google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html KINANA ACHARUKA NA KUSEMA: WASALITI CCM WAKO KUMI | UDAKU SPECIAL

KINANA ACHARUKA NA KUSEMA: WASALITI CCM WAKO KUMI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema hana mpango wa kuwahoji Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana na chama hicho kwa sababu ya misimamo yao inayokinzana na miongozo ya chama, kwa kuwa anawafahamu wote kwa majina na idadi yao haizidi kumi.

Kauli hiyo ya Kinana inafuatia taarifa zilizoripotiwa na gazeti hili hivi karibuni kuwa, CCM kimeanza kuwahoji baadhi ya wabunge wake, ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu ya kupingana na maelekezo ya chama hicho kuhusu Muundo wa Serikali mbili.

 “Sisi (CCM) hatuhoji mtu kwa sababu ya kuwa na msimamo tofauti, kwani hawa wenye msimamo tofauti na chama hawazidi kumi ama siyo zaidi ya 15,” alisema Kinana na kuongeza;

“Hawa watu mimi nawajua kwa majina, mmoja (jina tunalo) ni hatari zaidi kwa sababu anaweza kuwakusanya wengine na kuwashawishi wafuate msimamo wake, lakini waliobaki wote, hawatishi kwa kuwa wanabaki na misimamo yao wenyewe.”

Kwa mujibu wa habari hiyo, wajumbe waliohojiwa ni wale wanaotokana na Ubunge wa Jamhuri ya Muungano na ambao wanataka Muundo wa Serikali tatu. “Ni kweli hata mimi niliitwa na akaniambia (mwakilishi wa chama) ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha ya watu 90 na nikiendelea na msimamo wangu nitachukuliwa hatua,” alieleza mmoja wa wajumbe waliodai kuwa wamehojiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Maelezo ya Kinana

Kinana aliliambia gazeti hili kuwa, kulingana na muundo wa chama hicho tawala, viongozi wanaoweza kuwahoji watu ni yeye Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa chama Taifa. “Tena tunafanya hivyo kwenye vikao maalumu na kwa sababu ambazo haziwezi kuwa siri.”

Kinana alieleza kuwa taarifa kwamba CCM imewahoji watu 90 kutokana na kuwa na misimamo tofauti na chama hicho kuhusu Serikali mbili na kura ya wazi, siyo za kweli na anaamini imesambazwa na watu kwa malengo yao binafsi. Kinana anafafanua kuwa CCM kama chama kikubwa nchini chenye wafuasi karibu nchi nzima, hakiwezi kudhibiti mitizamo ya watu na kimsingi tofauti za mitazamo ndiyo msingi wa demokrasia.

Novemba 20 mwaka 2012 akizungumza katika kipindi cha Jenerali on Monday kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Kinana alitoa onyo kwa makada wasaliti kuwa atasimamia utekelezaji wa uamuzi wa Halmashuari Kuu ya CCM (Nec) ya kuwabaini na kuwaondoa viongozi wanaokwenda kinyume na matakwa ya chama na kukipaka matope.

Kura ya wazi na Serikali mbili

Katika hatua nyingine, Kinana alizungumzia msimamo wa chama hicho wa kura ya siri na muundo wa Serikali mbili, akieleza kuwa siyo jambo la ajabu, kwani katika mchakato wa kutunga katiba, kila kundi lina maoni na mtazamo wake na kuutetea kwenye mijadala.

“Wanaosema kuna vyama havina msimamo pale bungeni ni waongo. Siyo vyama tu, kila kikundi kina msimamo unaotokana na uchambuzi wao wa hali ya siasa nchini na wanachofikiri kina masilahi kwa nchi na watu wanaofuata mtazamo wao. Hawawezi kuniambia kama Lipumba (Profesa Ibrahim) na Mbowe (Freeman), hawana wanachosimamia kwenye mjadala huo wa Bunge Maalumu,” alisema na kusisitiza:
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Badilika ww Mzee wacheni kuwa na mawazo mgando na kulazimisha mambo kuwa hivyo hivyo kila siku sababu ya kulinda maslahi ya matumbo yenu,Mjue kuna MUNGU tu na ufisadi wenu huo na atawachoma bila huruma wala hatowaacha,mnataka kuifanya nchi km yenu CCM mna hati miliki kakupenda NYERERE ama? shwain,,,,,,,Asotaka mabadiliko ni mjinga tu hata awe kasoma vp,hamna maendelea yatakayokuja bila mabadiliko...Imefika wkt CCM KUONDOLE MADARAKANI,mmeturejesha nyuma sanaaa imetoshaaa....

    ReplyDelete
  2. CCM hawana huruma hata kidogo
    Watanzania tuamke , pilau ya siku moja inatutesa miaka mitano,

    ReplyDelete
  3. Ccm wote wasenge na mwaka kesho lazima mchekee choon pmbfu zenu

    ReplyDelete

Top Post Ad