GAZETI LA MWANANCHI LAMUOMBA RADHI RAIS KIKWETE

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jana katika gazeti hili tulichapisha habari iliyokuwa ikielezea kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwatembea wagonjwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) jijini Dar es Salaam.

Katika habari hiyo tuliwataja aliowatembelea kuwajulia hali kuwa ni Rajab Maranda, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kwa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), pamoja na mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Salum Mkambala.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imeeleza kuwa Rais Kikwete hakwenda kumuona Maranda bali aliwatembelea wanahabari wawili ambao ni Salum Mkambala wa Channel Ten aliyelazwa wodi binafsi D, na Margaret Chambiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyelazwa wodi binafsi .

Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa Rais Kikwete aliwajulia hali wagonjwa wengine wawili, John Mhina na Reuben Nyanga ambao wako chumba kimoja na Mkambala.

Tunachukua nafasi hii kuomba radhi kwa Rais Kikwete kwa usumbufu ambao ameupata kutokana na habari hiyo.

CHANZO: Mwananchi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msirudie tena kubuni habari tutawafungia.

    ReplyDelete
  2. Dunoma sanaaaaaa!

    ReplyDelete
  3. Hebu muacheni mh.rais apumue jamani,anahitaji pongezi kubwa kwa kazi anayoifanya na sio huu upumbavu wenu mnaobuni mkikosa habari,pumbavu sana..

    ReplyDelete
  4. Mwananchi hivi hamjui kuwa kama hujachunguza habari kwa kina na kupata uhakika, huna haki ya kuongea? Kuweni makini, na uandishi wenu. Mnadhalilisha watu.

    ReplyDelete
  5. Ukanjanja. Wanamchafua mtu makusudi kisha wajifanya kuomba radhi kwa unafiki

    ReplyDelete
  6. Mh nae hatulii kutwa hospitali kutwa kufungua barabara kutwa safari za nje.Enzi za Mwalimu ulikuwa haumsikii hata miezi sita.Mambo ya misiba na kwenda hospitali angemuachia Pinda.

    ReplyDelete
    Replies
    1. asipofanya hivyo mtasema, akifanya mnasema watanzania hamna shukurani kabisa na wala hamna jema, mkibebwa nishushe mkishushwa nibebe lo

      Delete
    2. wakati wa mwalimu ulikuwepo? acheni ujinga acheni atimize wajibu wake!

      Delete
  7. Wewe ndio chizi kabisa

    ReplyDelete
  8. Mchunguzeni mwandishi wenu habari aliipata wapi?

    ReplyDelete

Top Post Ad