FACEBOOK WAINUNUA WHATS APP, WAMILIKI WAWA MABILIONEA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


San Fransisco. Mtandao wa kijamii wa Facebook umenunua programu ya huduma za meseji ya WhatsApp kwa dola za marekani bilioni 19 (TSh 30.9 trilioni) katika taarifa iliyotoka mapema leo.
Ununuzi huo wa WhatsApp umetengeneza mabilionea wapya angalau watatu, akiwemo mwanzilishi wa WhatsApp, Jan Koum, ambaye atajiunga na bodi ya wakurugenzi ya Facebook.
Mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Brian Acton, naye anaingia katika orodha ya mabilionea wapya vijana.
Miaka 4 iliyopita, Acton alijaribu kuomba kazi Facebook na Twitter baada ya kupunguzwa kutoka Yahoo, inaripoti blogu ya teknolojia ya Techcrunch.
Hakufanikiwa.
Leo hii, program aliyoitengeneza na rafikiye wa Yahoo, Koum, inagombaniwa na kampuni zilezile zilizomkataa na hatimaye, imenunuliwa kwa mabilioni ya dola na Facebook.
Wengine walioula ni wawekezaji wa kwanza wa WhatsApp toka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia.
Techcruch inaripoti vijana wa Sequoia wametengeneza zaidi ya dola bilioni 3 (TSh 4.9 trilioni) – mara 50 ya pesa waliowekeza – katika ‘dili’ hilo.
Facebook, ambao ni mtandao mkubwa kuliko yote duniani ukiwa na wanachama zaidi ya bilioni 1, inaamini kuwa WhatsApp itasaidia kuongeza uwepo wake katika masoko mbalimbali duniani, hasa katika nchi zinazoendelea Afrika, Asia na Amerika Kusini ambapo teknolojia ya simu za mkononi imeshika hatamu.
Uamuzi huo unaipa Facebook nafasi ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake, itarithi zaidi ya watumiaji milioni 450 wa WhatsApp.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg anaamini uamuzi wa kuinunua WhatsApp kwa dola bilioni 19 ni wa busara, kwa kuwa “[WhatsApp] ni mtandao unaokuwa kwa haraka, ambayo itafikia watumiaji zaidi ya bilioni moja hivi punde.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad