ladha Construction Limited ya Jijini Dar Es Salaam ulianza kutekelezwa tarehe 4 Februari 2008 ambapo Shirika la Nyumba litakuwa na hisa asilimia 25 na mbia ana asilimia 75 mara baada ya mradi kukamilika. Kwa mujibu wa sera ya ubia iliyoanza kutumika mwaka 1993 na kuhuishwa mwaka 1995 na 2005, Shirika la Nyumba la Taifa lilikuwa likitoa ardhi ambayo ilikuwa ikihesabika kama asilimia 25 ya mtaji wake kwenye jengo husika na mbia alikuwa akipata asilimia 75.

Kwa mujibu wa mkataba huo mbia mwendelezaji M/s Ladha Contruction Limited kama walivyo wabia wengine, anapaswa kabla ya kuanza ujenzi kupata vibali kutoka kwenye mamlaka husika na kuwa na wataalam wa ujenzi na washauri waliokubalika na kuthibitishwa na mamlaka husika. Aidha, mbia huyu akishapata wataalam hao ndiye anayehusika kuingia nao mikataba ya kazi ya kujenga na kusimamia ubora wa jengo husika kwa mujibu wa sheria. Katika mradi huu mbia mwendelezaji aliajiri wataalamu wote waliosajiliwa na Mamlaka husika ambazo ni CRB, ERB, AQRB na Mansipaa husika na mamlaka nyinginezo. Kwa kuwa ujenzi ulikuwa bado haujakamilika, Shirika lilikuwa bado halijapata asilimia 25 ya umiliki wake.

Pia tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, Shirika la Nyumba la Taifa, lilisimamisha utoaji wa miradi mipya ya ubia mwaka 2010 ili kuweza kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa miradi ya ubia na hivyo kuwezesha kutengeneza sera mpya. Kama sehemu ya zoezi hilo, shirika pia lilifuta jumla ya mikataba 64 ambayo ilikuwa imesainiwa lakini haijaanza ujenzi.

Katika sera mpya ambayo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni Shirika litahusika moja kwa moja katika kuteuwa mjenzi mtaalam (contractor), msimamizi mtaalam wa mradi husika (consultant) na kusimamia kikamilifu shughuli zote za ujenzi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya vyomba husika kuwasiliana na mjenzi wa mradi huu. Aidha, taarifa zinaweza kupatikana moja kwa moja kutoka M/s Ladha Construction Limited ambaye ndiye mbia mwendelezaji aliyekuwa anasimamia ujenzi huu.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
 
S.L.P. 2977 Simu: 2851590 DAR ES SALAAM
Telegrams : "NYUMBA" TANZANIA
Fax 2851442


Ni wawekezaji,ambao waliahidi kutoa fursa sawa za ajira kulingana na fani ya muombaji,lakini hali si shwari migodi ya barrick hasa buzwagi na bulyanhulu... Rushwa iko wazi bila pesa kazi hazipo,wanatangaza magazetini kila kukicha lakini kwa uhalisia barrick wameendekeza rushwa sana.

Tumefika hapo, tumekaa hapo muda mrefu imefikia hatua mtu anakuambia ni kiasi gani cha pesa utatoa ili kupata nafasi fulani,mfano kama kazi ina mshahara wa laki 8 kwa mwezi utatakiwa kutoa rushwa ya million moja,na watakupa mkataba wa miezi sita,ukihitaji kuendelea utatakiwa kulipa millioni tena'

Kwa ujumla migodi ya barrick hasa buzwagi na bulyanhulu imetapakaa rushwa,kazi inayohitaji mtu wa digrii utamkuta form four kigezo ni kwamba alitoa rushwa:Wanao husika hususani TAKUKURU tembeleeni maeneo hayo nendeni kijiji cha kakola,bugarama,ilogi na mwingiro halafu waulizeni wananchi suala hili watawaambia sababu ni jambo ambalo sasa limekuwa ni kama utamaduni..

Kama wapo humu wanaohusika waje wakanushe.
By Mdau
Source:Jamii ForumsWANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).

Kukamatwa kwa wanawake hao ambao ni Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na Ziada Mukamurera (25), kunafuatia mmoja wao Esperance kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kuwa alikuwa ameibiwa fedha taslimu Sh 800,000 na hati ya kusafiria.

Lakini, Polisi walipofika nyumba ya kulala wageni waliyofikia iliyopo eneo la Area D walikuta wanawake wengine wawili ambao walikuwa wakikaa chumba kimoja na Esperance.

Uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa mwanamke huyo hakuibiwa na kubaini wote si raia wa Tanzania. Hata hivyo kilikosekana kifungu cha kuwashitaki ndipo waliamua kupeleka sakata hilo Uhamiaji ili liweze kushughulikiwa.

Kulingana na maelezo yao, Esperance alitangulia kuja nchini kisha kuwaita wenzake ambao ilikuwa ni mara ya kwanza kuja nchini, lakini hata hivyo alisema kuwa, kumekuwa na makundi ya wanawake kutoka Rwanda wanaokuja nchini kipindi cha Bunge na hata mwaka jana kuna kundi lilikuja wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Uhamiaji, wanawake hao waliingia nchini na kujitambulisha kuwa walikuja Dodoma kufanya biashara ya vitenge, lakini hawakuwa hata na kitenge kimoja ambacho kingeweza kuwaonesha kuwa walikuwa wakifanya biashara hiyo.

Juhudi hizo za Uhamiaji zinadaiwa kuwafikisha hadi klabu moja maarufu ya usiku iliyopo eneo la Area D ambapo walinzi wa Kimasai walikiri kuwafahamu wanawake hao na walikuwa wakiwafuata nyumba ya wageni waliyofikia kama mtu alikuwa akiwahitaji na walikuwa na ni wateja wa klabu hiyo ya usiku.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Norah Massawe alikiri kukamatwa kwa wanawake hao na polisi na kukabidhiwa Uhamiaji.

Alisema mwanzoni wanawake hao walidai kuwa walikuja Dodoma kwa ajili ya kununua vitenge kwa ajili ya biashara na waliposhikiliwa na Polisi kwa siku kadhaa waliomba kurudishwa nchini kwao.

Alisema wawili kati yao walikutwa wakiwa na vidonge vya ARVs, lakini haijafahamika moja kwa moja kama walikuwa wagonjwa au la.

“Siwezi kusema walikuwa ni makahaba bali wanahisiwa hivyo kutokana na biashara waliyosema wanafanya kutoeleweka na hata maelezo ya walinzi wa klabu ya usiku kuwa walitambuliwa kama wateja wao, kwa kweli hilo siwezi kulithibitisha,” alisema.

Aliwataka wananchi kuwa makini na watu wasiowafahamu kwani hivi sasa Mkoa wa Dodoma umekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu hasa katika kipindi cha Bunge.

Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Dodoma, Audrey Njelekela ambaye alisema kuwa, wamekuwa wakitoa elimu kuanzia ngazi ya Mkoa hadi mtaa ambapo kuna timu ya Mkoa ya Ukimwi na hata kwenye halmashauri kuna waratibu ambao wamekuwa akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Ukimwi.

Alisema kuwa kwa sasa kiwango cha maambukizi kwa Mkoa wa Dodoma ni asilimia 2.9 kwa takwimu za mwaka 2011 na 2012 ikilinganisha na takwimu za mwaka 2007 hadi 2008 ambapo kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 3.3.

Alisema kuwa waratibu wa ngazi ya halmashauri wamekuwa wakitoa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi kwenye maendeleo mbalimbali ikiwemo klabu za usiku.

Alisema kwa kuwa kondomu zinasambazwa maeneo mbalimbali yakiwemo ya starehe ni vyema wananchi kuhakikisha wanazitumia. “Matumizi ya kondomu ni muhimu sana kwani maeneo ya klabu za usiku na maeneo mengine ya starehe watu wengi wanachukuana tu lakini wanakuwa hawafahamiani,“ alisema.

Alisema kuwa kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu katika Mkoa wa Dodoma hasa kipindi cha Bunge, umakini zaidi unahitajika.

CHANZO: HABARI LEO

Hii  ni  kauli  ya  msanii Diamond kuhusu Q chief: mi nafanya kazi, mazoezi na dancers, nahangaika kutafuta sare, kuandika nyimbo nzuri, wakati nafanya yote hayo we unakula unga, halafu unakuja kusema nasafiria nyota yako, nisafirie nyota ya mla unga? mi staki, staki, agombane na wakubwa wenzake kina dully mi aniache na wadogo wenzangu staki...?


Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira"

"Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"

Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

"Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"

" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"

Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa