MBWANA SAMATTA AMWAGIA SIFA KEDE KEDE MRISHO NGASSA LIGI YA MABINGWA AFRICA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshambuliaji wa kimataifa mtanzania anayekipiga  TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mtanzania Mbwana Samatta, amesema Mrisho Ngassa wa Yanga amefanya kitu cha maana kwa kupiga ‘Hat-Trick’ mbili mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Samatta alisema idadi hiyo ya mabao si kazi rahisi kwenye mashindano makubwa kama hayo.
Yanga iliifumua Komorozine ya Comoro mabao 12-2 na kuiondosha kwenye mashindano na sasa itaikabili Al Ahly ya Misri ambayo Samatta amesema si timu ya ajabu lakini si laini kama hakuna mipango ya maana.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Lubumbashi, Samatta alisema: “Mabao sita ni mengi sana kufunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ni dalili nzuri kwake na kwa timu.
“Pia yanaashiria mambo mazuri kikubwa, lakini asibweteke kwani anaweza kufanya kitu kikubwa katika mashindano hayo endapo Yanga itafanikiwa kusonga mbele.
“Ngassa ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu, kwangu sioni kitu cha ajabu sana kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja kwa sababu nafahamu uwezo wake, lakini inaashiria pia kwa sasa yuko vizuri sana kimwili na kiakili.”
Kuhusu Yanga na Al Ahly, Samatta alisema: “Al Ahly ni timu kubwa na kama ulivyoona ni mabingwa, lakini mpira ni mchezo wa ajabu, nina imani kama Yanga watajituma, wanaweza kuwavua ubingwa na wao wakasonga mbele.”
Mazembe nayo imo kwenye michuano hiyo na inajiandaa na mechi dhidi ya Astres de Douala ya Cameroon. Kuhusiana na mchezo huo, Samatta ameweka wazi kuwa maandalizi yao ni ya nguvu.
Story kwa hisani ya Mwanaspoti
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad