TASWIRA YA TANZANIA YACHAFUKA NCHINI UINGEREZA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kwenda London Uingereza kuhudhuria mkutano wa kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani ukianza wiki hii, tatizo la ujangili limeweka wingu zito kwa Tanzania.

Rais Kikwete ni kati ya viongozi wa nchi 50 watakaohudhuria mkutano huo, utakaokuwa chini ya wenyeji wa mwana wa Wales na Waziri wa Mkuu wa Uinegerza, David Cameron,

Taarifa ya gazeti la The Mail on Sunday la Uingereza la Februari 8, limeitaja Tanzania kama kinara wa ujangili kwa kuua zaidi ya tembo 11,000 kwa mwaka, huku Rais wake (Jakaya Kikwete) akielezwa kufumbia macho.

Pia, gazeti hilo limemhusisha Rais Kikwete kuwa na urafiki na wafanyabiashara ya meno ya tembo, huku likiwahusisha wafadhili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika biashara hiyo.

“Utawala wa Rais Kikwete umetawaliwa na mauaji ya tembo yaliyovunja rekodi katika historia ya nchi yake. Kibaya zaidi, wahifadhi wanasisitiza kuwa, ndani ya Serikali kuna viongozi wanaoshiriki biashara hiyo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika mkutano huo, viongozi wa nchi 50 na mawaziri wataweka mikakati dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori, yenye thamani ya pauni 6 bilioni za Uingereza kwa mwaka zinazotumika kufadhili magaidi.

Taarifa hiyo inasema kuna wafanyabiashara wakubwa wa Dar es Salaam wanaohusika na ujangili.

“Miongoni mwao ni  matajiri wakubwa nchini, wafadhili na wanachama wa CCM na ndugu wa karibu wa Rais Kikwete. Lakini wanao marafiki wakubwa, huku majaji, waendesha mashtaka na polisi hurubuniwa kwa urahisi,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, taarifa hiyo inadai kuwapo kwa idadi kubwa ya Wachina wanaofanya biashara ya mafuta nchini, huku baadhi yao wakihusika na ujangili.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu alikiri kuona taarifa hiyo na kwamba, Rais Kikwete atahudhuria lakini aliipuuza taarifa hiyo.

“Ni kweli Rais Kikwete atahudhuria huo mkutano, lakini taarifa ni ya None sense, crap and malicious (ya kishenzi, kipuuzi na ovu),” alisema Rweyemamu.

Juhudi za kumpata Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita  muda mrefu bila kupokelewa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lazima aipuuze kwa sababu hana jibu la facts,hats mahakamani ukikaa kimya ni kwamba unakiri7

    ReplyDelete
  2. unaxema nyarandu akupokea xm?!....alikuwabzy na mikakat ya kulihujumu taifa

    ReplyDelete
  3. hivi hii nchi inaepelekwa wapi na hawa
    viongozi wanaopenda mkwanja ...
    kwani nyiesimnapewa mshahara tamaa ni zanini ..au mnashindwa kupangilia mipango yenu acheni
    hizo nyie mnatuboa .......

    ReplyDelete
  4. Tanzania tunauwa mali asili. Badala ya kukuza biashara ya utalii.Kweli ng'ombe wa masikini hazai.

    ReplyDelete
  5. ndiyo hao hao mnawashangilia na kutaka kuwachagua badala ya kutaka mabadiliko, halafu mnapiga makelele, kubalini mabadiliko, tuwape nchi watu wengine tuone watakavyofanya.

    ReplyDelete
  6. Endeleeni kuchagua viongozi wasiokuwa na hata "elimu dunia". Viongozi waliokuzwa na Umoja wa Vijana feki na kuleta "Uniform - mavazi ya kijani na njano" Kuonyesha kama wanasera bali hamna lolote mbali ya kujikwamua wao na familia zao kutoka kwenye umaskini. Wananchi amkeni: wengine wanakuja na sera za kuvaa suti.

    ReplyDelete
  7. KUMAMAYO ZENU MNA LALAMIKANINI? TUENDELEE KUYACHAGUA HAYAMACCM YAENDELEE KUTUHUJUMU!

    ReplyDelete
  8. 1Unajua hata msemaji wa Ikulu ni mzIgo kama wale mawaziri yeye ni matunda ya EPA. 2.Wachina hawawezi kukosa (they are plunderring with impunity kwa kuleta kapero/skuff/vilemba/mashati & fulana za chama

    ReplyDelete
  9. Tusidanganyane usalama wataifa wanajua wezi na majangili wote,na wafanya biashara wote,JWTZ,WAPEWE dhamana ya kushuhulikia hili jambo,pamoja na uhamiaji,na ujambazi nchi itapona,liwepo jeshi la pamoja kati ya polisi na jeshi,haiwezekani wanyama wakauliwa kama vile hakuna ,serikali ktk nchi yetu,inasikitisha sana,kwa aibu ,madini ya tanzanite,hivyo yataisha hatahatujui haya faida kwa taifa,sasa sijui tunajivunia nini? bado tunatakiwa jitihada ktk usimamizi wa mali ya umma.

    ReplyDelete

Top Post Ad