VICK KAMATA:UTAJIRI HUU UNAHITAJI MAELEZO YA ZIADA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa. Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania angependa kuyapata.

KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni. Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii. “Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro. “Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina la baba halikutajwa).

MAFANIKIO YAANZA Mwaka 2006, Vicky alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano. Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita. 

MJENGO WA GHOROFA MBILI Akiwa mbunge, Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne. Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake. 

MAGARI YAKE SASA Kama walivyo matajiri wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 261. Ana Toyota Voxy- Noah ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16. Kamata pia anamiliki BMW X5 likiwa na thamani ya shilingi milioni 130. Mara nyingi anapokwenda bungeni, Vicky hutembelea gari linalomudu mikiki ya barabarani, Toyota Land Cruiser ‘VX’ ambalo lina thamani ya shilingi milioni 90. Pia mwanamama huyo ana gari aina ya Toyota Altezza alilolinunua kwa shilingi milioni 25. 

ANAMILIKI MGODI WA DHAHABU Wakati hayo yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa, mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu Geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya mafanikio yake. “Vicky amenunua mgodi wa dhahabu Geita, mimi ni mtu wangu wa karibu, hapendi kusema mafanikio yake wala watu wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa, muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema chanzo cha habari.

ANA SHAMBA LA EKARI 157 Utajiri wa mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa, ni pamoja na shamba lenye ekari 150, Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Pia ana shamba la miti Kibamba, Dar lenye ekari 7. NI MFUGAJI Mbali na mambo mengine, Vicky ni mfugaji kama ilivyo asili ya Wasukuma. Anafuga ndege aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.

ANASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA Katika mambo ambayo huenda yanachangia kuchota baraka, mheshimiwa Vicky anawalipia ada ya sekondari watoto yatima, walemavu na wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.

KIPATO CHAKE KIKOJE?

Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge, ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara. 

AMFUNIKA ANNE MAKINDA Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba la kifahari la Vicky Kamata linalifunika lile la bosi wake ambaye ni spika wa bunge, mheshimiwa Anne Makinda. Yeye nyumba yake ipo Kijitonyama.

ULINZI NYUMBANI KWAKE USIPIME Uwazi lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa Vicky na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24. Ili mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi kwa dakika zisizopungua kumi.

HI NDIYO CCM INAYOWATETEA MASIKINI NA WAKULIMA NAWANYONGE.

Credits:Global Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

23 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NO COMENT;au kunautratra!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. kwa vyvyote kuna utata, utajiri huo wote wakati kuna umasikini kibao katika nchi yako, alafu na hizi siasa zetu za Africa, ukipata tu basi wewe tajiri, ndio maana kila siku na kila mtu anapiganiana kuingia huko kwenye siasa, kwani ndio njia ya utajiri, kwa kuiba kuhujumu mali za umma, ufisadi, kila aina ya uharamia umejaza huko kwenye siasa,

    ReplyDelete
  3. Naweza sema alipotolea.ila mhhhh ! Naogopa kwenda segereaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. 2 children from our presidaaa usiogope

      Delete
    2. Hahahah yeeeleewiiii

      Delete
  4. Huyo katombwa sana
    na Baba Rizi... Na ndiye aliemuwezesha kimaisha!!

    ReplyDelete
  5. CCM oyeeee! Hakuna kuzubaa tafuna mpaka mifupa.

    ReplyDelete
  6. lakini yeye ana sifa ya ziada maana kwa uzuri wake lazima anaitumia nafasi azipatazo

    ReplyDelete
  7. Lakini huyu dada ni mzuri sana nimpenda

    ReplyDelete
  8. chakula ya mkubwa!!

    ReplyDelete
  9. Mwambie ataje baba ya Watoto ndo mtajutraaaaa kumfahamu.

    ReplyDelete
  10. Wanawake wengine wananahati,kapelekwa uingereza kusoma,karudi kapewa kazi bank kuu,kazalishwa Watoto wawili sasa hivi anakula matunda,asalaleeeeeeeeeeee ,ndo mana mwakimu Nyerere alisema wanawake mmekalia uchumi wenu.

    ReplyDelete
  11. Kwenye kampeni za uraisi alikuwa bega kwa bega na mwenye nchi,mwache ale vyake

    ReplyDelete
  12. Udaku mnasema ulinzi nyumbani kwake msipime?sasa baba alindwe,Watoto wasilindwe huo Si Utakuwa usenge baridi?

    ReplyDelete
  13. Ile kampuni mke Wa shabani kaiita WAMA,kwani hakujua Kama Asha anatembea na Shabani?asalaleeee,mwenye kunielewa kanielewa.

    ReplyDelete
  14. Ulinzi lazima uwepo shabani anaendaga kupasha joto

    ReplyDelete
  15. Haaa kumbe huwo utajili ndio ule wa ufisadi, hmmm Africa hili kazi kweli kweli na na hawa viongozi wa bara hili, uchumi wanauweka mifukoni mwao. si maslahi ya Taifa. na kodi twa zidi lipishwa, ili waweze jaziliza viroba

    ReplyDelete
  16. itabidi iwe hivyo

    ReplyDelete
  17. heee kumbe nyumba ndogo mama naniliu!!!!!!

    ReplyDelete
  18. mama mdogoooooooooooooooooooooooooooooo, mrs mtawala wa nchiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii napita tu

    ReplyDelete

Top Post Ad