ULEVI WA SHISHA WASHIKA KASI BONGO..WAGUNDULIKA UNA MADHARA MAKUBWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Umeibuka ulevi mpya nchini ambao umethibitika kuwateka vijana hasa wa jiji la Dar es Salaam, huku kukiwa na taarifa za kitaalamu kwamba ulevi huo una athari za kiafya kwa watumiaji.

Ulevi huo ni kupitia starehe au anasa mpya ya uvutaji shisha; ulevi ambao watengenezaji hutumia chombo maalumu chenye bomba la kutolea moshi, ambacho huwekwa tumbaku, maji na moto.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa tumbaku huwekwa katika chombo hicho na kuunguzwa kwa moto, kisha moshi wa tumbaku hupita kwenye maji na huingia kwenye bomba, kisha watumiaji huanza kuvuta.

Sehemu maarufu ambako shisha inauzwa ni Ufukwe wa Coco, maeneo ya Kinondoni, Mwananyamala, Sinza Barabara ya Shekilango na maeneo kadhaa ya mitaa ya mjini.

Mmoja wa watumiaji wa shisha, Ismail Ndunguru alisema yeye na vijana wenzake hutumia siku za mwisho wa wiki kwenda kuburudika kwa uvutaji katika hoteli moja iliyopo mjini, Mtaa wa Garden jijini Dar es Salaam.

“Kuvuta shisha kwa siku nzima ni Shilingi 10,000, mkimaliza, mnarudisha bomba. Tukiwa vijana wengi inafurahisha sana kuvuta,” alisema Ndunguru.

Taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa, mkupuo mmoja wa shisha, una kemikali hai 4,800 na kwamba kemikali hizo husababisha saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa upumuaji.

WHO inaeleza kuwa, kiasi cha uvutaji wa shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara 100 au 200.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani ya mwili na mfumo wa hewa, Meshack Shimwela alisema madhara ya shisha ni kama yale yanayosababishwa na uvutaji wa sigara pengine na zaidi kutokana na kilevi hicho kuwa na tumbaku nyingi.

Dk Shimwela alisema licha ya kuwa watengenezaji na wavutaji wa shisha hudai kuwa haina madhara kwa sababu huchanganywa na maji, lakini bado madhara yake ni makubwa.

“Maradhi yote yanayosababishwa na uvutaji wa sigara ndiyo yanayosababishwa na shisha, kwa mfano saratani ya mapafu na mdomo, kifua kikuu na mzio ambao unaweza kusababisha pumu,” alisema Dk. Shimwela.

Dk. Shimwela alisema ni vizuri watumiaji wakajua madhara ya shisha, badala ya kuchukulia kuwa ni mtindo wa maisha tu au starehe isiyo na madhara.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ASIKWAMBIE MTU SHISHA INA RAHA YAKE

    ReplyDelete
  2. endeleen kuozesha mapafu kwa raha zenu izo

    ReplyDelete
  3. Kazi kwenu wala tumbaku eti mnaita shisha

    ReplyDelete
  4. tunapenda kuiga vitu tunaviona kupitia video,tukijua n ujanja kumbe ushamba

    ReplyDelete
  5. Mtajijua wenyewe.shisha's members oyeeeeee

    ReplyDelete
  6. ushuzi mtupu. watu wanaiga vitu ambavyo hawajui madhara yake wao wanadhani ni ufahari na ujanja. baada ya miaka kaadha ndo watakuja kuona madhara yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kila kitu kina madhara acha watu wafurahi....hata domo lako unavyoongea usenge pia ni madhara...madhara gani unayo yajua we nyamafu

      Delete
  7. Nyambav wew msenge

    ReplyDelete
  8. Shisha's oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!

    ReplyDelete
  9. Na mtatoboka sana mapafu nya'ngau wakubwa nyie!

    ReplyDelete
  10. Hasa bongo mnaambukizana TB tu!

    ReplyDelete
  11. KUMAMAKEEEEE.......SHISHAAA MPANGO MZIMA WASHAMBA NYIEEE MSIOJUAAAA PUMBAVUU!!!!!! SHISHA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEHHHH

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna alie kukataza kuvuta ndugu yangu kejeli ya nini!?

      Delete
  12. Badala ya 2mbaku naweka bangi ucpime!!

    ReplyDelete
  13. Kaz kwelikweli uyu mvutaji kama yupo arusha vile

    ReplyDelete
  14. We usipime shisha ukiweka bangi unapata handasi balaa nakumbuka maisha club mara ya kwanza kuvuta nlikunya ila ukizoea rahaaaa,tukutane coco beach.

    ReplyDelete

Top Post Ad