"RAIS KIKWETE ALIKUWA SAHIHI HAKUKOSEA" KUNDI LA TANZANIA KWANZA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KITENDO cha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kukosoa hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutoa maoni yake kuhusu rasimu ya Katiba, kimekosolewa.

Pia, imesisitizwa kuwa hakukosea kufanya hivyo na kwamba hotuba yake, haikuvuruga wala kuingilia mchakato ulio bungeni.

Kundi la Wajumbe wa Bunge Maalumu, linalojipambanua kama Tanzania Kwanza, limesema Rais alichofanya kama kiongozi wa nchi mwenye hekima na busara na uchungu kwa nchi yake ni kueleza faida na hasara ya mifumo ya serikali, iliyowasilishwa kwenye rasimu ya Katiba.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, wajumbe wa kundi hilo linaloongozwa na Said Nkumba na Dk Emmanuel Nchimbi, walisema kitendo cha Rais kuchambua rasimu, si kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba na wajumbe wake.

Wajumbe wanaounda kundi hilo wako 400 na waliozungumza jana na waandishi wa habari jana ni Nkumba, Nchimbi, Evod Mmanda, Seleman Jaffo, Mahmoud Thabit Kombo, Asha Mtwangi, Amon Mpanji na Waride Jabu.

Akisoma tamko la wajumbe hao, Said Nkumba alisema Rais hakubadilisha sheria ya mabadiliko ya Katiba, hakupiga kura kwenye vifungu vya Katiba, bali alieleza faida na hasara ya mifumo ya serikali, iliyowasilishwa kwenye rasimu ya Katiba na kuachia wajumbe kazi yao.

Nkumba alisema Rais Kikwete kawapa wajumbe moyo na kuhimiza wamalize kazi haraka na waifanye kwa weledi huku wakiweka maslahi ya taifa mbele.

“Hata pale alipotoa maoni yake kuhusu vifungu vya rasimu hiyo, alisisitiza kuwa uamuzi wa mwisho ni wetu sisi wajumbe wa Bunge hili.”

Katika hotuba yake, Rais alisema msingi wa kutolewa kwa rasimu ni kuwezesha wananchi waichambue, waikosoe, wairekebishe, waiboreshe na hata ikibidi waibadilishe na mwisho wapige kura kwa pamoja.

Rais Kikwete alisema rasimu hiyo haikupelekwa bungeni kama Msahafu wala Biblia na ndiyo maana zimewekwa hatua mbili baada ya kazi ya Tume kukamilika.

Kundi hilo la wajumbe, limesema Rais akiwa Mkuu wa Nchi, pia ana nafasi yake katika mchakato wa Katiba “Sisi wana Tanzania Kwanza tunashukuru kwamba Rais alitutabanaisha kuhusu maeneo muhimu ya kuzingatia ambayo Tume haikuyaainisha kwa upana wake ikiwemo mipaka ya nchi yetu.”

Alisema pamoja na kazi nzuri, iliyofanywa na Tume, rasimu hiyo inaweza kubadilishwa na kufanya hivyo siyo kuwadhalilisha wajumbe wa Tume hiyo.

Mwenyekiti huyo alisema wajumbe watimize wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia matarajio ya Watanzania.

Umoja huo ulitaka watu ambao hawakufurahishwa na hotuba ya Rais, waondoe hamaki, watulie na washirikiane kufanya kazi ya kuandika Katiba mpya.

Nkumba alisihi Watanzania kutoruhusu watu wachache, kuweka Bunge Maalumu rehani kwa malengo ya kutengeneza mtaji wa kisiasa.

“Tunataka Watanzania wawaone na kuwahukumu wale watakaotaka kuvuruga au kukwamisha mchakato adhimu wa kupata Katiba mpya kisa tu Rais kaenda kulihutubia Bunge hilo,” alisisitiza.

Juzi viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walikutana na kushutumu kile walichodai hatua ya Rais kuhutubia Bunge hilo na kutoa maoni yake kwa kuichambua rasimu wakati yeye siyo mjumbe wa Bunge hilo.

Walisema walikerwa na kitendo hicho, wakidai kinaonesha wazi kwamba CCM haina utashi wa kuandika Katiba kwa maridhiano, bali kwa kutumia ubabe ukiwemo wa kuvuruga Katiba.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad