WADAU KUWENI MAKINI..... HEBU SOMA HII STORY

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WADAU KUWENI MAKINI..... HEBU SOMA HII STORY
Nimetapeliwa Sinza
Ndugu zangu nisaidieni kama naweza kuwapata walionitapel na warejeshe malipo niliyoyatoa.

Siku moja nilienda Sinza kwa Remy nikitafuta nyumba!Nilionyeshwa dalali na nikazunguka naye,nyumba alizonionyesha sikuridhika nazo!Baada ya cku 2 nikapigiwa simu na akasema umepata nyumba?Nilimjibu bado then kanambia njoo kwa Remi kuna nyumba!Ndugu zangu nilitoka Posta Haraka,nilipofika Kwa remi nilimpigia simu akanambia kuwa yeye ameenda kumuonyesha MTU shamba lkn ana kijana wake anaitwa Fred,after 6mins alikuja kijana akatupeleka kuangalia nyumba.Niliona nyumba nikamuuliza mwenye nyumba yupo wapi?Akasema Makongo!Kesho yake huyu Fred(0656389300) akatupeleka makongo kwa Mwenye nyumba tukalipa.

Siku ilifika ya kuhamia kabla ya kuhama tuliwasiliana na yule mwenye nyumba hapatikan kwa simu.Kumbe tumelipa kwa MTU fake.Nilifungua RB na nilienda na police wawili pale nilipolipia geti halikufunguliwa!Siku nyingine niliwachukua ten a police wa upelelezi tukavizia mvua inanyesha tukapiga hon getin geti likafunguliwa na Kijana akatukaribisha sebulen,wale polisi wakiwa na nguo za kiraia walimuuliza yule kijana mzee yupo akasema yupo wakamwambia sisi nin wagen wake.Ile nyumba INA kigorofa na yule kijana alipanda juu dk5 akashuka akasema kwan hamkuwasiliana na Mzee kwa simu?

Mzee hayupo yupo Zanzibar na anakuja Leo jion,.Police walimwabia yule kijana Tupe namba zake yule kijana akatoa namba na polisi alipiga ile no. Jamaa akapokea akasema hayupo Zanzibar na anafanya kazi bank na hataki usumbufu kama police WAPO kwenye nyumba yake basi waichukue au waichome moto,Ila huyu jamaa naamin alikuwa ndan nikawambia polisi wakasema hawana search warrant.Tukarudi.

NDUGU ZANGU NAWAOMBENI MAWAZO YENU AU USHAURI ili tuwakamate hawa matapeli waweze kurudisha hizi hela kwan nilikopa ndugu zangu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole madalali wa sinza Ndio zao

    ReplyDelete
  2. Kwanza pole ulikubali vipi kuandikiana mbali musengeandikiana hapo sinza? Hawa kuwapata wapigie tena madalali kwa namba nyengine na maongezi mengine ilikumainisha kama unataka kiwanja au nyumba ya kununua.

    ReplyDelete
  3. Da pole ila uo ni uzembe ata mm nilitakaga kutapeliwa nilikuwa natafuta nyumba na madalali wa kino nami nikapigiwa kama nmepata nkasema bado uyo dalali aliyepiga sikumjua ila alisema no yangu kapewa na dalali wangu akamtaja ambae mm namjua tukaenda adi sinza ilikuwa maeneo hayo hayo kwa remmy akatuonesha nyumba ya kwanza na yapili lkn zote kwa nje tulishangaa kwann atuingii ndani akasema jtatu wenyenyumba wako job ya mwisho tulipenda lkn nayo atukuingia ndani akampigia mwenyenyumba akasema yuko kwa mke mdogo kimara akamuliza nani yupo akasema amna mtu ndani mkewake mkubwa kasafir akataka tukalipe mbezi cha ajabu nyumba nzur sana lkn bei rahis tukastuka tukamwambia tutakuja kesho ili tuone ndani natutakuja na dalali wangu alompa no tukampa cha mguu akaenda kesho yake nikampigia dalaliwangu wa mwanzo akasema akumpa mtu no sasa tukamtumia msg yule kaka kwamba unataka kututapeli akujibu badalayake alipokea mwanamke akatuliza sisi nani ye ndo mwenye simu tuliwatukana sana kwa utapeli tumepoteza helaza kuzunguka na bajaji na ya usumbufu kulipa tulipombana sana dalali wangu ilionekana kama walishirikians kwasababu yeye alisema huyo atakuwa msafir tape sana kaiba namba ataiba namba za watejawangapi.. sasa ndugu yangu usione nmeandika mgazeti ukisomA vzur utajua unanzia wp mtafute dalaliwako wa mwanzo au mtu aliyekunganisha nao then mpeleke police akila kibano atawataja wenzie maranying wanashirikiana na huyo dalali atakuwa mweupe a.ajichubua kama shoga hv wafatilie hela yako utaipata au nenda pele kwa madalali wa kwa remmy wape kitukidogo watakutajia wanajuana madalaliwananjaa alitapeliwa mwanajeshi alitembeza kichapo madalali walitajana kwahyo fanya hivyo samahani kwakundika makala ndefu nikwajili ya kukupa mwangaza

    ReplyDelete
    Replies
    1. COMMENT KAMA HIZI NDIO ZINAZOHITAJIKA HUMU,SIO MITUSI KILA KUKICHA

      Delete
    2. Kwel kabsa Hugo mshaur anabusara sana

      Delete
  4. Mmmh nimeguswaaaa.. mmmh wabongo noma Naomi pia ilishawahi nitokea kinondoni posit na duka LA Manywele Cosmetics.Yani Kali kuliko zote yule mwenye nyumba ndo alitaka kutupapeli kz alitufungulia mpaka chumba anacholala na mkewe eti wangehama baada ya wiki Moja.Tukalipa looh wiki 2 baadae anatuzingusha mwsh was siku jirani pale wakadai ni kawaida yake kufanya utapeli wa aina by pesa anazingsh kwny biashr zakeu so ukimdai anapigwa mwngne ankrdshia we..MMMH DAR MJI WA MAJANGA SANA..BORA KUPATA USHAHIDI KW JIRANI KABLA YA MALIPO

    ReplyDelete
  5. Pole. Mkamate dalali wako atakutajia mwiz

    ReplyDelete
  6. Pole. Mkamate dalali wako yeye atakutajia mwizi wako.

    ReplyDelete
  7. Tafuta tingatinga na kaibomoe,ukishidwa basi waombe wale wenzetu wa arusha wakusaidie kuandama.

    ReplyDelete
  8. Acha ufala bwana ccm juu!Umeambiwa kwamba uyo dalali niwa arusha fyuuuu 8

    ReplyDelete
  9. kwa mujibu wa stori,tapeli wako anaitwa Moshi Majungu,anaishi Makongo Juu,ni kawaida yake kufanya hivyo, na akikamatwa anatoka baada ya siku tatu au mbili.anatumia gari aina ya pajero short chasis.andika email yako au tafuta njia ya siri ya mawasiliano nikusaidie jinsi ya kumkamata

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi nakuomba ucreate hata email account mpya kwa ajili hii ili uiweke hapa umsaidie huyu aliyetapeliwa au akupe namba yake ya simu.

      Delete
    2. AHSANTEN SANA; Email yangu ni (4noeldaniel@gmail.com)

      Ndugu uliyeandika March 7,2014 at 11:34 AM-tukiwa kwenye ile nyumba kijana wa kazi aliulizwa na police mzee yupo wapi na anaitwa nani? Alisema na kutaja kwa jina moja kuwa anaitwa Moshi.

      Delete
  10. Pole sana ndugu, huo utapeli wa hivyo madalali wanaufanya sana. Kinondoni kuna jamaa mmoja anajulikana kwa jina la Apolito, ana vijumba vizuri sana na bei ni ya kawaida ukionyeshwa hizo nyumba huchomoki lazima utajikuta unalipia. Jamani kuweni makini huyo jamaa pamoja na Dalali yoyote atakaye kupeleka hapo kwenye hizo nyumba ni matapeli Sababu hazipangishwi.

    ReplyDelete
  11. Ushaur, rudi police wakukamatie huyo mwenye hiyo nyumba kwan atakuwa anajua nchezo mzima na nani alikuwa kwake siku hiyo asikutishe anafanya kazi benki we wape polic kitu kidogo utapata matapeli wako. Pole sana.

    ReplyDelete
  12. pole sna ndugu

    ReplyDelete
  13. Mimi nilitapeliwa pia ila hivi sasa ninavoandika dalali ananyea kidebe sikukubali aisee

    ReplyDelete
  14. ndugu zake wamesema tukutane leo polisi ili wanilipe mshiko wangu tufute kesi

    ReplyDelete
  15. Usisahau kumbandika Na gharama za usumbufu ..usimlegezee

    ReplyDelete
  16. pole sana,nakuwa offline kwa muda.mimi ndio niliyekutajia jamaa huyo,ingia kwenye email yako angalia maelekezo

    ReplyDelete
  17. Daaa yani huo mchezo upo sana ukipata nyumba lakini ukaambiwa mwenye nyumba anakaa maeneo ya survey malimani city au makongo na anataka ukalipie nyumbani kwake juwa ni tapeli..!

    ReplyDelete

Top Post Ad