KUMEKUCHA DODOMA"TAMKO LA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA WA KUNDI LA “TANZANIA KWANZA”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sisi Wajumbe Wa Bunge Maalum la
Katiba tunaotoka makundi mbalimbali na pia tunaoamini katika kauli mbiu isemayo “TANZANIA KWANZA”, tunapenda kutoa tamko rasmi la kuunga mkono hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais alipokuwa akihutubia Bunge Maalum la Katiba Tarehe 20/03/2014 kama ifuatavyo:

Kwanza, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa hotuba yake aliyoitoa wakati akizundua Bunge Maalum la Katiba tarehe 20 Machi 2014.

Tunaamini Rais, kama Mkuu wa Nchi, alikuwa na haki na wajibu wa kutoa mwelekeo na maono yake kuhusu Rasimu ya Katiba na hatua hii tuliyonayo sasa ya kuipitia Rasimu kwenye Bunge la Katiba. 

Tunafarijika kwamba hotuba hiyo imepokelewa vizuri na Watanzania wengi kwenye kila kona ya nchi yetu na wengi wao wamekuwa wakitutumia ujumbe wakituhimiza kuizingatia hotuba hiyo katika kutimiza wajibu wetu.

Pili, tunamshukuru Rais kwa uchambuzi wake wa kina wa Rasimu na ushauri wake kwetu kuhusu haja ya kuweka taifa mbele, kushawishiana kwa hoja kuliko kulazimisha hoja na haja ya kutunga Katiba itakayoliimarisha taifa letu na kuendeleza umoja na ustawi wa
Watanzania. Sisi wana TANZANIA
KWANZA tutaendelea kushawishi kwa hoja na wala hatutalazimisha.

Tatu, tumeshangazwa na hamaki
iliyoonyeshwa na baadhi ya wajumbe wenzetu kuhusu hotuba ya Rais.

Tunasikitishwa na kauli zao zenye
mwelekeo wa kuhujumu mchakato wa kupata Katiba mpya. Viongozi
hawahawa wanaotoa kauli hizi
walionekana wakishangilia hotuba ya Rais pale aliposema yale waliyokuwa wanakubaliana nayo. Iweje watishie vurugu na kususia kisa tu Rais kasema baadhi ya mambo wasiyokubaliana nayo. 

Ustahamilivu wa kidemokrasia,
ustaarabu na hekima ya uongozi na utu uzima hautaki hivyo.Hotuba ya Rais imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya Muungano wa Nchi yetu kwa hoja ili Watanzania wawe na fursa pana zaidi ya kutafakari na mwisho kuamua. 

Mheshimiwa Rais ametimiza kauli yake ya kushawishi kwa hoja na si kwa kulazimisha.

Nne, Hotuba ya Mheshimiwa Rais
haikuvuruga wala kuingilia mchakato uliopo mbele yetu. Rais hakuingilia kanuni za Bunge maalum
tulizozipitisha, Rais hakubadilisha
Sheria ya mabadiliko ya Katiba, Rais
hakupiga kura kwenye vifungu vya
Katiba, Rais ameanza kwa kuipongeza Tume ya Mh. Jaji Warioba na kuipongeza kuwasilishaji wake.

Alichokifanya Mheshimiwa Rais kama kiongozi mkuu wa Nchi mwenye hekima na busara na uchungu wa Nchi yake na kutambua dhamana aliyopewa na Watanzania wote bila kujali makundi ameelezea faida na hasara za mifumo ya Serikali iliyowasilishwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tume. Rais katupa moyo na kutuhimiza tumalize kazi haraka na
tuifanye kwa weledi huku tukiweka maslahi ya Taifa mbele. Hata pale
alipotoa maoni na ushauri kuhusu baadhi ya vifungu bado Mh.Rais
alisisitiza kwamba uamuzi wa mwisho ni wetu sisi Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Tano, dhana ya kuichambua na
kuikosoa rasimu maana yake si
kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe wake. Msingi mzima wa
kutolewa Rasimu hii ni kwamba
Wananchi tuichambue, tuikosoe,
tuirekebishe, tuiboreshe na hata ikibidi tuibadilishe na mwisho tutaipigia kura sote kwa pamoja. Rasimu haikuletwa kama Msahafu wala Biblia na ndiyo maana zimewekwa hatua mbili baada ya kazi ya tume kukamilika: 

BUNGE MAALUM LA KATIBA na KURA YA MAONI YA WANANCHI. 

Rais akiwa mkuu wa Nchi, naye ana nafasi yake katika mchakato wa Katiba. Sisi wana TANZANIA KWANZA, tunashukuru kwamba Mh. Rais alitutanabahisha kuhusu maeneo muhimu ya kuzingatia ambayo Tume haikuyaainisha kwa upana wake ikiwemo mipaka ya Nchi
yetu. Tunawapongeza Wajumbe wa tume kwa kazi waliyoifanya na kuikamilisha.

Kazi inayofuatia sasa ni uchambuzi wa Rasimu waliyoiwasilisha. Katika hatua hii ya sasa ya Bunge la Katiba, Rasimu hii inaweza ikakosolewa na hata inaweza kubadilishwa sana. 

Tunawasihi Wajumbe wa Tume waondokane na dhana kwamba kazi yao inapojadiliwa tofauti na mapendekezo yao siyo udhalilishaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Sita, Sisi Wajumbe wa Bunge Maalum, wana TANZANIA KWANZA ambao idadi yetu ni zaidi ya Wajumbe 400 na ambao orodha yetu tutaitoa hivi karibuni kwa
wingi wetu na umoja wetu tunayo
dhamira ya kutimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Sheria na kwa kuzingatia matarajio ya Watanzania. 

Tunawasihi wale wenzetu ambao hawakuipenda hotuba ya Mheshimiwa Rais watulie, waondoe hamaki na sote tushirikiane kuifanya kazi hii, kama wapo ambao kitendo cha Rais kuja kuhutubia na kutoa uchambuzi wake kuhusu Rasimu, kinawafanya wasitake tena kushiriki
katika mchakato huu, basi uamuzi wao huo waufanye kwa namna ambayo haitatukwaza au kutuzuia sisi wengine tunaotaka kuendelea na shughuli hii ya mchakato wa Katiba. 

Tunawasihi viongozi wa Bunge Maalum wasivumilie wala kuendekeza vitendo vya vurugu za
makusudi vitakavyozuia uendeshaji wa Bunge. Tunawasihi msiruhusu watu wachache wakaliweka rehani Bunge Maalum ili kutengeneza mtaji wa kisiasa. 

Tunawasihi Watanzania wawaone na kuwahukumu wale watakaotaka kuvuruga au kukwamisha mchakato adhimu wa kupata Katiba mpya kisa tu Mh. Rais kaja kuhutubia Bungeni.

Mwisho, tunapenda kusisitiza kuhusu umuhimu mkubwa wa vyombo vya habari katika mchakato huu. Hiki ni kipindi muhimu sana katika uhai wa Taifa letu. Wananchi wengi wanafuatilia mchakato huu kupitia vyombo vya habari. 

Tunawasihi wamiliki, wahariri na waandishi wa habari wazingatie
weledi wa hali ya juu sana katika
kuripoti mchakato huu. Wananchi
wanapenda kusikia, kuona na kusoma yanayojiri wala sio propaganda za wanasiasa au makundi mbalimbali.

Tunapenda kuvisihi vyombo vya habari viwaunganishe Watanzania wote katika kipindi hiki muhimu na cha kihistoria.

Hata hivyo tunatoa shukrani zetu za
dhati kwa vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ushiriki wao
katika mchakato huu wa Katiba. Tunazidi kuwasihi waendelee kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa, kutokufanya kazi kwa kufuata propaganda za kisiasa au kufuata makundi, kutoa mizania sawa kwa maoni tofauti bila kuegemea maoni ya kundi moja au matakwa ya makundi fulani kwa kuwa mwisho wa siku sisi sote tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunakuwa na Tanzania moja.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Libariki Bunge Maalum la Katiba

“TANZANIA KWANZA”

Tunawashukuru kwa kutusikiliza.

Kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Katiba “WANATANZANIA
KWANZA”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. pumbu zenu nyinyi mnafanya nchi hii kama yetu eti " tanzania kwanza" hapa ni Tanganyika mnaogopa tukigawana mali mlizoiba za Zanzibar mtashindwa kurudisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuna mali gani zanzibar ya kuziiba ardh yenyewe tabu kipi tuibe kama samaki hata bara wapo, acha kuropoka kitu usichokijua

      Delete
    2. Yani hao jamaa ndo zao , hawana lolote ni mdomo tu na roho mbaya.
      Nakwambia tukiuvunja muungano watamkimbilia mwarabu coz hawajiwezi hao.
      So sad people.

      Delete
  2. Huo ni unafiki, ukikuwa hamjui mnaenda kufanya nn? Au ndio kulipa fadhila za uteuzi

    ReplyDelete
  3. Mm binafsi muungano siukubali k7bu wazanzibr hapa tanganyika wako huru sana ila ss tukienda zanziba hata kama utakaa mwezi mmoja tu, mpaka utaondoka hutaenjoy kwani wananyodo sana ubaguz kwao unaendelea hadi kesho, uvunjwe muungano kwetu ss watangayika hauna faida 100%

    ReplyDelete
  4. Unafiki tu umewajaa. Kwani aliitwa afafanue rasmu au afungue bunge maalum. Hale ni maoni yake ambayo alitakiwa ayakusanye kwenye tume. Tuwe wakweli jamani tuache unafiki kisa tu tumepewa vijinafasi vya kwenda kula laki 3 kwa siku.

    ReplyDelete
  5. Na ninyi na hcho kikundi chenu cha "Tanzania kwanza" mnachokifanya ni unafiki mkubwa. Sasa kama mko 400 mnachongojea nini? pitisheni katiba muokoe kodi zetu, unafiki mtupu. Hivi nahisi mtu mzima ukishakuwa liccccmmm unakuwa umefungwa kila kitu, sh****--n kabisa na usirudie kupost ujinga kwenye mitandao ya kijamii.

    ReplyDelete

Top Post Ad