VITA KATI YA MALECELA NA LOWASSA NI YA MUDA MREFU...SIRI YA UTAJIRI WA LOWASSA HII HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tokea enzi ya uhai wa Julius Kambarage Nyerere Faili la LOWASA kufahamika kuwa na utajiri wa kutosha linafahamika sana,na haijaanza leo kwa Lowasa kusemwa na kupewa shutuma kama hizo wala hazikuanza jana.

Zimeanza tokea kipindi Mwalimu Nyerere yuko hai,na hadi alishafikia hatua ya kuhoji utajiri wa Lowasa enz hizo akiwa kijana kama wa miaka 42 hivi,na kwa wakati huo miaka 42 huonekana kijana kweli kweli tofauti na sasa vijana katika umri kama huo washakuwa wazee tayari kutokana na ugumu wa maisha na frustuations zake.

Je,unafaham ni kwa nin MALECELA kwa kawaida tuh tokea hapo kale hampendi Edward Lowasa??

Hii vita haikuanza leo.,wanaccm hawa wawili na wenye ushawish kwenye chama hiko wameanza msuguano na malumbano tokea enzi hizo John Malecela akiwa Waziri Mkuu na Lowasa akiwa Waziri mwandamizi katika ofisi ya waziri ya waziri mkuu,kwa mantiki hiyo kwamba alikuwa chini ya malecela na kwa kumsaidia majukumu ya kazi ya siku zote za kuendesha serikali.

Enzi hizo wabunge wa jamhuri ya muungano wa tanzania walikuwa hawana magari ya kusafiria kama haya wanayokopeshwa kwa sasa,hali iliyokawa inawapa ugumu sana kuwatembelea wananchi wao majimboni hata wakati mwingine ugumu pia wa kuwahi bungeni kwa wakati kutokana na aina ya magari waliyokawa wanayatumia kipindi hiki kukosa stability ya kumudu safari na ukizingatia ubovu wa bara bara wa kipindi huko maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

Hili suala lilikua linaumiza sana serikali kipindi hiko chiniya utawala na usimamiz wake wazir mkuu wa kipindi hicho ndug john malecela.

Kutokana na kuwaza na kuwazua likaja wazo la kupeleka idea kwa serikali ya watu wa japan ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwasaidia kihali na mali ili iweze kujikwamua katika tatizo hilo,

Mungu si Athumani,serikali ya japan enzi hizo wakakubali kuwaunganisha serikali ya tanzania na kiwanda cha toyota na kuwapa ushirikiano wa hali ya juu katika mazungumzo baina yao na kiwanda hicho hadi ikafikia tamati ya makubaliano kwamba serikali ya tanzania inaweza kukopeshwa magari hayo kisha wakawa wanalipa pole pole ili kusaidia kukizi na kuikubali changamoto hiyo.

Serikali baada ya kufanikisha plan hiyo ikaja kwa wabunge na kuwaeleza kwamba wanaweza kukopeshwa magari kwa mkopo,wabunge waliingia na wasi was kias flan na kusema wao wataweza kulipa vpi gharama hzo ukizingatia pesa waliyokawa wanachukua kipindi hiko isingetosha kulipa mkpo huo??

Serikali kupitia kw wazir mkuu malecele wakawaambia nyinyi chukuen tuh,sisi serikali tutajua tunawasaidia vipi,kwaiyo chukuen kwanza ili mukabiliane na changamoto ya usafiri kwanza.

Wabunge walikubali wazo lile na deal likafanyika,mambo yakafana kisawa sawa.

Sasa baada ya hapo mtu pekee ambae alikuwa anafuatilia mchakato mzima ni wazir wa nchi ofisi ya wazir mkuu enzi hizo akiwa ni edward lowasa,alikuwa anafuatilia suala hilo kwa ukaribu sana.


Wale wajapan walipolipwa chao,kumbe kuna makubaliano ambayo yakishafiikiwa baina yao na wazir mkuu malecela ya kumpatia kifuta jasho kwa kufanikisha deal ile kufanyika kwa ukamilifu wake.

Na yasemekana kifuta jasho hiko kilikuwa cha maana sana,cha maana sana sana,

Bahati mbaya sana wale wajapan walipofika ofcn kuleta kifuta jasho kile walianzia kwanza kwa ofisi ya wazir wa nchi ili wapate nafas ya kumuona wazir mkuu,sasa walipokutana na lowasa yasemekana akawauliza mnafuatia nin tena mheshimiwa ili hali deal ilishafanyika kikamilifu??kwan kuna tatizo??wale wajapan wakamwambia kwamba kuna kifuta jasho yapasa tumkabidh muheshimiwa wazir mkuu malecela.

Lowasa,,akastaajabu..!!akasema ,,"mnasema"???hicho kifuta jasho mnataka kumfikishia vipi mheshimiwa hamjui kuwa yule ni mtu mkubwa sana??kuna utaratibu wa kumfikishia kwa protokali ya serikali,sasa sikilizen bwana....

Hiyo pesa nipen mimi nitamfikishia,kwan kwa sasa hata hivyo yupo safarin hadi arudi,so nipeni mimi nitamkabidh,wale wajapan kwa kuwa wanafaham katika mchakato mzima wa ile deal lowasa nae alikuwa anaifuatilia kwa karibu hawakuwa na was was sana kumwachia amana kama ile.,,wakamwachia na kusign nae kisha wakageuza zao.

Kilichotokea hapo sasa mungu mwenyew ndie anaejua,

Lowasa akapiga kimya,kimya na yeye,yeye na kimyaa,muda ukawa unazid kwenda naskia ile pesa akaanza kuifanyia michakato ya kuizungusha na kuwekeza kwenye biashara ya real estate kwa haraka haraka na kuzikodisha kwa taasisi binafsi hata balozi mbali mbali za nchi mbali mbali,

Naskia ipo moja ambayo aliikodisha kwa ubaloz wa south afrika hapa hapa nchini,na hadi leo naskia iyo nyumba ni mali ya lowasa pamoja na vitu vingine vingi,kwa ufupi lowasa kawa DON tokea kitambo sana.

Sasa maskin mzee malecela akaona siku zinakwenda na kifuta jasho kutoka japan hakifiki,,akaamua kunyanyua simu na kuwavutia uzi jamaa na kuwauliza,ebwan vipi ile kitu yangu??mbona nyinyi wajapan wabaya kias hiko??ina maana baada ya deal kufanyika mnatupa jongoo na mti wake??

Wajapan wakasema Booossi,mbona kifuta jasho tulishaleta mda mrefu sana??tulimkabidh bwana Edward yule wazir wako wa nchi katka ofc yako na alisema atakukabidh kwan ulikuwa safarini..!!!

Malecela kikamshuka,kikampoa na asijue hata awajibu nini,

Ikabid sasa amwite edward na kumuuliza,wewe edward pesa yangu iko wapi??na nani alikuambia uichukue kwa niaba yangu??

Edward akasema Boooss,kwa kweli pesa nilichukua lakin sasa kwa kuwa ulikua safarini nikaona niiweke kwanza hadi urudi,,sasa kama unavyojua pesa tena mzee,kulitokea fursa za uwekezaji nikaamua kujikopesha ili niizungushe kisha nitakurejeshea lakin sasa mambo hayajaenda kama yalivyopangwa ndio kwa maana unaona kimya hiv sijakutafuta.

Sasa malecela presha ikampanda na kumshukaaa,atasema nini??na ile pesa ni chafu na ya deal ukizingatia yeye ni wazir mkuu??kumbuka nyerere yupo hai kipindi hicho na akifaham ishu kama hizo panakua hapatoshi..!!

Ikabid malecela ajikaze kisabun na kufa na tai yake shingoni huku lowasa akiendelea kupimp na kujitanua kwa raha zake.

Kwa kias kikubwa hapo ndipo LOWASA alipoanza kuwapiga GAPE LA KIPATO wenzake walio wengi,na kwa kias kikubwa wenyewe hao ambao wako ndan ya system wanalijua hilo.

Ndio kwa maana tokea zama hizo VITA baina ya LOWASA na MALECELA haiwez kuisha kamwe,kwan mambo waliyofanyiana wawili hao yanatishaa.

Hiyo ndiyo siasa ya bongo ilivyo,DO OR DIE.
Source:Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndio mzee wa Richmond!

    ReplyDelete
  2. If thats true, the i can understand why, bt mzee must be very stupid, ukifanya deal na ukspigwa bao hua hatunununi piga ingine, atakufa na kihoro huyu mzee, amewahi kuitwa Omary ili awe mtu fulani sasa keishney.

    ReplyDelete
  3. Kaandike kitabu

    ReplyDelete
  4. tatizo la watanzania ni UNAFIKI.viongozi almost wote ni wezi..then huyo mzee mbona haeleweki? nafikiri mwisho wa cku watz wataamua ni nani wanamuhitaji na huyo mzee c msemaji wa watz

    ReplyDelete
  5. Poa tu ccm, nyie pigeni madili ya kufa mtu wadanganyika bado wamelala na wahenga walisema alalae usimwamshe.

    ReplyDelete
  6. Ok nahic badae JK akainasa ndio mana alishasema mzee richmond hafai kuwa Rais sio mwaminifu tena mbinafc mpeni kura awe rais atauza nchi aende zake ulaya

    ReplyDelete
  7. Mdogo mdogo, mpaka mwakani tutajua yote.

    ReplyDelete
  8. Alie msafi ndani ya CCM nani?

    ReplyDelete
  9. Mdaku u made my dei hahahahah

    ReplyDelete
  10. Hiki chama cha SISEMI wanaogopana nani watu wamajungu kupita.wanaingoza serikali na vyombo vyote vya dola, wanaitana mafisadi lkn hakuna anaepelekwa mahakani.

    ReplyDelete
  11. Lowasa atulie tu kama pesa tayari anazo za kumtosha sasa anataka kutumaliza kabisa jamani hatumtaki no mwizi sana mjanja sana kila nafasi anayokuwepo lazima apige pesa ya kufa mtu hafai hata kidogo nyie wakina ney wamitego mnaomfagilia hamumjui kwani mlikuwa wadogo wakati wake huyo mshua ni noma kwa wizi hafai

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha aibe.watu wenyewe wamelala.

      Delete
  12. sisiem, sisiem, sisiem

    ReplyDelete

Top Post Ad