MAPOLISI WAIPEKUA NYUMBA YA RUBANI WA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuala Lumper. Polisi nchini Malaysia wamevamia nyumba aliyokuwa akiishi rubani wa ndege iliyopotea na kuendesha msako mkali, ikiwamo kukusanya nyaraka muhimu ambazo zinazamiwa kuwa zitasaidia kufichua ukweli kuhusu tukio la kupotea kwa ndege hiyo.

Ripoti zilisema kuwa upekuzi huo, ambao pia umefanyika katika nyumba aliyokuwa akiishi rubani msaidizi, umefanyika baada ya kuibuka kwa taarifa zinazodai kuwa rubani huyo, Zaharie Ahmad Shah alikuwa na mrengo wa siasa kali.

Shah alikuwa ni shabiki na mfuasi wa wazi wa mwanasiasa wa upinzani, Anwar Ibrahim ambaye sasa yupo gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na vitendo vya fedheha.

Inaaminika kuwa rubani huyo alikuwapo mahakamani wakati mwanasiasa huyo alipopandishwa kizimbani mwezi Machi mwaka huu na pengine hakufurahishwa na hukumu hiyo.

Kwa sasa polisi wanashikilia nyaraka kadhaa, ikiwamo kompyuta ambayo inadhaniwa kuwa na taarifa muhimu zilizohifadhiwa na rubani huyo.

Polisi hao wameenda mbali zaidi kwa kuanzisha uchunguzi wa kimazingira ambao utasaidia kupata historia binafsi kuhusu maisha ya rubani huyo aliyetajwa kuwa na uzoefu mkubwa wa urushaji wa ndege.

Wataalamu wa saikolojia na wale wanaohusika na usalama wa anga wameitwa kuongeza nguvu ili kusaidia kuchambua taarifa zinazoendelea kukusanywa kuhusu mwenendo wa rubani Shah ambaye nyumba yake bado inaendelea kulindwa.

Kitendo cha polisi kuifanyia upekuzi nyumba ya rubani huyo pamoja na kukusanya taarifa zake binafsi kimeelezwa kwamba ni jitihada za Serikali kutaka kujiridhisha hasa kutokana na mazingira yanayohusisha upotevu wa ndege hiyo.

Wachunguzi hao wanataka kujua kama kumekuwa na tukio lolote la matatizo ya kiakili na kumewahi kujitokeza kwa changamoto za kifamilia kwa marubani hao au kwa yeyote aliyekuwamo kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Kuala Lumpur na kuelekea Beijing.

Pamoja na kwamba marubani wa ndege hiyo ya Malaysia walikuwa na rekodi nzuri, kuna wasiwasi pengine walikutwa na tukio lililosababisha kujiingiza kwenye hali ambayo ingepoteza umakini wa kuongoza ndege.

Uchunguzi pia unawalenga abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo iliyokuwa na umri wa miaka 11 na kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia upatikanaji ukweli halisi juu ya tukio hilo.

Serikali yaomba msaada
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu awarehemu kama wamekifa na pia awape moyo wa subra wote waliopotelewa na ndugu zao

    ReplyDelete
    Replies
    1. WAMESHA KUFA HAO,DEAL NA MAMBO MENGINE SASA

      Delete

Top Post Ad