UTEUZI WA MUME NA MKE BUNGE LA KATIBA WAKIVURUGA CHAMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zanzibar. Sakata la Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emmanuel Makaidi kudaiwa kufanya njama zilizofanikisha yeye na mkewe kuteuliwa wajumbe wa Bunge la Katiba, limechukuwa sura mpya baada ya kiongozi wa chama hicho Zanzibar kujiuzulu na kujivua uanachama.

Akitangaza uamuzi wa kuachana na chama hicho juzi, Naibu Katibu Mkuu NLD Zanzibar, Khamis Haji Mussa alisema ameshindwa kuvumilia kitendo hicho alichodai kinadhalilisha chama.

“Kwa hiari yangu nimeamua kujiuzulu uanachama na kuacha wadhifa niliokuwa nao ndani ya NLD, jina zuri la tawi la Ustawi wa Kitaifa wa Demokrasia ni nadharia tu, vitendo vyake ni udikteta na ubabe... nashauriana na wanasheria kuona kama kuna kesi ya kufunguliwa,” alisema Mussa.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya NLD Zanzibar pia kutoa tamko la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi huo, kwa madai walioteuliwa kutoka chama hicho ni mtu na mkewe hivyo kukosa sura ya Muungano.

Mussa alisema ameshindwa kuvumilia kwa sababu kitendo hicho kinadhalilisha chama na kinaashiria ukosefu wa misingi ya uwazi na uadilifu.

Alisema amefikia uamuzi huo kutokana na madai kwamba Dk Makaidi ameonyesha waziwazi anaiongoza NLD kwa ubinafsi, ubaguzi na kuitenga Zanzibar katika uwakilishi wa Bunge la Katiba. Mussa alisema Dk Makaidi amejidhihirisha ni mbaguzi na anaweza kuligawa taifa kwa misingi ya Uzanzibari na Utanganyika, ikiwa siku moja atabahatika kupewa dhamana.

Alisema utetezi uliotolewa na Dk Makaidi umekosa nguvu ya hoja, zaidi ametumia umwamba unaoweza kuvipaka matope vyama vingine vya siasa.

Katika utetezi wake, Dk Makaidi alisema NLD Zanzibar walichelewa kupeleka majina kwa Rais wa Zanziba na kwamba, kuteuliwa kwa mkewe hakuna matatizo kwa sababu ana sifa zinazotakiwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. unahela ya kutosha we jiuzuru tu

    ReplyDelete
  2. sawa ndo demokrasia

    ReplyDelete
  3. we jiuzuru tu, mtuachie tunaojua kazi

    ReplyDelete

Top Post Ad