EXCLUSIVE..JIDE AOMBA TALAKA, GARDNER APATA MSHITUKO..AELEZA KILA KITU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori:  Shani Ramadhan
UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuripoti mkasa wote.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya kutangazia redio moja nchini Kenya.
HABARI KAMILI
Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo.
“Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.
“Pia katika safari ya kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo hicho.

JIDE AHAMAKI
Chanzo kikatoboa kwamba Gardner alipofika nyumbani kwake na kumweleza mkewe, alikumbana na kitu ambacho hakukitarajia.
“Komando (Jide) alihamaki na kumjia juu akisema yeye hawezi kuondoka Tanzania kwenda kuishi Kenya, kama Gardner analiona jambo hilo ni heri kwake, amuandikie talaka yake na kuachana ili kila mmoja achukue hamsini zake,” chanzo kilizidi kuporomosha maneno.
KWA NINI JIDE HAKUPENDA? 
Habari zilizidi kuanikwa kwamba Jide au Binti Machozi alifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa kitendo cha kwenda kuishi Kenya kitaua bendi yake ya Machozi na sehemu ya biashara ya Nyumbani Lounge iliyopo Ada-Estate, Kinondoni, Dar.
MBAYA ZAIDI
Taarifa zikazidi kumiminika kwamba, mbali na Jide au Anakonda kuhofia biashara zake kufa, lakini pia hakupenda Gardner aondoke hata peke yake kwa sababu yeye ndiye meneja wa miradi hiyo miwili.
“Mimi nilipopata habari hizo nilikutana na Jide nikamuuliza, akanijibu ameamua iwe hivyo tu, kikubwa mumewe (Gardner) aamue moja kati ya hayo mawili kwani yeye ana haki akiwa kama mkewe wa ndoa,” kilisema chanzo kikimkariri Jide.
GARDNER AISHIWA NGUVU
Kufuatia majibu ya mkewe, taarifa zinasema mtangazaji huyo ambaye alishawahi kupiga mzigo kwenye kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar alijikuta akiishiwa nguvu na kuachana na dili hilo mara moja.
“Gardner alisalimu amri kwa mkewe, akaamua kuachana na dili la kwenda kutangaza Kenya. Lakini alifikiri sana akasema ni kweli kuhamia Kenya kungeua miradi yao ya Tanzania maana ingekosa msimamizi wa kuaminika,” chanzo kiliweka wazi.
KAMA ANGEKWENDA KENYA 
Siri hiyo iliyovujia mikononi mwa Ijumaa Wikienda haikuishia hapo, ilizidi kuanikwa kwamba kama Kapteini angekwenda Kenya na kuanza kazi, ilikuwa alipwe mshahara wa shilingi za Kenya laki 3 kwa mwezi (kama milioni 6 za Tanzania).

NAFASI YAKE BADO IPO
Mpashaji wetu alisema kwamba nafasi ya Gardner kwenye kituo hicho cha redio ambacho hakikutajwa, bado ipo lakini tamko la Jide nalo li hai, kwa vile hakubatilisha, endapo mumewe atataka kwenda hata kesho (Jumanne) aandike talaka.
WIKIENDA NA GARDNER
Baada ya kunyetishiwa taarifa nzima, juzi gazeti hili lilimsaka Gardner. Kwa njia ya simu lilimkosa, likamfuata Nyumbani Lounge. Lilipomkuta lilimsimulia kisanga chote cha ndoa yake kutikiswa na kitendo cha yeye kupata kazi Kenya ambapo alijibu hivi:
“Ndoa ni nzuri, ni kweli ilikuwa niende Kenya, nilipata kazi kule lakini kama familia ilikuwa lazima tukae na kupanga, mwenzangu hakuafiki.”
Wikienda: “Ni kweli shemeji ameomba uchague mawili, umwandikike talaka au uende Kenya?”
Gardner: “Ndiyo maana nimesema ndoa nzuri, lazima makubaliano yawepo, mke anaweza kuonesha msimamo wake na mume kama utakaa chini na kuufikiria ukapata jibu unakubaliana na mke wako wala hakuna ubaya.”
Wikienda: “Kule mshahara wako ungekuwa shilingi ngapi?”
Gardner: “Hiyo sasa ni siri ya makubaliano.”
Wikienda: “Kwa nini usiamue kwenda tu?”
Gardner: “Nimekwambia ndoa nzuri.”
JIDE BIZE
Juhudi za kumpata Jide ziligonga mwamba baada ya muda wote kuwa bize na shoo ya kukata na shoka aliyokuwa akiifanya siku hiyo kwenye ukumbi huo akikimbiza na nyimbo zake kali za zamani na hizi mbili zilizogeuka nyimbo za taifa, Joto Hasira na Yahaya.
RAFIKI WA GADNER AMCHAMBUA JIDE
Rafiki wa karibu na Gardner (jina tunalo) ambaye alisikia mahojiano ya mtangazaji huyo na Ijumaa Wikienda, alisubiri jamaa aondoke ambapo alianza kumchambua Jide.
“Nataka kuwaambia kitu, Jide ni mwanamke jasiri sana. Ana msimamo na anaposhikilia msimamo wake hatengui hasa kama atabaini kuwa yupo sahihi.
“Ni kweli jamaa (Gardner) alipata kazi Kenya tena mshahara mzuri tu, lakini mama (Jide) akaweka ngumu hakuna kwenda,” alisema rafiki huyo.

CREDIT: Global Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

27 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata sasa ameamua jambo la busara kwani huyo mumewe alikuwa mbinafsi hakufikiria kazi na biashara ya mwenzake,nampa jide pongezi kwa uamuzi mzuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. WANAUME hawana mpango .wanaume wamefilia

      Delete
  2. Wewe Gadner vipi?kukaa kote na mkeo,9 years hukuona umuhimu wa kumuhusisha mapema katika process zako,unasubiri mpaka last minutes umzoe kama mzigo? Big up lady...

    ReplyDelete
  3. wewe muandishi acha habari za uongo kuna siku mtakuja kufungwa nyie wajinga msione watu wanawanyamazia mkajua mmeyapatia maisha watu wanawavutia kasi. badala ya kuandika vitu vya maana unaandika huu uouuzi, tanzania mwenye hela ataendelea kuwa na hela maskini atabaki maskini wajinga wengi sana. upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  4. Mikundu nyi mmetuambia laki tatu za kenya,ambaz6 ni 6milion za tz,baadae tena mmemuuliza gardner akatosa kasema mshahara ni siri yake,nyie nani aliwaambia hicho kiwango? Nyambafu zenu.

    ReplyDelete
  5. hivi jide ana watoto wangapi?

    ReplyDelete
  6. 11:56 uko ktk sensa?????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimependa hilo jibu. Yeye yanamuhusu nini kama si umbea akishajua vimsaidie nn yy. Kupata ni majaliwa na kukosa ni majaliwa ya Mungu.

      Delete
    2. nimeuliza kwa nia njema tu

      Delete
    3. HAHAHAHHA NIMEPENDA JIBU @ 12:12 LOL

      Delete
    4. hahahaaa watu wana majibuuuu... big up mwanamke mwenzangu wewe jasiri na nakukubali mno

      Delete
  7. power of a woman. much salute to gardner. naheshimu mwanaume anayefanyia kazi mawazo chanya ya mke wake. i admire this couple.

    ReplyDelete
  8. Uandishi wa bongo wa kipumbavu sana

    ReplyDelete
  9. Ukikubali kuolewa sharti ulale bila chupi

    ReplyDelete
  10. wewe mwanamke hapo juu akili yako imesab..yaan jd kuomba gwasuma umefulah kwahiyo hutaki waendelee zaidi au wivu unakusumbua.

    ReplyDelete
  11. Maneno yanaumba my dear. One day yes. Umetamka mwenyewe talaka. Usije pata bp siku kakangu atakapokuandikia chezea kaka gad ww, rombo moja.unatishia yau halafu wifii nenepa kidogo basi unajikondesha sn

    ReplyDelete
  12. Gardner kashasema ndoa tamu .nawapa big up kwa conclusion nzuri

    ReplyDelete
  13. Nimefuatilia sana habari hii, nashangaa sana, ningependa tu kuwafahamisha watanzania na mashabiki wetu, binafsi sijawah kufuatwa na mwandish yoyote, habar hii ni ya uzush mtupu na imetungwa, nimeifikisha ngaz ya sheria ili kuilinda hadhi yangu na ya mke wangu.

    ...Gardner G. Habash

    ReplyDelete
  14. Kama kweli wewe ni Gardner inabidii uwashikishe adabu hao waandishi wa magazeti wana kera sana na habari zao za uongo na kuzalilisha watu bila sababu.

    ReplyDelete
  15. Gadner kamata wote buluza kortini hata hawa washakunaku wa udaku special nao mataahira tu.

    ReplyDelete
  16. Mambo ya ndoa za watu, ninyi wa magazeti yanawahusu nini? Tafuteni habari acheni umbeya.... pambaf zenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad