NDOA YA OBAMA NA MKEWE MICHELLE SHAKANI..TALAKA YADAIWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Marekani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani vya Ikulu ya Marekani, wenza hao wamekuwa katika migogoro na Obama alilazimika kusherehekea sherehe za mwaka mpya mjini Hawaii akiwa na binti zake wawili, Sasha na Malia bila kuwepo Michelle.

Jarida la National Enquirer lilieleza kwamba katika moja ya matukio, Obama aliwahi kukutwa akiwa na mwanamke mwingine katika ‘mazingira ya kutatanisha’ wakati mkewe akiwa safarini.

Kutokana na ripoti iliyotolewa na Bombshel , Michelle na Obama wamekuwa wakilala vyumba tofauti ndani ya Ikulu. Michelle pia anajiandaa kuhama katika jumba lao pale Chicago ambalo wameishi wakati wa uchumba wao miaka 21 iliyopita na kwa msisitizo watajadili juu ya talaka.

Taarifa ilidai tatizo limeanza miaka minane iliyopita pale Obama alipodhamiria kujijenga kisasa. Ni mtoto wao Sasha ambaye aliumwa ugonjwa unaosababishwa na woga wa maisha unaoitwa Spinal Meningitis ndiyo uliowafanya waendelee kuwa pamoja.

Kitabu cha Anderson kinaelezea tatizo lilivyoanza baada ya Barack Obama kuamua kuingia kwenye siasa, ambapo Michelle alisikika akimwambia mumewe; “Wewe unajifikiria mwenyewe tu.”

Naye Barack Obama amesikika akisema: “Sikuwahi kufikiri kamwe kwamba ningelea familia mwenyewe siku moja.” Anderson anadai kuwa Obama amechoshwa na malalamishi ya mkewe.

“Nampenda sana Michelle lakini ananiumiza na ubishi wake wa kila mara,” alisikika akisema Obama na kuongeza kuwa; “Anaonekana ni mwingi wa machungu na hasira siku zote.”

Akizungumza na televisheni ya CBS ya Marekani, Anderson alidai kuwa ilikuwa nusura Michelle atembee nje ya ndoa kwa sababu ya upweke.

Kwa miaka mitano wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wao wa kupata watoto kabla Malia hajazaliwa. Walishajadili sana suala la kuasilia watoto (adoption) na marafiki zake wa karibu lakini kwa bahati nzuri Malia alizaliwa mwaka 1998 na kuondoa wazo hilo.

Jina kamili la Obama ni Barack “Barry” Hussein Obama, Jr, alizaliwa Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawaii, alikulia huko huko Hawaii na Indonesia, baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Jina kamili la mkewe ni Michelle LaVaughn Robinson, alizaliwa Januari 17, 1964 Chicago, Illinois.

Kukutana kwako

Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 katika mazingira ya kikazi, walifunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika Kanisa la Umoja wa Kristu la Trinity lililopo Chicago, Illinois.

Lakini vyanzo vingine vya taarifa zinadai kuwa ndoa haiko imara, hasa baada ya tukio la Obama kupiga picha za pamoja bila aibu na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt (46) wakati wa mazishi ya aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrka Kusini, Neslon Madiba Mandela.

Obama akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, alikuwa akicheka na kumnong’oneza kitu waziri huyo mara kwa mara kwa muda wote, huku Michelle akiwa pembeni yake amenuna. Mara nyingi alikuwa akimshika shika mabega.

“Lakini kwa sasa Michelle anajiona kanyanyasika na kuaibishwa mbele ya dunia kwani picha hizo zilirushwa duniani kote kupitia televisheni, magazeti na mitandao mbalimbali. Alisikika akimtapikia Obama huku akisema “Nimechoshwa.”

Pia tatizo limekuzwa na safari ya kikazi ya Obama hivi karibuni kule Thailand ambayo ilimkutanisha na Waziri Mkuu mrembo kuliko pengine wote duniani , Yingluck Shinawatra.

Tarifa zaidi zilieleza kwamba usalama wa taifa nchini humo unafahamu kuhusu suala hilo, lakini umekuwa ukilichukulia kama suala binafsi na Michelle alionekana kukasirishwa kupita kiasi alipopata taarifa hizo.

“Baada ya tukio hilo Michelle aliamua kuwasiliana na mwanasheria wake akitaka kujua namna ya kuomba talaka na alimwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ilielezwa kwamba Michelle ataendelea kuishi mjini Washington DC hadi binti yao mdogo, Sasha (12) atakapomaliza elimu yake ya sekondari. Binti yao mkubwa, Malia (15) tayari ameshaingia sekondari.

“Michelle (50) kwa sasa ataendelea kuishi kwenye Ikulu ya Washington hadi Obama atakapomaliza muda wake wa urais ili tu aweze kuonekana kama yupo, lakini aliweka wazi kabisa kwamba wataishi maisha tofauti,” ilieleza ripoti hiyo ikimkariri mmoja wa vyanzo kutoka Ikulu hiyo. Ripoti hiyo ilikariri chanzo hicho kikieleza; “Michelle kwa sasa anaishi katika vyumba vya watumishi kwenye nyumba yao ya familia na anajiandaa kuchukua vifaa vyake na kuvipeleka kwenye nyumba yao binafsi ya Chicago”.

Taarifa nyingine ilieleza kwamba tayari mambo baina ya wanandoa hao yameshakuwa magumu kiasi kwamba wamekuwa wakiishi kwenye vyumba tofauti katika Ikulu ya Marekani.

Mgogoro wao

Barack na Michelle wamekuwa katika mgogoro kwa miaka kadhaa na wanalazimika kuwepo pamoja kwa sababu tu ya watoto wao na kulinda hadhi yake kisiasa. Lakini kwa sasa Michelle amekuwa mkali kweli kweli. Anaona kama amepuuzwa na kudhalilishwa mbele ya dunia nzima na amekuwa akipiga kelele akisema, “Nimevumilia vya kutosha”, taarifa zaidi zilieleza.

Kwa sasa Michelle anaonekana kupigania kukamilisha namna ya kupata talaka, lakini baadhi ya taarifa zinaeleza kwamba anafanya makusudi kuuchelewesha ili aweze kuukamilisha baada tu ya Obama kumalizia muda wake wa urais ambapo ataweza kupata Dola za Marekani 30 milioni kupitia mpango wa vitabu na zaidi ya dola 65 milioni kwa kuonekana hadharani.

“Kwa sasa Barack anaonekana kama amemwaibisha Michelle mbele ya dunia na kwa hili ni wazi kwamba atalilipa kwa gharama kubwa,” kilieleza chanzo kutoka Ikulu ya Marekani.

“Ni jambio lililo wazi kwa sasa kwamba Michelle ameshamwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye, japokuwa kwa sasa imekuwa ni suala gumu kwa kuwa anahitaji aendelee kuonekana wakiwa pamoja kwa sababu muhimu, lakini wanapokuwa nyumbani wanaishi maisha tofauti ya kutengana,” kilieleza chanzo hicho.

Iwapo taarifa hizo ni sahihi, hii inamaanisha kwamba Michelle ameudhika kupindukia na hii si mara ya kwanza jambo hilo kutokea miongoni mwao.

Tangu Obama alipochaguliwa kuwa rais, vitabu viwili vimemtaja vikidai kwamba wenza hao walikaribia kutengana katika kipindi cha miaka yao ya mwanzo ya ndoa na hata Michelle alifikia hatua ya kutaka kuomba talaka akidai kwamba anaona maisha yake ya kisiasa yanawanyima furaha na kuwa pamoja nyumbani.

Mwaka 2009 mwandishi wa siku nyingi wa Washington, Richard Wolffe alisema kwamba ndoa hiyo ilikuwa sawa na iliyovunjika miaka tisa kabla kutokana na harakati za kisiasa za Obama zilizokuwa zikimsababisha asiwe karibu na familia kwa muda mrefu.

“Kulikuwa na mawasiliano kidogo sana na familia yake na hata mapenzi yalipungua. Michelle alikasirishwa sana na hali hiyo akilaumu kwamba mumewe anaonekana kuwa mbinafsi; ilimpa wakati mgumu sana,” aliandika Wollfe.

Wakati huo Michelle alilazimika kutulia kwa kuwa tayari alishakuwa mama, mbinti zao awili, Malia na Sasha kwa sasa wana miaka 15 na 12. Mumewe ambaye walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa wakifanya kazi kwenye shirika moja la sheria mjini Chicago mwaka 1989, alikuwa ndiyo kwanza amechaguliwa kuwa Seneta wa Illinois na alikuwa akijipanga pia kuwania nafasi kwenye baraza la Congress.

Mke wa Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, Carla Bruni alipoulizwa katika moja ya vitabu kuhusu uzoefu wake wa maisha ndani ya Ikulu alijibu, ‘Acha kabisa! Usiulize ni kama jehanamu. Sikuwahi kuyafurahia’ ambapo Michelle alisema hakuwahi kuzungumza maneno ya aina hiyo.

Mwaka 2012 mmoja wa waandishi wa masuala ya siasa, Edward Klein alieleza kwamba Obama alionekana mwenye mawazo kupita kiasi, wakati ndoa yake ilipokuwa kwenye matatizo mwaka 2000 kiasi kwamba rafiki zake walihofu kwamba anaweza kujiua.

Alieleza kwamba Michelle alikuwa mwenye hasira kwa kuwa alimkataza Obama kuwania nafasi kwenye Congress, ushauri ambao hakuufuata na hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi.

“Baada ya kushindwa alirejea kwa Michelle kwa ajili ya kupata pumziko. Lakini Michelle hakuwa tayari kuonyesha huruma yoyote,” aliandika Klein aliyedai kwamba marafiki wa Michelle walimweleza kuwa tayari ameshafungua kesi akidai talaka.
-Mwananchi

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. So mr presidaa anamcheat fist lady duh hiyo kali kumbe kale kajamaa kakware haya bhana walipokutana sie hatukuwepo watajiju!

    ReplyDelete
    Replies
    1. If you believe what you are saying I GOT A BRIDGE TO SELL YOU ..

      Delete
    2. HABARI ni ya kweli maana ukishaona CNN FOX na TNX wana bleep ujue hapo

      Delete
  2. Shida zao,thats nothing he has killed n destroyed many,na wapate shida kabisa

    ReplyDelete
  3. Kama nini michele anitafute .mie napatika wingwi pemba.

    ReplyDelete
  4. HAITAKUWA AJABU KUTENGANA,KAMA WALITENDA DHAMBI INAANZA KUWATAFUNA.MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI NA MALIPO YANAANZA HAPAHAPA DUNIANI.WAANGALIE WALIPOJIKWAA WALEKEBISHE WAMTANGULIZE MUNGU ILI AWATIE NGUVU KWAKUWA YEYE MUNGU NDIYE MTAWALA WA DUNIA.

    ReplyDelete
  5. Njoo kwangu mimi mTZ hautalalamika kamwe.ntakuficha huku tandale mama utasahau maisha ya USA kabisaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmm we jamaa unatishaa utaweza kumpa ma lavidavi ya obamaaa kumshika viuno ol ze tym?? Hk tandale kwako......c majungu tuu yataendelea. .......bafu mita 15 kutoka nyumba ilipo mbaya zaidi la paspotsize...yy kazoea kwe mjisink wa maaaanaaa.hy endelea kujaribu bahati yk bhanaa.

      Delete
  6. HII NI STORY TU, TUCHEKE,MAGAZETI YAUZE BASI.WE UNAFIKIRI MAISHA YA HAO WATU NI SAWA NA WABONGO.WE LETE WEMA NA DIAMOND TUTAKUELEWA,TOFAUTI NA HAPO UNATUDANGANYA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bill Clinton aliye Mtia mtoto wa miaka 18 Monica lewinsky na kuzima sigara Kwenye uchi wake .Kennedy je?

      Delete
  7. mapenz ayachekwi kwan kila mmoja anajuwa hii kitu inavyo ungelewa dunian kote. mama obama una budi kumpenda uyo kijana unabid upunguze asila. asila asala mliwaze mwenzio akabiliane na majukum .na ww obama mpe maneno mazur mkeo na heshima asila zipunguwe .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Black America drama queen haoo

      Delete
  8. Hahahaha mdau 9:45 unanifuraisha saana

    ReplyDelete
  9. hayo ndo mambo ya wakubwa bwana!

    ReplyDelete
  10. Mapenzi hayana ukubwa kwa hiyo hata wao waweza achana tu

    ReplyDelete
  11. Hao ni watu wakubwa sana hapa duniani hayo mambo ya talaka yanatakiwa kufanywa japo na sisi vijana wa sasa tena ambao hatuna umaarufu kama wao wajirekebishe na hata kurudiana upya itakuwa aibu ya dunia hyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Obama defines marriage is btw people not man and woman

      Delete
  12. huyo ni shetani aliyeingilia ndoa yao na ashindwe kabisa, nawaombea hiyo migogoro itaisha tuuu...............

    ReplyDelete
  13. Kila zuri lina ubaya ndani yake kwa hiyo m nawaomba washauriane vema mambo yaishe jaman

    ReplyDelete

Top Post Ad