AKAMATWA AKIDAIWA KUUZA NYAMA YA BINADAMU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkazi wa Kijiji cha Kihinga, Kata ya Bugarama wilayani Ngara mkoani Kagera(jina tunalo), anashikiliwa katika kituo kidogo cha polisi cha kata hiyo baada ya kutuhumiwa kuuza kilo moja ya nyama ya binadamu kwa Sh100,000.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kihinga, Hassan Mohamed alisema kuwa jana saa mbili usiku, wananchi walipeleka fedha nyumbani kwake kununua nyama hiyo na alipowaona alikimbia na wananchi hao kwa hasira walimkimbiza ili kumuua na hapo hapo kuunguza nyumba yake.

“Mgambo ndio walimnusuru asiuawe na wananchi wenye hasira kali na alikimbizwa kituo kidogo cha polisi Kata ya Bugarama ili kuokoa maisha yake “.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa mgambo wa kijiji hicho, Emanuel Kaloli alisema wananchi waliandamana baada ya kusikia taarifa za kuwapo mtu anayeuza nyama ya binadamu na kutaka kuhakikisha ukweli huo.

Alisema baada ya wananchi kufika, walianza kumshambulia na kutaka kumuua, lakini wanamgambo wa kitongoji walifika kisha kumuokoa mtuhumiwa na hatimaye kumfikisha kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wake.

“Kijana aliyefahamika kwa jina la Man Balyamwabo mkazi wa Shina la Kalenge katika kitongoji hicho, ndiye aliyeambiwa kuwa angeuziwa nyama hiyo ya binadamu na kuleta taarifa katika uongozi wa kijiji ili uweze kuchukua hatua zaidia”.Alisema Kaloli.

Alisema nyumba aliyounguziwa pamoja na mali iliyokuwamo ndani hasa maharage, mavazi na vitu vinginevyo inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh2.6milioni. Pamoja na kuwepo kwa tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema mtuhumiwa inasemekana ni raia wa nchi jirani ya Burundi na alianza kuishi katika kitongoji hicho tangu mwaka 1981 kama kibarua wa kilimo kwenye mashamba.

Taarifa zinasema kuwa katika kuishi kwake na ndugu yake aliyefahamika kwa jina la Kahungu walikuwa wakituhumiana kwa uchawi na ilifikia mahala wakatofautiana na kaka yake ambaye alirejea kwao.

Polisi wilayani Ngara imethibitisha kumpokea mtuhumiwa huyo na kwamba linafanya mahojiano ya kina kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah mbona makubwa nyama ya binadamu tena jamani kweli hii dunia inakoelekea mwisho wake si mbali.

    ReplyDelete
  2. awataje wateja wake

    ReplyDelete
  3. Mdau umeongea pwenty ataje wateja wake.

    ReplyDelete
  4. daa inatisha sana

    ReplyDelete
  5. hii picha ni ya nyama ya ng'ombe aache uzushi

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha kuropoka , soma maelezo vizuri, umeambiwa ameuza kilo moja, yaani ilimixiwa kwenye hiyo ya ng'ombe fala usishtuke.

      Delete
  6. kumamake hao wanyarwanda hawafai huyo dawa yake ni kumfila mpaka ataje hao wateja wake

    ReplyDelete
  7. Duuuuuu miaka mitano ijayo cjui tutakuwa wap jaman kwa hali hiiii Ama kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho

    ReplyDelete
  8. Hii ishu ya kula binadamu huko kagera,niliickia kitambo kuna kabila( ).......... sio wahaya lkn,ndio tabia yake tena niliambiwa mkizika wenyewe wanaenda kufukua ile maiti wanafanya kitoheo,sema sasa kuna media haya mambo yanaanza fichuliwa.

    ReplyDelete
  9. Watu kama hao ni bora kuwaletea umende tu!

    ReplyDelete
  10. sio nyama ya binadam acheni uoga nyie

    ReplyDelete
  11. UGUM WAMAISHA NDIYO UNAO SABABISHA MTU AFANYEKAZI ZAAJABU

    ReplyDelete
  12. Jamani msifiche wahamiaji haramu hata mpangaji mpya akihamia toa taarifa polisi hakuna utu sikuhz watanzania turudishe uzalendo

    ReplyDelete
  13. Jamani msifiche wahamiaji haramu hata mpangaji mpya akihamia toa taarifa polisi hakuna utu sikuhz watanzania turudishe uzalendo

    ReplyDelete

Top Post Ad