SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA KWA AGNESS MASOGANGE LAIBUKA UPYAAA.. WAZIRI ATAKA AKAMATWE NA AHUKUMIWE KWA KOSA HILO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAZIRI Kivuli wa Mambo ya Ndani, Vincent Nyerere ameibuka na kutoa kauli ya kutaka Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ akamatwe na kuswekwa ndani akidai kitendo cha kuachiwa huru Afrika Kusini kwa kesi ya madawa ya kulevya si sahihi kwa Bongo.
 
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Vincent Nyerere.
Akizungumza na Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani Jumatatu usiku na Runinga ya ITV, Nyerere alisema baada ya uchunguzi kufanyika ilibainika kuwa yale madawa kwa nchini Afrika Kusini si ya kulevya lakini kwa Tanzania ni ya kulevya.
Alisema kutokana na kubainika kwamba yalitokea nchini,  baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar walitimuliwa kazi, akasema basi ilikuwa lazima Masogange baada ya kutua Bongo akamatwe.


“Mimi nimeshangaa sana jamani, ilikuwaje watu watimuliwe kazini pale uwanja wa ndege kwa kuwatuhumu kuruhusu madawa ya kulevya kupita, kwa nini walimuachia huru yule binti (Masogange), basi waliofukuzwa nao warudishwe kazini,” alisema Nyerere.
Paparazi wetu, juzi alifanya jitihada za kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe lakini simu yake ilikuwa ikiita tu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa alipopigiwa simu alisema kule Afrika Kusini Masogange alipatikana na hatia na kuhumumiwa, kwa hiyo hakuna sheria ya kumkamata tena hapa nchini.
“Kule alihukumiwa kwenda jela au kulipa faini, ina maana alipatikana na hatia, akalipa faini na kuachiwa,  sasa kwa nini tumkamate huku?” alihoji Nzowa.
Simu ya Masogenge juzi ilikuwa ikiita mara kadhaa bila kupokelewa.
Julai 5, mwaka jana, Masogange na Melisa Edward walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kesi yao iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo ambapo Masogange alikutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miezi 32 au faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru baada ya kuonekana hakuwa na hatia.


GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kila nchi inasheria zake,yeye alihukumiwa kwa she ria ya sauz,akamatwe awekwe ndani

    ReplyDelete
  2. hii kali yani madawa ya kulevya tanzania lkn southafrica inakuwa dawa eee, halafu mnawashika mnawaachia mnategemea nn madawa kamwe hayawezi kuisha na mateja watazidi kuongezeka, sioni sabu ya nyinyi kutangaza mtu kakamatwa then mnamuachia bora muhalalishe tu kama south africa na kuita ni dawa za kutibu binadamu na si madawa ya kulevya

    ReplyDelete
  3. wameache tu...atajuhukumu mwenyewe na kuma yake...wasimuhukumu siku zote ndo wamuhukumu leo...alafu ilo demu baya kweli kwa china mitako na miguu.shepu baya..!!!sura ndo nzuri kidogo

    ReplyDelete
  4. madawa ya kulevya yana faida zake kwa mwanadamu pia. inategemea na jinsi yalivyoandaliwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. dawa ya kulevya kuma yake huyohuyo masogange..ndo dawa.

      Delete
    2. Wewe nana huna akili hata moja umejaa ushuzi tu sijui unalalagwa saangap na unakazi

      Delete
    3. kama Coca Cola ina madawa ya kulevya vile vile, ndio maana unajisikia kuburudiiiika ukiinywa, ila imeandaliwa tofauti ukilinganisha na sembe dona.

      Delete
  5. Not fr jamani , alishaga hukumiwa alipo kamatiwa ! Huyo waziri nae anashindwa kuwakamata ma big fish tena a nawajuwa..anataka kumuonea Agnes. Au alimtongoza akamkata? Maana ndio tabia ya wakubwa wakikutaka ukiwakata wanakudidimiza!!

    ReplyDelete
  6. Jamani, just use common sense, huyu waziri, alikuwa wapi? Tangia hiyo scendo ivume? Anaibuka leo? Kuna kitu anataka sasa kanyimwa!! Nyie eleweni

    ReplyDelete
  7. we vicent hujui sheria kafie mbele. mtoto mzuri unataka akaliwe na mabwana jela

    ReplyDelete
  8. ye anadhani masogange ndo pusha, mtoto wa watu hajui hata kumeza kete.
    huyu waziri ngoja aendelee kumshika mbuzi sharubu,aone. tized kuna gun, asije akaokotwa barabarani, wakina chifupa si tumewasahau jamani?

    ReplyDelete

Top Post Ad