KURA YA SIRI, WAZI KAA LA MOTO BUNGE LA KATIBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, juzi na jana wamekuwa katika mtihani mgumu wa kufikia uamuzi wa pamoja kuhusu utaratibu wa upigaji kura, kati ya kura ya wazi na kura ya siri.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilisema kutokana na mvutano huo, mjumbe mmoja, Chritopher Ole Sendeka, alijikuta akilia hadharani akitetea upigaji kura ya wazi.

Kikao hicho kilichofanyika juzi kati ya saa 2:00 na saa 5:30 usiku chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kilishuhudia mabishano makali kati ya wanaotaka kura ya siri dhidi ya wale wanaotaka kura ya wazi.

Habari hizo zilisema baada ya Pinda kufungua kikao hicho, alimkaribisha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Shamsi Vuai Nahodha, ili atoe mrejesho wa kikao cha mashauriano.

Inaelezwa kuwa katika kikao hicho, Nahodha aliwaambia wajumbe kuwa kutokana na mazingira yaliyopo ndani na nje ya Bunge kwa upande mmoja na wananchi kwa upande mwingine, kura ya siri haiepukiki.

“Kilio cha Ole Sendeka kwenye party cocas kikao cha chama (party cocus) juzi usiku kilitokana na kauli ya Nahodha kwamba kura ya siri haiepukiki,” alidokeza mbunge mmoja wa CCM aliyehudhuria kikao hicho cha faragha.

Mbunge huyo alilidokeza gazeti hili kuwa ndani ya kikao kulikuwa na mabishano makali baada ya kauli ya Nahodha, huku baadhi ya wabunge wakisema wananchi wamechoshwa na msimamo wa CCM.

Ni kutokana na mabishano hayo ndipo Ole Sendeka aliposimama akipinga mapendekezo yaliyotaka CCM kulegeza msimamo na kuridhia kura ya siri na wakati alipokuwa akizungumza alipobubujikwa na machozi.

Huku akilia katika kikao hicho, inadaiwa Ole Sendeka akisema kwamba kukubali kura ya siri ni kuitosa CCM na msimamo wake wa kutaka muundo wa Serikali mbili.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa Ole Sendeka alienda mbali zaidi na kusema endapo Pinda ataridhia kura hiyo ya siri, basi yeye (Pinda) na viongozi waandamizi wa CCM waliohudhuria watawajibishwa na CCM.

Kutokana na mtafaruku huo, kikao hicho kilishindwa kufikia mwafaka na kuahirishwa hadi jana saa 5:00 asubuhi ambapo hoja ya ama kura ya siri au ya wazi, iliendelea kuwagawa wabunge katika makundi mawili.

Wakati akifungua kikao cha jana, Pinda alisema kutokana na yaliyotokea katika kikao chao cha juzi usiku na baada ya kutafakari kwa mapana yake, chama kimeamua kibakie na msimamo wake wa kura ya wazi.
Kutokana na yaliyojitokeza jana (juzi) na hasa ukiona mtu mzima analia, tumetafakari tumeona tubaki na msimamo wa kura ya wazi,” alisema mmoja wa wabunge akimkariri Waziri Mkuu Pinda.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, katika kikao hicho ilielezwa kuwa kukubali upigaji kura wa siri ni kuiua CCM kwa sababu wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la Katiba, watapitisha muundo wa Serikali tatu badala ya mbili.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamehoji kitendo cha Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kuhudhuria kikao cha ndani cha wabunge wa CCM.

“Kificho ni mwenyekiti wa Bunge lenye makundi tofauti, sasa anapoingia kwenye kikao cha wabunge wa CCM kinachoweka mikakati ya kupingana na makundi mengine anatoa picha gani?” alihoji mbunge mmoja.

Taarifa za Kificho kuhudhuria kikao hicho cha jana cha CCM zilionekana kuwakera wajumbe wengine wa Bunge hilo, wanaotokana na vyama vya upinzani na wale wanaotoka katika kundi la wajumbe 201.

“Bado tunatafakari tuchukue uamuzi gani, lakini tukiona vipi, tutasusia kikao cha leo (jana) jioni, nyie njooni ndani lolote linaweza kutokea,” alidokeza mjumbe huyo anayetoka katika kundi la vyama vya hiari.

Kura ya siri, wazi yawekwa kiporo

Hata hivyo, jana mara baada ya Kificho kuanza kikao cha semina saa 10:40 alasiri badala ya saa 9:00 alasiri alisema semina hiyo imechelewa kuanza kwa sababu ya masuala muhimu.

Kificho aliwaambia wajumbe kuwa kamati ya mashauriano ilikuwa imemshauri kanuni ya 37 na 38 zinazohusu kura ya siri viwekwe kiporo kutokana na kutopatikana kwa mwafaka.

“Kamati imenishauri bado tuache kanuni ya 37 na 38 ili kamati ya mashauriano iendelee kunishauri vizuri zaidi ili baadaye tuje tuwaambie kamati ya kanuni iziandike vipi,” alisema.

Kutokana na ombi hilo, wajumbe waliafiki waendelee kupitia kanuni ya 32 hadi 36 na 39 hadi 43 ambavyo havina mvutano.
Mwananchi

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hili bunge la katiba kweli majanga kitu kidogo tu cha kutoa uamuzi wanashindana nacho nakupoteza muda je hayo mambo makubwa yanayokuja sijui itakuaje kama ni hivi miezi 3 haitoshi.

    ReplyDelete
  2. Huyu sendeka nae alikuwa ana hamu ya kulia ajalia muda mrefu kashalitia gundu bunge la katiba.

    ReplyDelete
  3. Sendeka anafirwa tu hana lolote. Hivi mtu na akili yako timamu kabisa unaweza lilia serikali 2 kweli. Kwa faida ipi hasa. Wazanzibar wenyewe hawataki cc tunalazimisha lazima anatiwa huyu mzee.

    ReplyDelete
  4. Wafunge hilo bunge hakuna wanachofanya

    ReplyDelete
  5. wasenge kweli.Kura siku zote za siri.kura za wazi kwani wanachagua mcheza shoo bora.

    ReplyDelete
  6. Huyo sendeka kuma la mama yake msenge mkubwa. Anajifanya analia analia nn mnafki mkubwa huyo halafu watanzania mjue hawa watu mule mjengon wanao sumbua n kama wanne hiv hawa nazan ndo wameambiwa wakibebe chama. Watu hao n sendeka,selukamba,umi mwalm, pamoja na jamaa moja jna limenitoka lkn n mbunge wa dodoma hawa wote n viaz

    ReplyDelete
  7. Mwisho wa siku tunaotaka kura ya siri tutashinda nyie jikanyageni na hivyo vikao visivyoisha

    ReplyDelete
  8. ccm kama wanazuga hivi ili waibe kura ktk hiyo kura ya siri wanacheza na akili za watu halafu wanakubali kura ya siri halafu washindi wao

    ReplyDelete
  9. Hivi katba ni ya ccm au ya wananch? Tunatambua kwamba ccm wana katiba yao sasa kwanin wanang'ang'ania selikali mbili? Ufisadi uo

    ReplyDelete
  10. Wanavuta muda kijanja ili wapate pesa nyingi. Bunge hili wizi tuu

    ReplyDelete
  11. Kura ya wazi au siri vyovyote vile SAMUEL SITTA ndio mwenyekiti wa bunge la katiba mnapoteza muda bure.

    ReplyDelete
  12. Watu wengi duniani wanaombea mabadiliko yanayoendelea afrika Tanzania kuhusu katiba,watanzania walioko Finland,Usa,Ujerumani,Canada,'Uk,etc
    Walio chaguliwa wasicheze na muda,Mungu akikasirika sijui?mtaisikia dodoma kama hadithi,muwe makini,na maisha ya Watanzania

    ReplyDelete

Top Post Ad