WATOTO WALIO ZALIWA WAMEUNGANA WAREJEA DAR BAADA YA KUTENGENISHWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watoto pacha, Elikana na Eliud waliokuwa wameungana wamerejea nchini jana wakitokea India walipokuwa kwa ajili ya kutenganishwa, tayari kwa kusherehekea kumbukumbu yao ya kutimiza mwaka mmoja leo.

Waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 10:30 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Oman, wakiwa na mama yao, Grace Joel (20) ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.

Elikana na Eliud walizaliwa Februari 20, mwaka jana wilayani Kyela, Mbeya wakiwa wameungana na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambako walipata rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Juni mwaka jana, Serikali iliwapeleka Hospitali ya Chennai, India ambako Desemba 16, mwaka jana walifanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha.

Akizungumza baada ya kutua jana, Grace alisema: “Nina furaha ya ajabu, sijui nimshukuru vipi huyu Mungu wangu, ni mkuu mno. Ninawashukuru sana madaktari wa India, ninawashukuru madaktari wa Muhimbili na sana naishukuru Serikali yangu kwa kunipa msaada huu mkubwa. Siamini kama leo ningekuwa narudi salama na watoto wangu kila mmoja akijitegemea,” alisema Grace.

“Kesho (leo) ni birthday yao, wanatimiza mwaka mmoja, ni furaha ya ajabu niliyo nayo, siwezi kuelezea. Siku nilipoambiwa watoto wangu watafanyiwa upasuaji mkubwa na watapumulia mashine kwa wiki moja, nilichanganyikiwa kwa kweli, sikutamani tena hata hiyo operesheni ifanyike ila sikuwa na jinsi zaidi ya kumwomba Mungu.”

Akizungumza uwanjani hapo, Dk Glory Joseph kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando ambaye aliongozana na watoto hao kurudi nchini alisema: “Watoto wamerejea salama na wanaendelea vizuri ila watakuwa Moi (Hospitali ya Mifupa Muhimbili), kwa uangalizi maalumu mpaka hapo madaktari watakapoona inafaa ndipo watapewa ruhusu ya kurudi nyumbani kwao Mbeya.

“Agosti watarudishwa tena India kwa ajili ya upasuaji katika njia ya mkojo na kufunga sehemu ya utumbo,” alisema.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema upasuaji wa watoto hao ulichukua saa 18. Katika muda huo, saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo, sehemu ya utumbo mpana, njia ya mkojo, kibofu na sehemu ya uume, wakati saa tano zilitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.

Pacha hao walifanyiwa upasuaji na madaktari 20 na wataalamu wengine wa afya ambao walitumia saa 18 kuwatenganisha. Kiasi cha Sh100 milioni kilitumika.

Meneja wa Huduma za Wagonjwa wa Kimataifa wa hospitali hiyo, Senu Sam alizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen juzi na kusema wamefanya sherehe kwa ajili ya mafanikio ya upasuaji huo.

Sam alisema pacha hao wameonana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, wiki tatu baada ya upasuaji... “Imekuwa faraja kuwaona wakitazamana. Eliudi alivishika vidole vya mkono wa Elikana na kuvichezea. Wanaonekana kufurahia mazingira mapya,” alisema Sam.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eee mungu wasaidie watoto hao wapone na waishi maisha yao

    ReplyDelete
  2. Mungu ni mwema sana, azidi kuwapigania na kuwalinda siku zote.

    ReplyDelete
  3. asante Bwana yesu kwa uponyaji wako, endelea kuwainua hawa watoto waje wakushuhudie kama wewe ni BWANA.

    ReplyDelete
  4. Mungu awakuze na kuwapa Afya njema Elikana&Eliud Love all baby (Happy Birthyday boyz)

    ReplyDelete
  5. Glory be to God, Happy birthday to twins

    ReplyDelete
  6. all the best mumy and ur sons...happy birthday.

    ReplyDelete
  7. To God be the glory.

    ReplyDelete
  8. LIHIMIDIWE JINA LA BWANA UWEZA NA UKUU NI WAKE YEYE

    ReplyDelete
  9. Mungu ashukuriwe amina.

    ReplyDelete
  10. Mungu ni mkubwa na hakuna linaloshindikana kupitia yeye mungu awajaalie afya njema

    ReplyDelete
  11. Kwa Mara ya kwanza nawapongeza wachangiaji wote wa comment hakuna matusi ila kumsifu Mungu

    ReplyDelete
  12. sure God is Gud all da tym tupo pamoja na ww mama kurwa na doto tunakuombea ww pamoja na familia yako.Mungu bariki madaktar wote wa india na wabariki wale waliotoa msaada huu sana bariki serikali ya tanzania na.madaktari.wa tanzania.waliochangia matibabu ya kurwa na.doto.

    ReplyDelete
  13. Thank u Lord umewasaidia na kurud kuja kucellebrate birthday na mm, I wSh u guyz a very long lyF

    ReplyDelete

Top Post Ad