MOROGORO KIMENUKA..WAKULIMA WACHACHAMAA..POLISI WATULIZA VURUGU NA MABOMU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Askari wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima  Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Joel Bendera  Ili kutatua Mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopo katika vijiji hivyo.Askari wa jeshi la Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya Machozi mara baada ya Wananchi wao kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya  mvomero

Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wameshika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.

Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji. 

Wakulima wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero wamefunga barbara kuu ya Morogoro Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi  baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao walikusanyikajana usiku na kufikia maamuziWakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa. Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad