AY AKANUSHA KUMTUNGIA NYIMBO JAGUAR...APINGA KUWA DIAMOND NI TISHIO KWAKE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa HipHop kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa nchini Kenya wa kumuandikia baadhi ya nyimbo mkali wa Kioo kutoka Kenya, Jaguar.

Katika mahojiano aliyofanyiwa nchini Kenya alikokuwa ameenda hivi karibuni, AY amesema hajawai kumuandikia wimbo wowote Jaguar na hata wimbo wao ‘Nimetoka Mbali’ kila mtu aliandika mashairi yake.

“Jaguar ni mmoja wa marafiki zangu. Tumefanya kazi pamoja na hakuna ukweli wowote kuhusiana na tetesi za mimi kumuandikia mashairi ukizingatia amekuwepo kwa muda mrefu kwenye gemu ya muziki hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wenye uzoefu wa kutosha na kufanya vizuri hata ukitazama ngoma niliyowahi kufanya nae ya Nimetoka Mbali, kila mmoja wetu aliandika mashairi yake kivyake hivyo huna haja ya kubisha kwa uwezo mkubwa alionao na naamini ni ushahidi tosha,” alisema.

Pia AY amepinga muziki wake kuathiriwa na Diamond kwakuwa kila mtu ana malengo yake katika muziki wake.

“Kila msanii ana mipango na mikakati yake ya kufikia malengo aliyojiwekea, sipo kujilinganisha na mtu yoyote, ushindani wangu ni kwa yule anayetaka kujaribu kutengeneza mkwanja mkubwa kushinda wangu, huo ndio ushindani wa kweli, hata hivyo siwezi kuwa juu milele.”

Source:Bongo5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nani ana mkwanja zaidi kai ya platinum na AY,,???

    ReplyDelete
  2. Ay yupo juu pia anamkwanja wa kutosha, nivile tu hapend kujionyesha, domo yeye zake sifa kila anachofanya lazima kila mtu ajue ulimbukeni mwingi

    ReplyDelete

Top Post Ad