CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE KUFUTA KAULI YAKE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa jumuiya za kimataifa.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga amani ndani ya nchi.

Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.

“Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga amani nchini,” alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya malalamiko yao.

Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na alihoji kwanini awatake WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala ya kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo ni polisi na majeshi na mahakama.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tushawazoea chdma...wafa maj hamkos kutapatapa....na bado mwaka huu mtaomba poo...nlishaahid nchi haitatawalika bas tulien muone power ya baba ritz frm magogoni.....mtapigwa sana mpaka muache tabia zenu za kishoga km lema

    ReplyDelete
  2. Yeah kaka walipotangaza nchi nzima kwamba TUTAFANYA NCHI ISITAWALIKE walisikia kwamba watashtakiwa jumuiya ya kimatifa?fake politician utawajua Tu.wamesahau na maneno Yao mengi.mpeleke mwenyekiti wako jumuiya ya kimataifa kwanza

    ReplyDelete
  3. Piga chadema hao

    ReplyDelete
  4. Acheni kushabikia upumbavu unaposema piga chadema unamaanisha hata kma bb yako ah babh yako kule waliko nao wapigwe mbo a mnakosa akili haya ya raisi ni sawa na yale ya waziri mkubwa aliporopoka watu wapigwe na vyombo vya dola mbona mnakua kma mijuc msiofikiria mbele kuna nini na pia kwakuwa hamfikirii mnaona kupiga na kuforce mnayoyataka nyie ndo babu kubwa mnaweza kupiga ndio na mkaua ila hamtaweza kuuwa mtu jambo alilosimamia litabaki pale pale

    ReplyDelete
  5. ni sawa na kumwambia baba yako mzazi funga kopo lako shwain wewe huna adabu afute vipi kauli yake kuwa na adabu chadema

    ReplyDelete
  6. Chdm ni manyani hawaoni mikundu yao.wakisema wao sio kosa wenzao inakua isue.

    ReplyDelete
  7. We need peace and happiness .God bless USA

    ReplyDelete
  8. Chadema acheni siasa za kitoto, watanzania sio wapuuzi kama mnavyozani, now tumewachoka.

    ReplyDelete

Top Post Ad