MBOWE, LIPUMBA NA MBATIA WAMEFIKIA MWISHO KUONGOZA SIASA ZA UPINZANI"WAMELALA"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari namna viongozi hawa wanavyoongoza harakati za kuleta mageuzi nchini na nimegundua kuwa viongozi hawa wameshapoteza ujasiri na uwezo wa kuendesha harakati za kudai mabadiliko.Kwa maneno mengine,viongozi hawa "wamechoka" au tuseme "wamechuja".

Kuna jambo ambalo tunapaswa kulitambua nalo ni kuwa "uwezo wa viongozi wa upinzani kuendesha harakati za mabadiliko is always inversly proportinal to time".Ufafanuzi rahisi wa kauli hii ni kuwa kadiri muda unavyokwenda ndivyo kadiri uwezo wa viongozi hawa kuendesha harakati za mageuzi unavyoshuka.

Viongozi hawa siku hizi wamekuwa "legelege" hata kushindwa kuwa na misimamo "thabiti" kwa mambo ya msingi na matokeo yake wamejikuta wakiburuzwa na chama dola na kuishia kuwa walalamikaji tu.

Kwa mfano,siku hizi hata maandamano yamekufa.Likitokea jambo zito na wakapanga kuandama,wakiitwa na IGP na kufanya kikao utasikia maandamano tumeyasitisha.

Mfano mwingine ni pale panapokuwa na jambo serious kama vile sheria ya mabadilo ya katiba n.k.Siku hizi mivutano juu ya mambo kama hayo yakitokea ndani ya bunge,wanaitwa Ikulu,wanawekwa sawa na baada ya hapo wanabadili misimamo alafu mwisho wa siku wanageukwa wanaishia kulalama bila kuchukua hatua.

Hata kwenye hili Bunge la katiba,nako mambo ni yale yale tu.Walikuwa na msimamo ianze hotuba ya raisi ndio ifuate hotuba ya Warioba lakini walipowekwa sawa na mwenyekiti wa Bunge hilo,bwana Sitta wakabadili msimamo na matokeo yake jana kila mtu ameyaona kwenye hotuba ya Jk.

Lipumba wa leo sio tena yule alieongoza ile CUF ya "jino kwa jino".Halikadhakika,Mbowe wa leo sio yule Mbowe alieongoza CHADEMA iliokuwa na "slogan" ya "opetation sangara","m4c" ya miaka hiyo n.k.Mbatia ndio kabisa amebaki kuwa mzee wa busara zisizo na tija.

Viongozi hawa siku hizi wamegeukia siasa za kistaarabu na maneno matamu huku wenzao(CCM) waki-take advantage ya busara zao kuwaburuza.

Nimakizie kwa kusema tu,baada ya miaka michache,Mbowe,Lipumba na Mbatia watakuwa kama Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP.

Mbowe,Lipumba na Mbatia are no longer strong enough to lead "effectively" opposition political parties.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unaongea usichokijua na waambie waliokutuma

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa nini? Kila siku mtu akiandika au kusema ukweli ametumwa. Nyie vipi?????

      Delete
  2. Kweli tupu wamelala usingizi wa pono

    ReplyDelete
  3. Mbona unaongea kama upo na hawala ako,nafikiri wote wana mawazo ya kibadidu kama yako,kabla huja andika upuuzi wako tulishajua.

    ReplyDelete
  4. Ukiona kobe kainama, anatunga sheria, huu ni usemi wa wazee wa siku za nyuma, ila vijana wa sasa hv tunajua kwmba tukiona kobe kainama huyu amesinzia, so ukwl hawa jamaa walianza moto sana, ila vailas kafanya kazi kwenye vichwa vyao wamepoteza muelekeo na nguvu ya kisiasa haipo tena kwnye vyama vyao, R I P. MBOWE, LIPUMBA & MBATIA

    ReplyDelete
  5. NI KWELI WAMELALA KWANZA WALIGOMA WARIOBA ASIWASILISHE WAKAITWA WAKALAINIKA WAKARUHUSU ALAFU LEO WANASEMA ETI RAIS KAMJIBU WARIOBA NI UPUMBAVU MTUPU WALIPASWA KUHAKIKISHA RAIS ANAANZA LEO HII ETI WANAIPONDA HOTUBA YA RAIS WATAISHIA KULALAMA TUUU....

    ReplyDelete
  6. Tuko pamoja anoy 5;44

    ReplyDelete
  7. kuna ukwel ndan yake kwa kinachoongelewa,mwanzo wao na sasa kuna tofauti kubwa sana kwao kisiasa.

    ReplyDelete
  8. yeah! ni kweli makeke yamepungua , anasema ukweli c kwamba kila anaekosoa vyama vya upinzani katumwa na ccm

    ReplyDelete
  9. ukitazama kwa makini kuna point hapa

    ReplyDelete
  10. Tanzania hakuna chama cha upizani kama alishidwa mrema na maalimu Seif basi tema. Wanaanza kwa kasi kubwa ila ndiyo mbio za sakafuni hazifiki ukingoni.

    ReplyDelete
  11. Mbatia huwa anapoint muhimu na mawazo yake au hoja zake huea zinalenga utaifa na siyo chama kama wapizani wengi ni kupinga kila.kitu

    ReplyDelete
  12. Kweli!anon 2:18 pm.......kama ili hoja yake ya ardhi iliyoko mtwara na idadi ya watu ikigawanywa kila raia ana uwezo wa kupata ekari kumi na mpaka kubaki akiba kwa vizaz vijavyo na kuongeza kwamba kwa wale investors wanaokuja kutaka kuwekeza mtwara kupata ardhi raia nae anahusika so serikali inakuwa kati ya raia na mwekezaji......kidogo inakuwa mtanzania nae anaweza kunufaika na ardhi yake........tofauti na sasa............hoja wanazo sema wanakosa sapoti sababu ya upinzani wao ila ilitakiwa ichukuliwe kama changamito kwa chama tawala kufanya kazi na upinzani panapo tolewa hoja za msingi za manufaa ya taifa ....safi raisi alivyomchagua kuingia bungeni ila bado haitoshi bila utekelezwaji wa hoja....sio kila hoja pinzani inapingwa .......ili uendelee kuvimbisha vitambi vyenu.......tunataka baada ya uchaguzi mnakaa pamoja na kuleta maendeleo kwa manufaa ya taifa nzima la tanzania na hata wawekezaji wananyokuja kuwekeza wajue taratibu,sheria na kanuni za uwekezaji sio kama sasa Mtu anamkamata tu mwekezaji wanaingia ubia ardhi Kwa fedha kesho mmepishana kidogo mwekezaji unamfukuza na wakati kashawekeza kwenye ardhi yako kama matukio tunayosikia yanatokea Zanzibar wawekezaji wananyongwa na kufukiwa mpaka ikigundulika mwekezaji kapoteza maisha ......tunawatisha wale wawekezaji wenye moyo WA kuwekeza tanzania na mtanzania akanufaika...........niishie hapa......tushirikiane wote kuijenga tanzania Kwa pande zote haijalisha Chama tawala au pinzan.....tanzania ni heaven of piece tudhihirishe Kwa vitendo.....
    Sipendelei kuona watanzania wenzetu ambao wanaitwa wapinzani wanavyopigwa na kuuliwa Kwa kusimamia haki...sasa wanaweza kukaa chin wakubwa WA nguvu ya Dola na kuwazuia wasitishe maandamano .....safi wametambua nguvu ya vyama pinzani........ila cha msingi ni kutekeleza hoja za msingi zenye manufaa ya taifa haijalishi imetoka chmama pinzani ama tawala...............

    ReplyDelete
  13. Additional to Anon 12:08 kiingereza rahisi hata Kwa ndugu zangu tuliokimbia shule........na hii ndio Chama tawala na pinzani wanatakiwa kuelewa..............
    "Power is really fear that leads to manipulation and control of others, which in turns leads to violence and suffering. Real power comes from connection to our deepest self to what is real." Freedom not a choice it's a must.............by burningspearmusic.......msidharau wanamziki wengi wao wametangulia wako mbele ya haki ila tunatumia maono yao..........

    ReplyDelete
  14. Eti hawaandamani....., hebu waandamane waone! Umesahau ile ruksa ya 'PIGENI, TUMECHOKA'. We'wachochee, wakione cha moto, maana inaelekea 'umemiss' vurugumechi, makanjanja mnakosa chakuandika.

    ReplyDelete

Top Post Ad