LEMA CHUPUCHUPU KUTIWA NGUVUMI BAADA YA KUANDIKA UJUMBE WA KUMPONDA JK

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema jana alinusurika kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi ili kuhojiwa kutokana na ujumbe wake aliouposti kwenye mtandao wa kijamii akiandika: “Rais Kikwete mbona umeamua kuliangamiza taifa.”

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la Katiba, Lema alisema maafisa wawili wa polisi walimfuata katika hoteli aliyofikia Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata na kumpeleka makao makuu ya polisi.

Lema alisema maafisa hao, ambao walikuwa wanatumia gari dogo, baada ya kufika hotelini hapo, waliomba aitwe na aliposhuka walimtaka kuandamana nao, hadi makao makuu ya polisi kwa mahojiano.

“Niliwauliza nikaandeke maelezo juu ya nini, walijibu kifupi wao ni chombo cha dola na walisema wametumwa na viongozi wa juu wa polisi na hawakuwa tayari kutaja tuhuma zangu,” alisema Lema.

Alisema baada ya polisi hao kusisitiza kutaka kumchukua, aliwaomba aende chumbani kujiandaa kabla ya kuwasiliana na viongozi wa chama chake na familia yake.

“Niliposhuka chini sikuwakuta na ndipo nikashauriana na viongozi wa chama hicho na kuamua kuondoka jana mchana Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Hata hivyo, alisema Chadema leo wanatarajia kutoa tamko juu ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wanachama wa CCM kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani hasa pale wanapodaiwa kupigwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Angalia wasije kukunyofoa macho na kukung'oa kucha kwa kutumia bisibisi.

    ReplyDelete
  2. kamanda Mungu yupo pamoja na wewe, hakuna amshindaye Mwenyenzi Mungu, tunakuombea.

    ReplyDelete
  3. Acha uongo wewe mtu yoyote hawezi kukamatwa kama kuku lazima wangekuja na kibali na usinge bisha waongopee wajinga wenzako,na wangekutaka hata hukohuko dom wangekukamata tu.

    ReplyDelete
  4. Dah kweli ndugu yangu jamaa limejitungia halafu mbona watu wanaishupalia kauli ya Kikwete ya kuondoa unyonge kwahiyo mlitaka wawe mandondocha hicho kitu hakuna mkianzisha vurugu jibu lake ni vurugu mtakoma mwaka huu mtatengeneza drama mpaka mkome

    ReplyDelete
  5. hii bongo baba, aliyekuambia mpaka kibali cha kukamatwa kitoke ni nani!! utabaki hivyo hivyo ndondocha!!

    ReplyDelete
  6. Wananchi tumeshakuchoka na upuuz wako..

    ReplyDelete
  7. Ukimwaga ugali mimi namwaga mboga ngoma droo hongera sana baba kikwete.

    ReplyDelete
  8. cjaona ht cha mana cha kuandika hp mmekosa habr zakutuandikia

    ReplyDelete
  9. chama cha vibaka, chadema.

    ReplyDelete
  10. huyo lema anatafuta umaarufu tuu nyambavu zake serikali haishindwi kumkamata km kweli ingemuhitaji hata ajifiche wapi angedakwa tuu sasa km hana la kuongea aende akabembeleze watoto nyumbani

    ReplyDelete

Top Post Ad