KESI YA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI MWANGOSI YANGURUMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam na Iringa. Kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi inayomkabili aliyekuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mwenye namba G. 2573 Pacificus Cleophase jana ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa mmoja kati ya 11 wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi, Longishu Losingo (29) amelalamika kuwa wanalishwa mchuzi wa maharage gerezani.

Kesi hiyo ya Mwangosi inasikilizwa na Jaji Mfawidhi, Mary Shangali.

Wakili wa Serikali, Adolf Maganda alidai kuwa mtuhumiwa Cleophase ambaye alikuwa askari polisi mkoani Iringa alifanya mauaji hayo Septemba 2 mwaka 2012 katika eneo la Nyololo, wilayani Mufindi.

“Mshtakiwa alitenda kosa hilo wakati alipokuwa akiwaamuru wafuasi wa Chadema kuondoka katika eneo la tukio walipopanga kufanyia mkutano,” alidai.

Maganda alidai kuwa katika tukio hilo, mtuhumiwa alifyatua risasi na kumpiga marehemu.

Wakili huyo alidai kuwa wafuasi wa Chadema walifika katika eneo hilo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano ambao katibu mkuu wa chama hicho alikuwa anatarajia kuhutubia.

Alisema mkutano huo ulikuwa ufanyike licha ya polisi kuwaandikia Chadema ikiwataka wauahirishe ili kupisha zoezi la sensa.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kuzuiwa kufanya mkutano, wafuasi wa chama hicho walianza kurusha mawe na kuwaumiza baadhi ya askari polisi, hatua iliyowalazimisha kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya kuwasihi kutokufanya mkutano huo.

Maganda alidai kuwa mshtakiwa akiwa na bunduki alikwenda katika eneo la tukio alilokuwa marehemu na kufyatua risasi na kumpiga marehemu ambaye alikufa papohapo. Alidai kuwa taarifa ya daktari inaonyesha kuwa kifo cha Mwangosi kilisababishwa na kupatwa na majeraha yaliyotokana na mlipuko mkali.
Credits:Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumanyoko cdm na kuandamana iyo vi?

    ReplyDelete
  2. Sasa apo mnachanganya mambo uyo anaesoma hayo mashtaka amesoma shule gan au ndo mnataka haki isitendeke manake apo kwenye maelezo mwanzoni anasema mshtakiwa alfyatua risasi alafu report ya daktar marehemu kafa kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko mkali tangu lini bomu likafanana na risasi jaman muogopen mungu kwa kuuwa watu alafu mnapindisha maelezo kwanza ninavyojua procedure za mahakama mpaka hapo judge atakuwa na hukumu yake tayar cos maelezo hayaeleweki

    ReplyDelete

Top Post Ad