TANZANIA INAWEZA KUZIPIKU NA KUONGOZA KIUCHUMI KATIKA NJE ZA AFRICA MASHARIKI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Licha ya nchi hizo kuwa chini ya mtawala mmoja wa kikoloni (mbali na Rwanda na Burundi), bado inaelezwa kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kuendelea kiuchumi kuliko wanachama wengine wa Afrika Mashariki.
Akizungumza katika mjadala wa bajeti za Afrika Mashariki ulioandaliwa na taasisi ya utafiti wa jamii na uchumi (ESRF) juzi jijini Dar es Salaam, mwakilishi kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdulla Makame anasema Tanzania ina kila sababu ya kuendelea kupitia ushirikiano huo.

“Tunazo fursa nyingi tu za kuendelea; tunayo ardhi kubwa na yenye rutuba, tunazo rasilimali ingawa kwa sasa kuna janga la ujangili wa meno ya tembo. Tuko pia kwenye eneo zuri la kijiografia.

“Tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Msumbiji. Hakuna nchi nyingine ya Afrika Mashariki inayopakana na nchi wanachama wote kwa wakati mmoja,” Dk Abdulla.

Bajeti Jumuiya ya Afika Mashariki

Pamoja na kuwapo kwa fursa hiyo anasema bado bajeti ya Serikali hailingani na matakwa ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Bajeti ya Taifa hailingani na malengo na mipango ya maendeleo ya Afrika Mashariki. Tungetarajia kuwa bajeti za maendeleo ya jumuiya ziwekwe moja kwa moja kwenye wizara husika,” anasema Dk Makame.

Anashauri waandaaji wa bajeti kuangalia vipaumbele vya jumuiya hiyo na kukamilisha sera yake.

“Tunayo Reli ya Kati iliyojengwa na Wajerumani wakati wa ukoloni. Ilitakiwa reli hii itumike kuleta maendeleo ya uchumi kwa Tanzania, lakini bado haina viwango vya kimataifa,” anasema Dk Abdulla.

Akijibu hoja hizo, Kamishna Msaidizi wa bajeti kutoka Wizara ya Fedha, Emmanuel Tutuba anasema tayari bajeti ya Serikali imeanza kutekeleza mahitaji ya jumuiya hiyo.

“Nikiangalia kwenye bajeti yetu naona kuna mambo mengi yameanza kutekelezwa na mengine yako ngazi ya kimataifa. Kwa mfano, sekta ya umeme, ukiangalia takwimu na uwekezaji wa Serikali utaona lengo ni kuuza umeme kwa nchi za Afrika Mashariki. Maendeleo ni mazuri hasa kwa umeme wa gesi kutoka Mtwara. “Hata ukiangalia upande wa kilimo, wenzetu wa NRFA walinunua mahindi mengi na kuyauza nchini Kenya, wanategemea kupata Sh8 bilioni.

“Hata ukiangalia viwanja vya ndege kwa mfano, wa Kigoma, umejengwa mahsusi kwa ajili ya kuunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda na Burundi. Kwa hiyo tayari kuna utekelezaji wa bajeti kwa maendeleo ya Afrika Mashariki.”

Biashara imeongezeka zaidi

aye Ofisa wa Shirikisho la Chama cha Wafanyakazi, Kilimo na wenye Viwanda (TCCIA), Adam Zuku anasema: “Tangu tumejiunga, ukubwa wa biashara umeongezeka tofauti na zamani, haijaridhisha, lakini inakwenda vizuri.

“Tunapozungumzia mtangamano huu wa sasa ni tofauti na wa zamani.

Mtangamano wa sasa ni wananchi zaidi kuliko zamani ambapo ilikuwa kwa viongozi pekee. Siku hizi mambo yanafanywa na wataalamu,” anasema. Anatoa mfano wa ukuaji wa biashara akisema hata mashirika ya viwango ya jumuiya hiyo sasa yanatambuana na kutoa maagizo yanayofanana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama usimamizi wa rasilimali na mgawanyo wenye uwiano kwa wananchi wote,bado hizo hoja zitabaki kuwa siasa tu tena siasa chafu ambazo baadaye zitatufikisha ambapo congo drc,Afrika ya kati na nk zilipo.TUACHE SIASA TUWE WATU WA VITENDO!

    ReplyDelete
  2. Hilo linajulikana lakini kama wananchi wataendelea kupumbazwa na vitu vidogo vidogo kama kampeni za kupewa vijizawadi uchwara (fulana) na hotuba za kuwalainisha mpaka kuwachagua viongozi wasiowajali wananchi wao kwa kujilimbikizia utajiri kutokana na maliasili ya nchi, basi nchi haitaenda popote na tutakuwa vituko vya majirani.

    ReplyDelete

Top Post Ad