MGOMVI WA MKE WA ZUMA KUREJESHWA TANZANIA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Mtanzania Stephen Ongolo anayekabiliwa na madai ya kutishia kutoa siri za mke wa Rais Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli (MaNtuli), huenda akarudishwa nchini na kuzuiwa kuitembelea Afrika Kusini milele.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Tawi la Uchunguzi wa Kesi, katika Jimbo la Kwa Zulu-Natal, Brigedia Clifford Marion, wakati kesi ya Ongolo ilipokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Camperdown, jijini Durban.

Ilielezwa kuwa, Ongolo si raia wa Afrika Kusini na kwamba alirudi nchini humo Januari 19 mwaka huu baada ya kurejea kutoka katika mizunguko yake katika nchi kadhaa za Afrika zikiwamo, Tanzania, Malawi, Msumbiji na Ethiopia.

Ilielezwa kuwa visa yake inamalizika Februari 18 mwaka huu.

“Atarudi nchini mwake Tanzania na hatarudi tena Afrika Kusini,” alisema Marion.

Chanzo chetu cha habari kilichohudhuria kesi hiyo, kilisema Brigedia Marion alihojiwa kuhusu taarifa za mashtaka dhidi ya Mtanzania huyo ambapo alitoa ushahidi kuwa Ongolo amekuwa akituma ujumbe mfupi kwenye simu ya MaNtuli, akimtishia kuwa atatoa siri kuhusu uhalali wa mtoto wake (MaNtuli).

Inadaiwa kuwa Ongolo katika ujumbe wake alidai kuwa mtoto mmoja wa MaNtuli si wa Rais Zuma.

Kabla ya kukamatwa, Ongolo alikwenda katika vyombo vya habari kadhaa vya nchini humo na kudai kuwa, anafahamu siri nzito kati ya MaNtuli na Phinda Thomo, aliyekuwa mlinzi wa MaNtuli.

Thomo, alikutwa amejiua mwaka 2009 bafuni kwake, lakini Ongolo anadai kuwa Thomo hakuuawa na badala yake, kifo chake kilipangwa kutokana na uhusiano wa siri kati yake na MaNtuli.

Mashtaka ya kutishiwa kuvujisha siri zake, yalitolewa na MaNtuli ambaye alidai kuwa Ongolo amekuwa akimlazimisha kumkutanisha kibiashara na Rais Zuma.

Brigedia Marion alitoa ushuhuda mahakamani na kuiomba mahakama kukataa kutoa dhamana kwa Ongolo ambaye alikamatwa mwishoni mwa Januari mwaka huu.

“Tofauti na inavyoandikwa kwenye magazeti, Ongolo alikamatwa baada ya kufika ofisini kwangu akija kulalamika kuwa kuna kesi ya wizi na uvamizi kwenye nyumba ya dada yake ambayo inasimamiwa vibaya,” alisema Brigedia huyo.

Alisema, Ongolo alipofika ofisini hapo alijitambulisha kama Stephen Ongolo lakini baadaye alibainika kama Stephen John Masunga ndipo Marion akalikumbuka jina kwani MaNtuli alikuwa ameshawasilisha mashtaka hayo polisi.

“Kukamatwa kwake ilikuwa ni bahati. Nilipoona jina ni lilelile, nikaangalia namba ya simu niliyopewa na MaNtuli na kuanza kuipiga na simu ya Ongolo ikaita na hapohapo nikamweka chini ya ulinzi,” alisema Marion.

Ilidaiwa kuwa baada ya Ongolo kukamatwa, simu yake na hati ya kusafiria vilichukuliwa na alipotakiwa kumpigia simu wakili wake, hakufanya hivyo na badala yake alimpigia simu mwandishi wa habari wa gazeti la Sunday Independent, Nathi Olifant.

Marion alisema, alikusanya ujumbe mfupi kutoka kwenye simu za Ongolo na MaNtuli na kubaini kuwa wawili hao waliwahi kukutana mwaka 2010.

Source: Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wabongo kweli tuna akili, yaani kama sinema vile

    ReplyDelete
  2. Akili gani utapeli na wizi mtupu haya sasa arudishwe kwao na atafungiwa milele kujifu anya ajua kumbe hana ajualo tusije tukasikia tu naye alijinyonga.watu bana why can't u mind ur own business.

    ReplyDelete
  3. Asilimia kubwa ni umbea tu na alitaka tu kumchonganisha huyo Mantuli na zuma.Wabongo sijui tukoje jitu zima uchonganishi tu,kuna watu utafikiri wanga kwa roho zao za wivu walizonazo na ndo zinawapelekea kuchonganisha watu.Hata kama ni kwel wewe ongolo inakuhusu nini??na hata wengine elimu haziwakomboi wako chuo lakini kutwa kuchonganisha watu.

    ReplyDelete
  4. Umbea ni Asili haijalishi una Elimu au hauna,muache arudi bongo tuchome maindi wote!! Zuma ana wake kibao hatari kitu gani mke wake nae akizaa na mtu mwingine,ukimwaga mboga mwingine ana mwaga ugali maisha yanasonga,uliyaka umaarufu umekutokea puani,na huyo dada wa kukaa nae mbali maana akijua siri yako kwishinei,unaleta usanii mpaka nchi za watu kazi kwelikweli.

    ReplyDelete

Top Post Ad