google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html SUMAYE AKATA RUFAA KWA KUZUIWA KUFANYA KAMPENI ZA URAIS | UDAKU SPECIAL

SUMAYE AKATA RUFAA KWA KUZUIWA KUFANYA KAMPENI ZA URAIS

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amekata rufaa Kamati Kuu ya CCM kupinga adhabu ya onyo kali aliyopewa na chama kutokana na madai ya kuanza kampeni za urais mapema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza na gazeti hili mjini Dodoma jana, Sumaye alisema kwa ufupi hakuridhishwa na adhabu hiyo na kuthibitisha hilo, tayari amekata rufaa.

Hata hivyo, alisema hadi jana hakuwa amepata mrejesho wowote kwa sababu kanuni hazielezi ni muda gani anatakiwa kuwa amepewa taarifa kuhusu rufaa hiyo.

Sumaye na wanachama wenzake, Edward Lowassa, Bernard Membe, Stephen Wassira, William Ngeleja na January Makamba walitiwa hatiani kwa kuanza kampeni mapema, hivyo kupewa onyo linalokwenda sambamba na kutowania nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 12.

“Siwezi kuwazungumzia wenzangu, nazungumza kwa upande wangu, sikuridhishwa na adhabu hii na nimeshakata rufaa ingawa sijapata majibu yoyote, naendelea kusubiri,” alieleza Sumaye.

Waziri Sumaye alikataa kuzungumzia hali ya utekelezaji wa adhabu hiyo, akisema anachosubiri ni mwitiko wa rufaa yake aliyoiwasilisha Kamati Kuu ya CCM, mwanzoni mwa mwezi huu. “Sina kumbukumbu nzuri ilikuwa tarehe ngapi, lakini ni mwezi huu wa tatu.”

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa juu ya rufaa hiyo alisema hana taarifa zaidi ya habari hizo kuzisikia kutoka kwa mwandishi.

Hata alipotakiwa kueleza nani anatakiwa kuwa na taarifa hizo, alisema: “Mimi ndiye msemaji wa chama, hakuna wa kuzungumzia suala hili zaidi yangu. Kwanza inatakiwa ijulikane, rufaa hiyo imepelekwa ngazi gani ya uongozi kwa sababu kila ngazi ina muda tofauti wa kufanya vikao vyake vya uamuzi.”

Nnauye baada ya kuelezwa kuwa rufaa ya Sumaye imewasilishwa Kamati Kuu ya CCM, alisisitiza kuwa hana taarifa nayo na kwamba haiwezekani rufaa ipelekwe kwenye kikao kilichotoa adhabu husika.

Hata hivyo, Sumaye alisisitiza kuwa rufaa yake ameiwasilisha Kamati Kuu kwa mujibu wa kanuni zinazohusika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. unapoteza muda wako bure wala urais hupati hizo hela ulizonazo bora ukawape watoto yatima ili mungu akupunguzie madhambi ulionayo shwain wewe

    ReplyDelete
  2. wapenda matusi utawaona tu!!!! sasa hapo umetukana kwani kakosa nini? hiyo ni haki yake ya msingi kama hakulidhishwa na adhabu aliyopewa.

    ReplyDelete
  3. Hawataki lowadsa awe na mpinzani,mi lowadsa simpendiiiii mbinafsiiiiiiiii,kula na ukoo na familia yake tuuuuuuuuu,

    ReplyDelete
  4. Kati ya vijana ambao siwapendi NAPE unaongoza yaani we msenge unajifanya unajua sana kila kitu, elimu yenyewe mbovu, we mtoto kima sana

    ReplyDelete
  5. Hivi nyie ccm mnadhani kuendelea kuwa mabilioney ndo kuishi vizur hapa dunian, woote mliotajwa hapo juu kwa ufisadi mliofanya ndan ya nchi hii unatosha na utajir mlionao unawatosha kabisa kuendelea kula na watoto wenu hadi na vitukuu vyenu mpaka mnakufa na bila kufilisika, kueni na huruma jamani ebo, pia kumbukeni kuna kifo na sjuwi mtajibu nn maskin

    ReplyDelete
  6. Kura yangu nampa makufuli wengine mafisad

    ReplyDelete
  7. Kabisaaa lowasa umekula vya kutosha jamaniiiiiiiii Si uwaachie na wengineeeeeeeeeeee,?ubinsfsi unakusumbua.Mungu wangu sikiliza sala zangu usimpe uraisi huyu mtu pleaseeee,ameshakomba alivyokuwa waziri mkuu yatoshaaaa

    ReplyDelete
  8. Bora tu awe huyu raisi kuliko lowasa jaman

    ReplyDelete

Top Post Ad