google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html SHILOLE AIBUKA NA ‘SERENGETI BOY’ MPYA | UDAKU SPECIAL

SHILOLE AIBUKA NA ‘SERENGETI BOY’ MPYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya

KWA mara nyingine, staa anayekimbiza kwenye filamu na muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ au ‘Shishi’ ameibuka katika penzi jipya na bwana mdogo anayechipukia katika muziki wa Bongo Fleva, Nouh Mziwanda, Risasi Mchanganyiko limeinasa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Shilole kwa sasa hasikii wala haoni kwa Nouh pamoja na kwamba wawili hao wanaonekana kuwa na tofauti kubwa ya kiumri , Shilole akionekana kuwa mkubwa zaidi ya Nouh.

“Shilole ni kama anambemenda  Nouh lakini ndiyo hivyo, haoni wala hasikii, kila siku wako pamoja kama kumbikumbi,” kilisema chanzo chetu.

Waandishi wetu waliwafuatilia wawili hao kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kuzinasa picha zao walizozipiga katika mikao ya kimahaba.
Baada ya kuzinasa picha hizo, mapaparazi wetu walimtafuta  Nouh na kumweka mtu kati kuhusu uhusiano wake na Shilole.

“Ni kweli ninatoka na Shilole ni mpenzi wangu na sidhani kama nitakuja kuachana naye maana tunapendana sana na nimevutiwa na mavituz yake,” alisema Nouh.
Kuhusu tofauti ya umri wake na ule wa Shilole, Nouh alisema umri huwa haumati katika mapenzi.

“Mapenzi ni mapenzi na umri utabaki kuwa namba tu, ni vyema  mtu ukaongozwa na hisia zako kuliko kuhofia umri wa mtu ndiyo maana miye ninakula vinono,” alisisitiza.
Pia, Nouh alisema hakutarajia kukubaliwa na  Shilole baada ya kumtokea walipokutana  katika  studio moja jijni Dar na sasa wamekolea kwenye penzi motomoto.

“Nampenda Shishi, nafanya kila njia nimshawishi awe mke wangu wa ndoa,” aliongeza. 
Hata hivyo, Shilole alipozungumza na waandishi wetu alipatwa na  kigugumizi kukubali uhusiano wake wa kimapenzi na kinda huyo wa Bongo Fleva.

Shilole alisema Nouh ni rafiki yake kama walivyo marafiki zake wengine.
Waandishi wetu walipomuonesha picha zao walizokuwa wamekaa katika mikao ya  kihasarahasara, Shilole aliangua kicheko na kisha akasema:

“Mh! Sina la kuwajibu kama picha zinasema mimi na Nouh ni wapenzi haya.”  
Hii siyo mara ya kwanza kwa Shilole kuripotiwa kutoka na Serengeti Boy, siku za nyuma alishawahi kuripotiwa na gazeti dada na hili la Ijumaa Wikienda akisema anapenda kutoka na ‘Serengeti Boys’.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo mvulana nzuri..lol,wamependeza sana..umri si kitu .

    ReplyDelete
  2. miguu imebabuka kwa krimu loh!utadhan mguu wa mzee
    punguza kujikoboa unataka hadi mishipa ya kijan ionekaneeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Kama ni wapenzi shida yenu nini?mbona kawaida sana

    ReplyDelete

Top Post Ad