NCHI HII INAPOTEZA MWELEKEO WASOMI MKO WAPI?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni ukweli usiopingika nchi hii inapoteza uelekeo tofauti na miaka ya 60. Miaka ya 60 hatukuwa na wasomi wengi sana kama maprofesa, madoctor, masters, na bachelors ukilinganisha na ilivyo sasa, chakushangaza nchi ndio inazidi kutumbukia kwenye kila aina ya uovu, na kwa bahati mbaya hakuna hata anayefanya utafiti na kujua tatito ninini.

Miaka ya 60 ilikuwa nafuu kulikuwa na uadilifu tofauti na ilivyo sasa, hivi sasa watoto wanazaliwa wanaanza elimu ya msingi mpaka kufikia vyuo vikuu wakiona wizi, chuki, uongo, fitna.... nikitu cha kawaida tofauti na miaka ya 60. Ukosefu wa uadilifu umefanya ongezeko la wahuni mtaani, mpaka kufikia hatua mtu anashindwa kutofautisha msomi na asiye msomi.

kwa bahati mbaya wahuni hao wanaanza kuingilia polepole sector nyeti ya siasa hapa nchini.

Kila anayelala na kuamka anakwambia namimi nataka kugombea ubunge, matokeo yake tunakuja kupata wahuni wa kisiasa kazi kurushiana matusi majukwani mfano halisi ni mh. Lusinde alipokuwa kwenye kampeni huko Arusha. Pia matokeo yake utakuja kuona wahuni wa kisiasa walivyotaka kuivuruga chadema na kuitana wasaliti huku wakipandikiza chuki kwa wanchi huku sisi tunabaki tunashabikia tukiwapoteza watu muhimu katika ukombozi kwa walio masikini.

Hivi sasa msema kweli ndiye muongo na msema uongo ndiye mkweli.Niseme kwamba chadema ni chama makini sana ila kikihendekeza wahuni wanashinda humu Jf wakipandikiza chuki ndani ya jamii kitapoteza uelekeo.

Umuhimu wa kuwasomesha wanafunzi huku hatuoni faida yao uko wapi? Wengi wanaishia kuwa wanywa pombe, na watu wa vijiweni. Kila aina ya raslimali tunazo wameshindwa hata kutupatia elimu zao tukazalishe, wamesubili ajira wakale rushwa au nao kutamani ubunge wakawe wezi na kupata kiinua mgongo.
By  mayange from JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ajira mnawapa watoto wenu na ndugu zenu halafu mnasema wasomi tuko wapi,acheni ukuma huo.Mwisho wenu unakuja pumbav

    ReplyDelete
  2. I second u mdau..nami nasema PUMBAVUUU kabisa.Huwa sipend kutukana ila na uchungu sana ajira wanawapa watoto wao,rafiki,na jamaa zao.Kina sie tusomjua mtu twapata ajira kwa kudra za mwenyezi Mungu na kusugua goti sana kusali.Loh Ole wenu wote mnaokatili wananchi kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe IPO SIKU MTALIA KILIO CHA KUSAGA NA MENO.MNAUMIZA WATU WENGI SAANA direct and indirectly.MTALIPA HUZUNI mnazotusababishia nyie na vizazi vyenu.Munaweza kuwa na pesa nyingi za kutuibia watz ila hamtokuwa na furaha.HIVI huwa mnasali nyinyi mafisadi?mbona hamumwogopi MUNGU?Anawaona na ipo siku atakosa UVUMILIVU..and that is WHEN YOU WILL BE PUNISHED.

    ReplyDelete
  3. Mnavyolalamikia our government mnakosea coz Ajira Nyingi now dayz tunaomba kwenye office binafsi na sio government. Coz gvrnment yetu inatoa ajira Za uwalimu udocter jeshi, police , na kazi balimbali zinaOusu jamii wanobana ni watu binafsi coz Ndio wamebase kwenye sector tulizosomea wengi . Kinachotakiwa ni mfumo mzima Wa sheria Za office binafsi kubadilika ndipo haki itatendeka

    ReplyDelete
  4. GOVERNMENT sio solution Jamani Hivi lini mtaelewa .Government always ni matatizoo.Get skill and self employ (capitalist rocks )

    ReplyDelete
  5. kote ni ujuani tu ndio upate kazi au uwe na mshiko c serkln wal sect binafsi utu haupo umebaki unyama tu. wat wanahah kutfut kaz acha zarau kabisa juu ya hili.

    ReplyDelete
  6. halafu mnataka kumpa nchi FISADI!! kweli Watanzania bado saaaaaana, akili ni duni kweli.

    ReplyDelete
  7. Mmm we Admn huyo m2 anaeitwa Masters na Bachelors ndo nan? Maana Doctors na profeseli hapo naelewa.

    ReplyDelete

Top Post Ad