KOCHA WA AL AHLY AICHAMBUA YANGA KAMA KARANGA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Kocha Msaidizi wa Al Ahly, Ahmed Ayoub ameichambua Yanga kwa kusema ni timu bora katika kushambulia, lakini si nzuri kwenye safu ya ulinzi.

Yanga itaivaa Al -Ahly Jumamosi hii katika pambano la raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mahojiano na mtandao wa klabu hiyo, Ayoub alisema, ushindi wa jumla ya mabao 12-2 ilioupata Yanga dhidi ya Komorozine ni uthibitisho kwamba safu yake ya ushambuliaji ni moto wa kuotea mbali.

Katika michezo 17 ya Ligi Kuu Tanzania Bara safu ya ushambuliaji wa Yanga imefunga mabao 41 na kuruhusu mabao 12 hadi sasa.

“Yanga ina safu ya ushambuliaji yenye nguvu kwani imefunga mabao 12 katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa ilipocheza na Komorozine ambayo matokeo ya jumla ni 12-2,” alisema Ayoub.

Aliongeza: “Ina kikosi chenye nyota watano wa kulipwa kutoka Congo, Rwanda, Burundi na Uganda ambao wana mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji.”

Pamoja na kusifia safu ya ushambuliaji ya Yanga, kocha Ayoub alisema atatumia udhaifu wa ngome ya ulinzi kupata matokeo mazuri.

Alisema beki ya Yanga si imara kwani haina ushirikiano wa kutosha miongoni mwa wachezaji wake husika.

“Timu ya Tanzania ina udhaifu katika eneo la ulinzi ambako kimsingi hakuna muunganiko mzuri wa wachezaji wanaocheza eneo hilo,” alisema Ayoub.

Kocha huyo alishuhudia pambano la kwanza kati ya Yanga na Komoriozine lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Kauli ya kocha huyo ni changamoto kwa Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm kwani ni wazi anatakiwa kuisuka kikamilifu ngome yake ya ulinzi kabla ya mchezo kati yake na vigogo hao wa Misri.

Safu ya ulinzi ya Yanga inaundwa na mabeki wa kati Kelvin Yondani na Nadir Haroub pamoja na mabeki wa pembeni Oscar Joshua anayecheza kushoto na Mbuyu Twite kulia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mwaaaarabu subiri kichapoooooo!! ila angalia tu usijekula za wiki!!!! utaibika Mwaaarabu!!!

    ReplyDelete
  2. Endeleeni kujidanganya nyie Yebo yebo lkn muda utazungumza Jpili lugha zitabadilika

    ReplyDelete
  3. mgogoro wa yanga unaanza jpili maana kawaida yao wakifungwa waanza kutafutana ubaya

    ReplyDelete
  4. nyie mnaojibu huku ni azam nini? maanake nyie kama ni simba mnatakiwa kukaaa kimyaaa, sababu nyie ni marehemu, mechi nne pointi mbili!!! hamko ligi moja na Yanga nyie!! wanajeshi wanakusubirini!!!

    ReplyDelete
  5. ALBADIR FC nyie endeleeni kununua jezi za waume zenu al ahly.

    ReplyDelete

Top Post Ad