IKULU YAMTAKA ASKOFU KAKOBE AACHE POROJO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema haina muda wa kujibu porojo zilizotolewa na Askofu wa kanisa la Full Gospel Fellowship, Zachary Kakobe kwani ina kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Imesisitiza kuwa ofisi ya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu haifanyi kazi za porojo kama sehemu ya kuendesha utawala wake, badala yake iko makini kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kwa kulinda na kuheshimu demokrasia na kufuata katiba ya nchi.

Kauli hiyo inatokana na waraka maalumu unaodaiwa kutolewa na Askofu Kakobe na kisha kupelekwa Ikulu.Hata hivyo, kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema haijathibitisha rasmi kama waraka huo umefika katika ofisi hiyo.

Akizungumza juzi na gazeti la Jambo Leo kwa njia ya simu,Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu alisema serikali si lazima ijibu Porojo zilizotolewa na Kakobe, kwani Ikulu ni sehemu nyeti ya kutumikia wananchi katika maswala ya msingi na yenye tija kwa taifa.

"Yaani unataka niseme mambo ya porojo badala ya kuelekeza majibu yenye kutatua matatizo ya wananchi",

alisema na kuongeza kuwa swala hilo lilishajibiwa na kaimu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, Dr Florence Turuku ambapo alilitolea ufafanuzi wa kutosha.

Waraka huo uliotolewa kwenye vyombo vya habari na Askofu Kakobe ulikuwa ukieleza namna Ikulu "ilivyotupa kapuni" majina yote ya wapentekoste waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, hivyo kuwafanya wapentekoste takribani milioni 10 kukosa mwakilishi hata mmoja.

Pia waraka huo ulidai kuwa baada ya kukosa uwakilishi, Ikulu ilitoa kauli za kejeli kuwa, haijawahi kupokea jina hata moja la mpentekoste.

"Ofisi yako imeona kwamba ni haki hata kwa waganga wa kienyeji kuwakilishwa katika bunge hilo kuliko wapentekoste kupata mjumbe hata mmoja", ilisema sehemu ya waraka huo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti la Jambo Leo walisema Askofu Kakobe amezoea kulumbana na Serikali, hivyo uamuzi wake hauna mashiko.

"Tunajua ana waumini wengi wanaomsikiliza, lakini kwa maswala ya kiserikali ambayo inaaminika haina dini ni vigumu kuitabiria mabaya, kwani yeye kama mchungaji alistahili kukaa pamoja na ofisi husika na si kwenda kunukuu vitabu vitakatifu kwa kuitabiria mabaya serikali",
Alisema Patrick Haule ambaye ni Mwinjilisti. 

Chanzo: Gazeti la Jambo leo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. naomba kuuliza kwa anayeejua kanisa lake linaendelea

    ReplyDelete
  2. yeye ajaitabiria serikali..katabiria watu ambao wameishika hiyo serikali..muwe mnaelewa basi hata kama mamentally...yeye kasema kapewa ujumbe na kaufikisha na ajaomba majibu kutoka kwenu..midomo juu,,,Mlikuwa wapi toka mwanzo kuwa makini na ujenzi wa taifa la tz ndo muwe makini leo.

    ReplyDelete
  3. Kakobe msenge tu. Akatombwe zake Nigeria huko. Mwizi mkubwa

    ReplyDelete
  4. ana mapepo huyoo..atasubiri sanaaa..

    ReplyDelete
  5. Nana hongera kwa kumuelewa huyo mzee vizur kwani hata siku za nyuma manabii waliwatabiria wafalme wa nchi husika, endapo walienda kinyume na huadilifu wa kimungu, na ikawa kwmba walipoendelea kukaza shingo zao, MUNGU akaadhibu nchi yote kwa kosa la mtu mmoja au wawili

    ReplyDelete
  6. Nana hongera kwa kumuelewa huyo mzee kwani hata siku za nyuma wafalme wa nchi walipoenda tofauti manabii waliwatabiria mabaya, na kuendelea kukaza shingo zao kukapelekea madhara makubwa kwa nchi husika, hata kwa wale wasio na hatia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwendeni zenu na ufreemason wenu

      Delete
  7. Mimi hua siwashangai manabii hawa kina Kakobe. Mama Rwakatare. Mzee wa Upako nk. Mimi huwashangaa waumini wao zaidi. Hivi inawezekanaje ukawa very serious na makanisa ya hawa watu huku unajua fika ni wasanii tu? Wanachumia matumbo yao. Wao matajiri wa kupindukia kutokana na sadaka wakati waumini wao wanajazwa matumaini tu yaa HOPES huku ni masikini wa kutupa. Hii brain washing ya aina hii ni zaidi ya babu wa Loliondo bt people cant c. Ni vipofu. Jamani hakuna tajiri atakaeuona ufalme wa mbinguni. Mcha Mungu hawezi kuwa tajiri. Atapata wapi hela na akizipata hugawana na maskini kama alivyokuwa Mama Theresa wa India au hata Baba wa Taifa tu Mwl Nyerere. Hao ndio angalau wanaweza kuwa na sifa za ucha mungu hata kama kibinadam hawakukamilika. Lakini sio kina Kakobe. Rwakatare na Mzee wa Upako wale ni majambazi kiaina tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad