SIRI YAFICHUKA MAUAJI YA WAFARANSA WALIOTUPWA KWENYE KISIMA CHA MAJI Z’BAR

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zanzibar Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji (KZU) na Polisi wamefanikiwa kuvunja zege lililokuwa limejengwa kufunika kisima walichotupwa raia wawili wa Ufaransa, baada ya kuuawa na kupata sehemu za miili yao ikiwamo fuvu la kichwa.
Aidha, siri za mauaji hayo zimeanza kuvuja, ikielezwa kwamba waliotekeleza unyama huo walilenga kupora nyumba na kiasi kikubwa cha fedha.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi na Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI) Yussuf Illembo, alisema kuwa hadi jana mchana, mifupa miwili ya mapaja, fuvu la kichwa na miwili ya mbavu imepatikana kutoka ndani ya kisima hicho.
Alisema kwamba Kikosi Kazi cha Uokoaji kinaendelea kufanya kazi eneo hilo la Matemwe lililopo Shehia ya Kaskazini, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Kazi bado ni ngumu, tunaendelea kuzamia ndani ya kisima na itakapokamilika tutatoa taarifa. Tuacheni kwanza tufanye kazi hii nzito na ngumu kwa wakati huu,” aliomba DCI Illembo.
Zoezi hilo lilifanyika huku likishuhudiwa na ofisa mmoja wa Ubalozi wa Ufaransa nchini na kuelezwa kuwa marehemu hao walinunua eneo la ardhi na nyumba kwa Sh150 milioni kwa kutumia jina moja la mzawa wa Zanzibar, kutokana na sheria kutoruhusu wageni kumiliki ardhi visiwani humo. 
 Watu hao, Francios Chererobert Daniel, aliyekuwa mtumishi mstaafu wa ngazi za juu wa Serikali ya Ufaransa na mkewe Brigette Mary, walipotea tangu Desemba 27 mwaka jana.
Baadaye taarifa za kupotea kwa watu hao zilifikishwa Polisi ndipo msako wa kuwatafuta ulipoanza na baadaye kugundulika kuwa, kuna watu wameuawa na miili yao kutupwa katika kisima cha maji kilichopo ndani ya ua wa nyumba hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya waokoaji na mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia gazeti hili kwamba sehemu hizo za mwili zinazosadikiwa kuwa za Wafaransa hao, zimefukuliwa baada ya kazi kubwa ya kuvunja zege kwa kutumia mashine maalumu inayofanywa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo.
“Tumefanikiwa kutoa sehemu ya miili, imehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyeomba jina lake lisitajwe.
Alisema kuwa kazi ya kuvunja zege hilo ilikuwa ngumu, walilazimika kuwachukua vijana wengine raia wa kawaida ili kuifanikisha.
Akielezea mazingira waliyokutana nayo chini ya kisima walichotupwa Wafaransa hao, alisema kuwa baada ya zege kuvunjwa walikuta nguo nyingi zimejazwa chini yake na juu yake kujengwa zege hilo kabla ya kumwagwa saruji isiyochanganywa kitu ili kufunika kisima kwa lengo la kupoteza ushahidi. 
Hata hivyo, vyanzo vya habari vinaeleza kuwa zoezi hilo lililazimika kusitishwa kutokana na sehemu ya chini ya kisima kupita mkondo wa maji ya bahari, hivyo kulazimika kutafuta mashine ya kuvuta maji.
“Kazi hiyo ikiweza kufanyika ndipo tutakapoweza kwenda katika kina kirefu zaidi cha kisima hicho ili kukusanya mifupa. Tukipata idadi ya mifupa na mafuvu yote, tutaweza kujua waliouawa ni wangapi,” kilieleza chanzo kimoja.
Sheha wa Shehia ya Matemwe Kusini, Denge Khamis Silima alisema kuwa wanapata faraja kuona zoezi hilo limepata mafanikio tofauti na siku ya kwanza na kwamba kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa umakini huku akiitaka Serikali kuwapatia vifaa waokoaji ili kufanikisha kazi hiyo.

Siri ya mauaji
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa siri ya mauaji hayo ni baadhi ya watu kutaka kupora nyumba, waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao pamoja na fedha zinazodaiwa walikuwa nazo raia hao wa kigeni wakitaka kununua eneo la kujenga hoteli kwenye ufukwe wa Urowa.
Inelezwa kuwa kabla ya kuingia Zanzibar, Wafaransa hao walifikia Nairobi nchini Kenya ambako inadaiwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini humo aliwashauri kwenda Zanzibar kuishi na kuwekeza.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa kabla ya watu hao kuuawa, mbwa wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Allan, alipewa chakula chenye sumu na kufa na kwamba sehemu ya mabaki ya chakula hicho yaliliwa na mbwa wa jirani ambaye pia alikufa.
Aidha, mifuko mitupu ya saruji inayosadikiwa kutumika katika ujenzi wa zege la kisima hicho, imeokotwa nyuma ya ukuta wa nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao. 

MWANANCHI
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kashfa nyingine kwa nchi.Kutoka tindikali sasa mauaji ya kisimani.

    ReplyDelete
  2. HIVI WAZENJ WAMEKUWA WAKATIRI KIASI HICHO,,EE ZANZIBAR NA TANZANIA KWA UJUMLA KUNATISHA SANA,,WATU TAMAA IMEWATAWALA MNO...WANAUWA TU UTAFIKIRI HAPA DUNIANI WATAISHI MILELE.

    ReplyDelete
  3. Mimi sishangai, unapokuwa na nchi ambayo takribani asilimia 12 hawana njia ya kupata kipato cha aina yoyote, majanga km haya ni vitu vya kutarajiwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. asante mdau.....gap ya tajir na maskinn kubwa mnoooooo wengi tunaishi ktk dhiki

      Delete
    2. Mdau umeongea, na hakuna mwanasiasa anaeongolea kupunguza mbinu za kupunguza kiwango cha wasiokuwa na ajira nchini(unemployment rate)
      makampuni yanapoanzishwa unakuta wanaopewa kipaumbele ni watoto wa wakubwa ambao kimsingi walishakuwa ktk ajira.ie makampuni ya cm, benki etc

      Delete
  4. Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga

    ReplyDelete
  5. MIMI NAFIKIRI ZNZ SASA HIVI INA WATU WENGI SANA NA MCHANGANYIKO WA MAKABILA TOFAUTI SANA NA UKIZINGATIA HALI YA MAISHA NI MAGUMU SANA KWELI LAKINI HAIJAAZA LEO HII HALI YA MAISHA NI MIAKA MENGI SAIVI, LAKINI HUU MSHANGANYIKO WA WATU TOFAUTI NDIO MATTER.

    ReplyDelete
  6. MIMI NAFIKIRI ZNZ SASA HIVI INA WATU WENGI SANA NA MCHANGANYIKO WA MAKABILA TOFAUTI SANA NA UKIZINGATIA HALI YA MAISHA NI MAGUMU SANA KWELI LAKINI HAIJAAZA LEO HII HALI YA MAISHA NI MIAKA MENGI SAIVI, LAKINI HUU MSHANGANYIKO WA WATU TOFAUTI NDIO MATTER.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kubagua mdau apo juu, hii hali ya raia wa kigeni kutendwa nikutokana wazanzibari hawataki maendeleo wanaona kama utamaduni utaharibiwa wakati kuharibu wataanza wao wenyewe. Sasa saivi matukio yanaongezeka ya ajabu hivo yatachangia kushuka kitega uchumi kwa kiasi kikubwa. Maana zanzibar wanategemea tourism. Saivi tanzania bara na kenya watajizolea wageni wakati wazanzibari maisha yakizidi kupanda kwa hali itakavyozidi kuwa ngumu.

      Delete
    2. Acha kubagua mdau apo juu, hii hali ya raia wa kigeni kutendwa nikutokana wazanzibari hawataki maendeleo wanaona kama utamaduni utaharibiwa wakati kuharibu wataanza wao wenyewe. Sasa saivi matukio yanaongezeka ya ajabu hivo yatachangia kushuka kitega uchumi kwa kiasi kikubwa. Maana zanzibar wanategemea tourism. Saivi tanzania bara na kenya watajizolea wageni wakati wazanzibari maisha yakizidi kupanda kwa hali itakavyozidi kuwa ngumu.

      Delete

Top Post Ad