MJAMZITO JIUZA SIKU TATU KABLA YA KUJIFUNGUA!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
YELEUUUWI! Mwanamke mjamzito aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamisa amenaswa laivu na ‘makachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers,  akijiuza huku akiwa na ujauzito wa miezi nane na siku 27, zikiwa zimesalia siku tatu afikishe miezi tisa tayari kwa kujifungua.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita usiku wa manane Mbagala-Zakhem, Dar, wakati OFM ikiwa katika oparesheni zake kwenye danguro moja maarufu linalojulikana kwa jina la Kwaswai lililopo maeneo hayo.

OFM ikishirikiana na polisi wa Kituo cha Mbagala-Kizuiani ilifumuafumua danguro hilo na kuwanasa watu kadhaa wakifanya vitendo haramu na hatarishi vya ngono lakini kilichowastaajabisha na kuwaacha midomo wazi watu waliofurika katika eneo hilo, ni mmoja wa machangu hao kunaswa akiwa na ujauzito.

Akizungumza na OFM baada ya kuulizwa sababu za kujiuza akiwa katika hali hiyo, mjamzito huyo alisema hayo yote yanatokana na ugumu wa maisha kwani alipata mimba akiwa katika kazi hiyohiyo.

Alipoulizwa ujauzito wake una umri gani alidai kuwa bado siku tatu tu itimie miezi tisa akajifungue.
Aliongeza kuwa kwa sasa mmiliki wa danguro hilo amemkataza kujiuza katika danguro lake kwa kuwa angeweza kujisababishia matatizo hivyo aliamua kufanyia biashara zake nje ya danguro hilo.

“Mbona mnanikamata jamani! Mimi sihusiki na danguro hilo la...(akimtaja mmiliki) kwanza ameshanikataza kujiuza kwenye danguro lake kutokana na hali yangu. Yote ni maisha tu jamani!” alisema.

Baadaye Hamisa pamoja na wenzake walipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa kituo cha polisi Mbagala-Kizuiani wakisubiri sheria ichukue mkondo wake kwani shitaka kubwa linalowakabili ni uzururaji.
Global Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wambea wakubwa wenyewe wanawannua wanajifanya nyoko wamuache asje akazalia huko kama hana hela zavifaa afanyeje kwa mfano

    ReplyDelete
  2. nikweli mdau manawanaume naonichanzo chamaadili kuhalibika ,huyodada ilitakuwa mwanaume aliempahyomimba amuhudumie lakiniutakuta mhuskahataki amekataa namaisha mjininimagum sana anaonabora afanyeili asogeze skumana kuhudumiwa ospital nighalama mpila,nguo unawezaukaambiwa ujenapea 10zavitenge mabeseni2 badohujala kamamzazi yaniinauma sana hapoamtaje tumwenyemimba achukuliwe hatua .

    ReplyDelete
  3. watoto wanaozaliwa gerezani wanakuwa na matajiri huko baadae kama alivyokuwa afen shakur mama yake marehemu tupac shakur

    ReplyDelete

Top Post Ad