google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html MCHEZA MPIRA TAMBWE ATANGAZA KUONDOKA SIMBA | UDAKU SPECIAL

MCHEZA MPIRA TAMBWE ATANGAZA KUONDOKA SIMBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Sweetbert Lukonge
STRAIKA wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe huenda akavunja mkataba wake na klabu hiyo na kuondoka zake mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, ikiwa timu hiyo haitapata nafasi ya kuwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa.

Tambwe ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 19, amesema kuwa matarajio yake wakati anajiunga na klabu hiyo yalikuwa ni kuiona ikishiriki mashindano ya kimataifa, hivyo kukosa kushiriki michuano hiyo kutamtibulia mipango yake na ametamka wazi anafikiria kuondoka klabuni hapo.

Simba ipo katika nafasi ya nne na haina matumaini ya kushika nafasi ya kwanza wala ya pili kwa kuwa imesaliwa na michezo minne, ambapo imezidiwa pointi 10 na Yanga inayoshika nafasi ya pili.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe, raia wa Burundi alisema hatma yake ya kuendelea kubakia Simba itajulikana baada ya kumalizika kwa ligi ya msimu huu ambayo ipo katika hatua za lala salama.
Alisema anaweza kuondoka au asiondoke Simba lakini alisisitiza kuwa kila kitu kitajulikana baada ya Aprili 19 ambapo ligi itakuwa inafikia tamati.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad