SETH: KANUMBA ANANITOKEA NDOTONI..MWEEEE!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Joseph Shaluwa na Erick Evarist
SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo ya kushangaza, akidai kaka yake huyo amekuwa akimtokea ndotoni.

Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa Kampuni ya Kanumba The Great Film baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 07,2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari hizi, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, kwa sauti ya huzuni, Seth alisema: “Kiukweli sina amani, hii hali inanitesa sana. Kila mara ananitokea ndotoni na kunieleza mambo yanayofanana.”

MAMBO GANI?
“Analalamika kwa nini eti ofisi yake aliyoiacha haina mafanikio. Sasa nashindwa kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia. Analalamika kwa nini filamu hazitolewi, ni jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo wangu,” alisema Seth.

AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika, nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.

AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“Mara ya tatu sasa, ndiyo maana nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza ni kwamba, kila anaponitokea, lazima nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa kasi na kutoka jasho jingi.
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia kimya, ikabidi nimwambie mama.”

MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
“Mama alishtuka na ameshangazwa sana na hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara ngapi, nikamwambia tatu, akasema lazima tufanye maombi kuondoa hali hiyo,” alisema Seth huku akionesha uso wa wasiwasi.
Credits:Global Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu kwa kutafuta umaarufu hamjambo, msenge fanya kazi mwache mchiz apumzike kw aman

    ReplyDelete
  2. haya akikutokea tena muulize alikuwa anafanyaje kuendesha hyo ofc nawe ujifunze

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kuvaa suti tu hakuna njia nyingine!!

      Delete
  3. Akikutokea tena muulize vp moto wa huko ukoje atupashe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaha u ve made ma day mdau

      Delete
    2. Daaah wadau kweli mwazimuuu..eti moto wa wpi...

      Delete
  4. Ameondoka na Usanii Wa bongo na hela zoteeeeeeeee! Akikujia tena muombe arudishe! Wasanii wamechanganyikiwa no money! Waliokuwa kwenye maself wamerudi kwenye single room!!!!!! Uwiiii""

    ReplyDelete
  5. Akikujia tena mwambie ofisi hafanyi kazi sana ngono kwa wasanii ndio inalipa.

    ReplyDelete
  6. Akikurudia tena mwambie Lulu umalaya unaendelea kuliko mwanzo na mimba yake alitoa magereza sawa.

    ReplyDelete
  7. Kwanini asikutokee wakati mnafuja mali zake ndio mambo ya mtegemea cha ndugu. Tafuta zako dogo.

    ReplyDelete
  8. Hakuna lolote. Usitudanganye.

    ReplyDelete

Top Post Ad