FAIDA ZA WABEBA MABOX WAISHI NCHI ZA NJE KAMA UK KWA UCHUMI WA TANZANIA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

wabeba boksi ni wa Tanzania wanaoishi ughaibuni, wakifanya kazi za mikono, kama vile kubeba na kupanga mizigo ya bidhaa madukani, kusafisha maofisi, kusafisha vyombo mahotelini, kuwatunza wazee, na kadhalika. Watanzania wanaposema kubeba boksi, wanamaanisha kazi za aina hiyo. Na jina hilo linatokana na huu kweli kuwa wengi wa wahusika wanabeba na kupanga maboksi.

Wabeba boksi wanataniwa sana katika jamii ya kiTanzania. Wabeba boksi wengi nao wanajitania. Watanzania wengi wanaziona kazi za boksi kuwa ni kazi duni. Napenda kubadili mtazamo huo kwa kuelezea umuhimu wa boksi. Natumia hilo neno boksi kwa sababu linatumika pia kumaanisha kazi ya kubeba boksi.

Jambo moja la msingi ni kuwa wabeba boksi wanatumia nguvu zao kujipatia kipato. Wao ni tofauti na wezi au mafisadi, ambao wanakula jasho la wenzao. Kwa msingi huu, mbeba boksi anastahili heshima.

Kila kazi halali ina umuhimu wake katika jamii, iwe ni kilimo, uvuvi, usafishaji vyoo, ualimu, udaktari, au upigaji muziki. Kila kazi ya aina hiyo inastahili heshima. Mpiga boksi anafanya kazi muhimu. Bila yeye, jamii itakwama. Anastahili heshima.

Wabeba boksi, kama vile walivyo waTanzania wengine wanaoishi ughabuni, wanatoa mchango mkubwa katika kipato cha Taifa, kwa hela wanazotuma nyumbani, iwe ni kwa ndugu, jamaa, marafiki, au taasisi. Nimesoma taarifa kuwa mwaka 2008, kwa mfano, watu hao waliliingizia Taifa dola zaidi ya 100 millioni. Wenzetu waKenya wanaoishi nje waliingiza nchini mwao dola zaidi ya 400 millioni. Ni wazi kuwa mbeba boksi, akiwa ni mmoja wa watu hao, ni mtu muhimu kwa uchumi wa Taifa. 

Je, lipi bora zaidi: kukaa vijiweni nchini bila ajira, au kubeba boksi? Hili ni suali la kutafakariwa.

Kuna wabeba boksi ambao, baada ya kukusanya hela, wanaanzisha miradi nyumbani wakiwa bado ughaibuni, na wengine wanarudi nyumbani na kuanzisha hiyo miradi. Kwa njia hiyo, wanatoa ajira kwa wananchi wenzao.

Mpiga boksi, kwa kukaa ughaibuni, anajifunza mengi. Anarudi nchini akiwa na upana wa mawazo kuhusu dunia na uzoefu wa nidhamu ya kazi, vitu ambavyo vinaweza kutoa changamoto kwa wananchi wengine.

Kwa ufupi, boksi lina umuhimu na heshima yake.

ngoja. niwape mfano mnaweza na nyie kufungua
www.diasporamessenger.com/kenyans-abroad

kenyans living abroad sent back home ksh 110.76 billion. ( $ 1.29 billion) na hii ni mwaka jana pekee hizo ni zaidi ya Trillion 1 za Tz

Money Stunna From JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mi ni msichana ninaejituma,nimetuma kwenye account yangu pesA si chini ya million 30.kwa umri wangu hizo hela kwangu ni nyingiiii nimenunua gari,natunza wazazi kila mwezi nadondosha vipound kwa wazee,uingereza ndo mpango mzimaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na hapo sichuni mabuzi ni hela ya kazi za mikono yangu.

      Delete
    2. Natuma dollar 1000 kila mwezi nyumbani .dollar 1000 ni mshahara wa nani bongo?

      Delete
  2. bola nibebe box kulikoni kumtegemea mtu au kukaa bule maskani na wengi tushajenga tuna magali na maisha yetu mazuli kulikoni walio wengi huko bongo

    ReplyDelete
  3. KUNA WATU BONGO WANAOJITUMA KUFANYA KAZI,NA KUNA WENGINE WANAANGAIKA KUTAFUTA KAZI BONGO HAWAPATI KAZI,HATA INGEPATIKANA YA KUBEBA BOX WANGEBEBA,,,,MAISHA HOME NI MAGUMU SANA,,MTU ANAKUWA NA KISOMO CHAKE,LAKINI KAZI HAPEWI WANAPEWA WALE WANAOJULIKANA KWA WAKUBWA,,,,KWA KWELI NYUMBANI BONGO KUNA UBAGUZI SANASANA,,,
    HAPA ULAYA UNAPEWA KAZI KULINGANA NA ELIM YAKO,,
    NA PIA HIYO WANAYOSEMA KUBEBA MABOX,KULEA WAZEE,UJENZI KWA UJUMLA KAZI ZA MIKONO NDO ZINAZOLIPA HUKU ULAYA,SIO KAMA HUKO NYUMBANI UKAE KATIKA KITI UPULIZWE NA KIYOYOZI NA MWISHO WA MWEZI UPOKEE LAKI3,LINI UTAJENGA WEWE?ZAIDI ZAID UTASHINDANA NA WENZAKO KWA KUENDESHA GARI ZURI BARABARANI...NDO MAANA WENGINE WAMEAMUA KUJITOSA CHINA NA MADAWA YA KULEVYA..
    PIA WATZ TUSIWE NA ROHO YA KWA NINI,,NASIKIA RAIYA WENGI HATUTAKI WANAOISHI UGAIBUNI WAWE NA RAIYA MBILI,,,HIVI MTU AKIWA NA RAIYA MBILI ANAKUPUNGUZIA NINI WEWE MZALENDO??? KWA NINI MZAWA WA TZ ASIWE NA RAIYA MBILI,YA HUKO ANAKOBEBA MABOX NA YA ALIKO ZALIWA,ILI AKIMALIZA KUBEBA MABOX AJE KUJIPUMZIKIA NYUMBANI KUUNYOSHA HUWO MGONGO WA MABOX

    ReplyDelete
  4. kazi ni kazi ilmrad ni halali.Sisi huku bongo elimu unayo kazi unatembea mpaka unaona dunia haina huruma.Kazi bongo zinaenda na msemo "It doesnt matter what you know but who you know"Ni kujuana tu ndo unapata kazi kama humjui mtu basi unajihesabia maumivu.So kheri yenu nyie mnaoingiza pesa..heshima kwenu.

    ReplyDelete
  5. mimi niko dar nataka nije ulaya..ntafanyeje...nchi gani hi ya shida hivi hamna future nimesoma nina masters ila salary ndogo sana.me bado mdogo nina nguvu naweza fanya kazi yeyote ya mikono na ya akili.am very fluent in english.am a maried women with two kids. 29 years

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dollar 11 kwa saa masaa 12 kwa siku 7 au 5 kwa week uta pata kiasi gani? It's a lot of money .Tanzania nyuma Sana bado wanaoa mini education is more important than having skills.

      Delete
  6. Me ni msichana wa umri wa miaka 27,naomba niunganishwe na watu walioko huko ulaya nije nifanye kazi hizo.ninaelinu ya degree.plz nipo tayali kudeki na kuosha vyombo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe kuna Kazi zaidi ya hizo . Bena box ni jina tu.Kwanza box Kama Hilo kubeba dollar 2O kwa saa na ukiumia m gongo wanaogopa lawsuit wanakupa vifaa na kusema ukweli sijaona mtu akibeba Hivyo .

      Delete
  7. roho inauma navyoona wasomi wenye degree na masters wanateseka tanzania nyumbani.mm niko middle east unapokaa na waarab wanakwambia nchi yenu ni tajiri sana kwann nyie ni maskini? tanzania ya leo kama humjui waziri kazi nzuri hupati.njooni dubai kazi zipo..qatar na saudia.mjue english vizuri tu kazi unapata

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli? Sasa inakuwaje mpk nikafika huko? Me ndie niliyetoa coment hapo juu 3:16

      Delete
  8. tusaidieni tuje huko.kweli tz bado.pia urasimu mwingi sana.me nataka kija huko.nina degree.poa hata niogeshe wazee nipate ela niwekeze huku inisaidie for future

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo ya wazee wanaonjesha chumvj.Actually my first job ilikuwa nursing home hata Huyo January makamba nursing home kafanya Kazi .Kummwamusha Mzee kumkumbusha apige mswaki na avae .Dollar 600 kwa week times 4 dollar 2400 .Million ngapi shillings Nyie potezeni Muda tu huko

      Delete
  9. Mcitake kudanganya wa2 nyinyi wabeba box . Watu tumeishi Europe miaka mini . I'm talking 2 my experience nimekaa London 5 yrs nilienda kusoma maisha ni magumu sana ukikutana na wa2 kama wamechanganyikiwa full stress Wabongo wamepauka mpaka ukikutana nae anakula kuna. Watu wengi wanaongangania ulaya hawana elim anaishi maisha ya dhiki sana ameshapoteza muda kurudi bongo anaona aibu wenzake aliowaacha wako mbali kimaisha mifano 2nayo mingi ndugu zetu kila siku wako huko wengine wanalia maisha magumu. ukiwa na akil bongo maisha mazur haya na ubaguzi ila ukiwa mvivu utataka kwenda nje. wa2 kibao wamekaa abroad Wamerud hawana mbele wala nyuma wanaanza kuomba misaada ndugu zao hapa nyumban.Ulaya ilikuwa Zamani Enzi za kina nyerere waliopelekwa kusoma ndo walifaidika wali Rudi na magar na kujenga majumba na degree zao . sasa hiv wanaoenda abroad hata kusoma hawasomi wanarudi bila vyet hali ngumu. kazi zenyewe hakuna wanapeana mi polish 2 . bongo life tambarare ukipatia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao ni wanaoenda ulaya na kutaka kuishi Kama Bill gates Lazima yatakushinda.wewe unaenda USA unaanza kulipia Gari ili watu wakuone ,neighbourhood gani unaishi na zip code,na sifa tebetebe.Mfano Haya take home 2400 dollar kwa mwezi ( Gari ku finance plus insurance 600 dollars ,rent 800,umeme 150,Simu 150,cable 220,chakula,kuvaa Lazima uzidiwe

      Delete
  10. aisee5:24 unanikatisha tamaa.huku bongo mbona shida sana jamani.magojwa yanayotibika watu wanakufa tecno....ipo chini sana.government mafisadi tu masikini anaendelea kuwa chini daily anampa mtoto wake elimu ya kayumba mtoto anashidwa kucompete exams na wa school bus so anafeli maisha yanaendelea kuwa magumu sana.so tukisikia nje kidogo kuna unafuu ndo tunataka twende sasa wewe umenishtua na kunikatisha tamaa.sasa tumuamini nani..mimi sina ndugu wala rafika alieenda ulaya nimuulize...nashidwa nimuamini yupi.anaesema kula ela huko au anaesema hamna kitu wabongovwamepauka..na nyie mlio huko tupeni proces tuzianze kama itawezekana jamani

    ReplyDelete
  11. Ulaya kwanza isake education. na uzoefu wa kazi, hapo poa kabisaa,utafanya mambo yako mengi tu kwanza hakuna urasimu, muhimu uwe mchapa kazi yako na makini na kazi yako

    ReplyDelete
  12. ntapataje hiyo ya kiwaamsha wazee asubuhi...hata kueaogesha no problem.am ready

    ReplyDelete
  13. Jobs Foreighners.com.Good luck

    ReplyDelete
  14. ok.thnx.let me try now

    ReplyDelete

Top Post Ad