google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html RAIS KIKWETE MBONA UMEAMUA KULIANGAMIZA TAIFA-LEMA | UDAKU SPECIAL

RAIS KIKWETE MBONA UMEAMUA KULIANGAMIZA TAIFA-LEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mh Rais, nakusalimu!

Kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbambali mbali vya habari wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wako wa NEC (CCM ) ni kauli hatari na yenye laana kubwa sana ya damu za Watu wengi katika Taifa letu. Ninaona wakati mgumu mwingine ambao Taifa letu linaingia kwa sababu ya kauli yako ambayo sasa imetangaza mauaji rasmi yatakayoongozwa na Viongozi mbali mbali wa CCM Nchi nzima huku Polisi wakiendelea kusimamia kama kawaida yao.

Mh Rais , Kwa mujibu wa maneno yako umethibitishia Umma wa Watanzania kuwa mmejadiliana kwenye kamati Kuu na kukubaliana kuwa sasa yale mambo mliyokuwa mnayafanya kwa kificho sasa yamethibitishwa na Kamati Kuu ya Chama chako na kutangazwa na wewe mwenyewe kuwa , kuumiza , kuua , kutesa na kudhalisha sasa imekuwa sera rasmi ya CCM na umeithibitisha kauli hiyo mbele ya Wajumbe wa Baraza Kuu la CCM ( NEC).

Mh Rais , kwa kauli hii naomba nikuambie kuwa umeamua kumalizia kipindi chako kwa mikono iliyojaa Damu na Roho za Watu . Nafasi uliyonayo ni kubwa sana sio jambo jepesi kuona makosa makubwa au madogo na kutubu , wapambe ni wengi ambao kwa kumsifu Mfalme hata kwa ujinga maisha yao na ya watoto wao yataendelea kuwa bora , lakini nakuhakikishia kwa kauli hii iko siku utajuta na kulaani ni kwanini ulitoa kauli mbaya na yenye hatia kama hii kwa Kiongozi mkubwa wa Nchi kama wewe . Vijana wa CCM sasa wamejipanga kuua na kuchinja hadharani kama ambavyo umeagiza wafanye na Polisi watakuwa Kimya kabisa kama ambavyo siku zote wamekuwa lakini mara hii watasaidia wazi wazi kabisa unyama wote utakaofanywa kwani wao pia wamesikia Amri yako na wewe ndio Mkuu wa Nchi hii.

Mh Rais, mambo mengi yanachangia kuvurugika kwa Amani lakini moja kubwa ni pale Polisi na Mahakama zitakaposhindwa kutenda wajibu wake katika kutenda haki haswa pale uonevu unapokuwa dhahiri . Naweza kutambua matendo yote mabaya yanayotokea wakati wa Uchaguzi kuwa yamesababishwa na Upendeleo wa Jeshi la Polisi kwa Wanachama wa CCM pindi wanapofanya uhalifu dhidi ya wenzao wa Vyama Vingine vya Siasa. Mwaka jana 2013 wakati wa uchaguzi wa marudio wa Madiwani wa kata nne Arusha Mjini watu zaidi ya 16 waliumizwa vibaya na Green Guard na matukio yote yaliripotiwa lakini mpaka leo hakuna Mtu aliyefikishwa mahakamani kujibu mashitaka, lakini unakumbuka na unajua kuwa mkutano wetu wa kufunga Kampeni hizo za Udiwani ulipigwa BOMU na Watu Wanne waliuuwa na Zaidi ya 100 kuumizwa vibaya na wengine wamebaki na Vilema hata leo na tumekuomba uunde tume ya Kimahakama ili tukuletee Wauaji wa watesaji wa tukio hilo lakini mpaka leo umegoma na badala yake zimekuwepo jitihada nyingi zinazofanywa na Jeshi la Polisi kubambikia Watu kesi nikiwemo mimi na kutesa watu kwa kiwango ambacho hakielezeki.

Mh Rais, Watu wameteswa na wanaendelea kuteswa sana katika Nchi hii na kazi hiyo inafanywa na Polisi na ccm na hapa ndipo mashaka katika jamii yanatokea na Jamii kuona ulinzi wao huko mikononi mwao na sio mikononi mwa Polisi na sheria za Nchi. Sasa umetangaza Watu wapigwe na wachinjwe hadharani , jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba umeamua kuangamiza Nchi uliyoapa kuitetetea na ulioagiza wapigwe sina uhakika kama watakua wamelala chini wakati wanapigwa au wamefumba macho wakati wanateswa na kama itakuwa kinyume maana yake kutatokea Ugomvi ambao madhara yake mimi kwa sasa sielewi ila wewe MKUU uliyotoa amri utakuwa unajua.

Mh Rais, Wewe wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu umeshindwa kuamrisha Polisi walinde Raia na mali zao na sasa umeamua Watu wachinjane? kwa kauli hii unasubiri nini Ikulu ? Hata hivyo Nguvu ulizonazo sio Imara sana kama Nguvu alizonazo Mwenyezi Mungu . Mateso na Damu iliyomwagika katika Taifa hili kwa uzembe wa utawala wako hakika utalipa kama sio wewe Watoto wako na Wajukuu zako elewa kuwa hakuna dhambi itakayopita bila kulipwa. Kauli yako hii inaleta hofu kubwa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 lakini hatutaogopa kufanya kampeni kwa sababu Rais ameruhusu tupigwe na tuchinjwe, tutasonga mbele kutafuta haki tunayoamini kama ambavyo pamoja na matangazo mengi ya malaria kuua lakini hatujawahi kutembea huku tumevaa chandarua .

Mh Rais wewe sio Mungu , hata hivyo unamkumbuka Jean Kambanda aliyekuwa Waziri Mkuu wa Rwanda mwaka 1994 alishatakiwa kwa kutoa kauli kama yako na kugawa mapanga kwa Vijana wa Nterahamwe na kusababisha mauaji makubwa sana Rwanda na tarehe 18/7/1997 alikamatwa Nairobi na baadae alishitakiwa na kufungwa Maisha kwenye mahakama ya ICTR Arusha na hii ilikuwa tarehe 4 sept 1998, sikufundishi uoga hata kidogo ila ni muhimu kujadili historia muhimu kulingana na wakati.

Mh Rais thamani yako haitatokana na kusababisha CCM iwe madarakani tena bali Haki kuwa madarakani katika kipindi ulichotawala ni hekima ngumu kuielewa lakini ni lazima tuiseme. Tunaenda Kalenga kupigwa na kuchinjwa kwa sababu tu umewapa Watu wako ujasiri wa kufanya hivyo lakini elewa kuwa kila tukio litakalosababishwa na kauli zako ni tukio ambalo utalipa gharama zake. Makala zangu kama hizi uwezi kuzipenda sana Mh Rais, Wapambe watakuambia huyu kijana ni muhuni na maneno mengi ya kejeli lakini elewa kwamba anayekupenda ni anayekuambia ukweli, kwani ukweli thamani yake ni kubwa mno hata kama una madhara ya muda.

Mh Rais, Ninapata hofu ninapoandika waraka huu kwani kama ni kwazo basi unaweza kuamua kufanya chochote dhidi yangu lakini napata faraja kuwa kifo kipo tu hata kama utafuti haki na ukweli kwani Bibi yangu kule Machame hakufa kwa kuwa aliandika waraka bali ni umri tu ulimuondoa. Mh Rais ukweli nakuambia usipofuta kauli yako yenye lengo baya kwa Nchi yetu basi nimemuomba Mungu afanye jambo muhimu dhidi yako na jambo hilo muhimu liko wazi kuwa kama wewe ni chanzo cha Taifa kuharibika kwani nini anaendelea kukupa pumzi? Hapa nitaonekana muhuni tena lakini Mh Rais wema wako ni katika haki na sio sifa.

Mwisho, Mh Rais, Mamlaka yana tabia ya kudanganya akili nikuombe Rais wangu usikubali mamlaka ikudanganye hata kidogo, futa kauli yako, watakaokuona mjinga wao ndio wajinga. Najua Polisi na Jeshi wanakutii wewe lakini Dhambi na hila iko mbali na MUNGU.


Godbless Lema (Mb)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UOGOPI KUNG,OLEWA KUCHA

    ReplyDelete
  2. PUMBAVU LEMA NA CHADEMA YOTE. SASA NYIE MNATAKA NINI???? KUMANINA ZENU, MLETE FUJO TUWAANGALIE TUUUU, MATAKO YAKO. LETE USENGE UONE TUNAVYOKUONDOA, UKIKAA NA NIDHAMU YAKO HAKUNA WA KUKUGUSA. MATAKA WEWE. AMANI MNAICHEZEA WENYEWE MIKUNDU NYIE MSIO NA SHUKRANI. KWANI NANI ASIYE MAPUNGUFU, MNATAKA CCM IENDESHWE NA MALAIKA. TUTAONA SASA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. we acha usenge kumamayo zako, we utalinda Dunia? matako yako hii Dunia si ya baba yako malaya vumbi wee nenda kamtishe mama yako mkundu wako!

      Delete
  3. MUULIZE ULIMBOKA ALIFANYWA NINI?

    ReplyDelete
  4. Mbona waTZ mmekuwa wababe? Badala ya kuzingatia vitu muhimu naona wooote mmekuwa wanaSiasa, Noumer. Na huyo raisi ndio kabisa bora kabla hajafungua mdomo wake angeenda muuliza ushauri mkewe! Acheni upumbavu, nchi tajiri lakini raia maskini.

    ReplyDelete
  5. hajasema watu wapigane wala wachinjane kasema ule unyonge wao umefka kikomo,nyinyi mnawatuka,mnawadhihak nakutoa taarifa ya uongo juu yao,unadhan hawachok eeeh,unyonge wao unaweza kuwa kikomo kwa staili nyingi,mkiandamana na wao wataandama,mkiwatuc na wao watawatuc,kila kitu kina mwanzo na mwisho n smtymz ni bora kufanya maamuz magumu ili kupata maendeleo mbona mizengo pinda alisema pigen unadhan alitengua kauli yake...kwasababu ukiandama bila kibal nakuleta fujo pigaa tuu,mambo ya kubembelezana hayapo tena cz hatutafka km kila cku tunashkana mashavu ucfanye kile mara ucfanye hiki...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani ukiwa kiongozi hasa raisi wa nchi ni vizuri Mola akakupa busara na hekima kama mf suleiman huyu raisi ni chaguo la Mungu basi afanye yampendezayo na si kuwafurahisha wachache

      Delete
  6. Chadema kuma nina zenu si mlizoea kuwafanyia fujjo kila siku wenzenu mkiwaona mafala walivyokuwa kimya baada ya amiri mkuu kutangaza unyonge baaas anangalia mikundu inavyowacheza kwa uoga
    mlitegemea kila siku mtaangaliwa tu mkitofoa wenzenu nyie c mliona nyie pekee ndio mnaweza ugomvi au mmeyavulia maji nguo yaogeni sasa mlikuwa mkiyataka yale ya kenya ya 2007 mkiona wenzenu wanafaidi hayo sasa yanakuja
    ukijua ugomvi jua na kujilinda co kukimbia ngoja mi nianze kunoa panga langu ambalo cjalitumia kitaaaambo maana nilijua tu hata barabara iwe ndefu vipi haikosi kona sasa barabara ya chadomo yenye mabasi maarufu yaitwayo ugomvi yanakaribia mwisho wa safari yake
    TUSUBIRI TUONE MWISHO WENU

    ReplyDelete
  7. TEKENYENI MIKUNDU YENU KAMA MLIVYOZOEA MUONE MZIKI. MLIDHANIA NCHI YENU HII??? NCHI YETU SOTE, SISI NA NINYI UNAPATA SOTE. SASA GUSA UNATE. FOOLISH CHADEMA NA LEMA

    ReplyDelete
  8. Walisema kuwa mweusi ni tatizo na kweli nahamini sasa ndio maana Baba zenu wanalipwa laki 2kwa mwezi na uliemchagua hanachukua kwa siku leo mijitu na akili zenu mnaona ni sawa please umefika mda wa watanzania kuwa more indepent muone hao wanashelia kama hawaja hacha hiyo tabia ya kujigawia wao

    ReplyDelete
  9. Ama kwel hawa viongoz wanatuangusha wapiga kura wao.Nichaguen mimi jamani..Mimi oyeee

    ReplyDelete
  10. Wewe uliosema "weuc ni tatizo" kuma la mama yako,huyo Lema yeye wakati anaiba magari ameuwa watu wangapi leo ndio ajifanye anasikitikia damu za watu? Nae kuma la mama yake na anae mtetea pia.

    ReplyDelete
  11. sasa ndo nini iyo? mijitu mingine bwana!

    ReplyDelete
  12. Kaka punguza hasira!Najua mwanaharakati wa kweli,lakn lugha za matus hazijengi kwan mitandao hii inasomwa na wengi!Tumia lugha elekez kama msomi watu watakuelewa tu ndugu!

    ReplyDelete

Top Post Ad