WAPINZANI WAPINGA HOTUBA YA JK BUNGE LA KATIBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wenyeviti wa vyama vya Upinzani vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR-Mageuzi, jana usiku walikutana ili kutoa kauli ya pamoja, kutokana na hotuba ya ufunguzi wa Bunge kwa maelezo kuwa tayari Rais amevuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Wakati viongozi hao wakikutana, Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji, Christopher Mtikila alisema, Rais ameingilia mchakato na kutoa maelezo jinsi ya  kuandika Katiba.

Wakizungumza na gazeti hili jana mara baada ya hotuba hiyo, Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Ibrahim Lipumba, walisema wameipokea kwa masikitiko makubwa hotuba hiyo.

“Tunakwenda kujadili hotuba ya Rais na tutatoa msimamo wetu,” alisema Mbowe.

Awali Katibu wa muda wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Julius Mtatiro alisema Rais Jakaya Kikwete amevuruga mchakato wa Katiba, kwani walitarajia angetumia mamlaka yake kama Rais kuwaunganisha.

“Rais tulitarajia angeongea kama mkuu wa nchi, lakini amezungumza kama Mwenyekiti wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo wa Muungano jambo ambalo hatukulitegemea,” alisema Mtatiro.

Alisema kwa Rais kutoa msimamo ni sawa na mwongozo jambo ambalo limevuruga mchakato mzima.

Hofu ya kuvunjika Bunge

Wakizungumza nje ya Bunge, baadhi ya wajumbe wameeleza kuwa hotuba ya Rais Kikwete kama ikitekelezwa uwezekano wa kupata Katiba Mpya utakuwa mgumu.

Mjumbe Luhaga Mpina alisema kwa jinsi rasimu ilivyoandikiwa na kama muundo wa serikali mbili ukipita basi rasimu ya Katiba itabidi iandikwe upya.

“Rasimu yote imetengenezwa kwa mfumo wa serikali tatu sasa hapa kuna hatari ya Bunge kukwama ,” alisema.

Mtatiro kwa upande wake alisema sasa kuna hofu ya kushindwa kupatikana Katiba Mpya kwani Rais amewachanganya wajumbe na kama watapitisha maoni yake itabidi rasimu kuandikwa upya.

Mjumbe Mustapha Akoonay, alisema upatikanaji wa katiba upo shakani kwani sasa upinzani utakuwa mkubwa juu ya muundo wa muungano.

“Kwa sasa nadhani itabidi turudi upya kwa wananchi kupata kura ya maoni juu ya muundo wa muungano,” alisema.

Lucy Owenya alisema  Rais amegeuza mkutano wa Bunge kuwa ni mkutano wa Chama Cha Mapinduzi, kwani ameshindwa kabisa kutoa mwelekeo wa nchi na badala yake ametoa msimamo wa CCM.

“Kutokana na hili, naamini kabisa Bunge halitakuwapo na ni bora iwe hivyo kwa kuwa amejibu hotuba ya Warioba na kwa maana hiyo amepingana na mawazo ya wananchi.”

Godbles Lema alisema kuwa Rais hakuja kuhutubia taifa bali alikuja kufanya semina na kujibu hotuba ya Warioba.

Mjumbe huyo ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini alionyesha shaka kuwa baada ya muda wa wiki tatu hakutakuwa na Bunge la Katiba kwa kuwa wako baadhi ya watu ambao hawatakubali kilichofanywa na Rais Kikwete.

“Waliochukua fedha ni vyema wakaenda kumalizia nyumba zao kwa kuwa kiongozi wetu amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafurahisha wanaCCM lakini kwa Watanzania hatutakubali,” alisema Lema.

John Cheyo alisema, “Mimi ninachokiona ni maridhiano tu, suala la kufumua rasimu halinipi shida kwa kuwa vitu vyote vinavyoletwa bungeni huwa ni mali ya Bunge na hivyo tutafanya tunavyoona sisi inafaa.”

Mchungaji Peter Msigwa, alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na upinzani ni kukubali na kuruhusu Jaji Warioba atangulie kuwasilisha rasimu yake akasema hilo ndilo lililowagharimu.

Alitaka Bunge livunjwe mara moja ili warudi kwa wananchi wakaamue na kuwahukumu kutokana na kile ambacho walikifanya katika Bunge ambalo kwa maoni yake wamekula fedha za walipa kodi bure.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa aliipongeza hutuba ya Rais Jakaya Kikwete ya uzinduzi wa Bunge la Katiba.

Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, alisema kwa kifupi hotuba ya Rais Kikwete ni nzuri. Lowassa alitoa kauli hiyo, wakati akitoka nje ya Bunge, muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge hilo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Katiba ilisha andikwa na ccm, wanatuzugatu hawa

    ReplyDelete
  2. Wapinzani tumeshawazoea. Wao husikiliza mambo ili wabishane na si kuelewa. Uwezo wao wa kufikiri ni finyu sana. Ni sawa na mbwa anayebweka kila amuonapo mtu kumbe wengine ndo wale walomfuga. Pengine angeelewa asingebweka. Si lazima utoe tamko ndo tukufahamu kuwa wewe ni mpinzani. Rais alisema wenye maamuzi ya mwisho ni wajumbe pekee ila yeye alitoa angalizo na changamoto tena kwa mifano. Ni rahisi sana aisee wala huitaji kuwa na Phd kuelewa hilo. Wapinzani na wajumbe ndo wapo bungeni kutengeneza katiba, wakichemka ni wao. Tutawalaumu. Kama wanaona hawawezi kazi waseme ili wateuliwe wengine kazi iendelee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAWANA jema kila siku ni kupinga yeye kasema kaawachia wao kutunga katiba but wawe makini kama ni serikali tatu basi wawe na tija katika serikali tatu na kama mbili basi waiboreshe mlitaka asemeje, mtajibeba mmezoea kutafuniwa nyie mmeze tengenezeni katiba sasa sio kuropoka ropoka tu hovo mnafikiri mmekwenda bungeni kutembea shwain nyie

      Delete
  3. Hasa huyo lema na mbowe wake ni wapuuzi sana,yani siipendi chadema mm kwaajili ya huo usenge wao,wangesimama wao wangehutubia nn? Lema fani yake tunaijua hana lolote�� rais kahutubia kitu cha maana sana,CCM oyeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  4. Umeshawaita 'wapinzani', unategemea nini hapo?? Ni kupinga tu kwa kwenda mbele. Kawaida yao kupinga kila kitu, JK katoa mawazo yake kama raia wa TZ na akasema wazi maamuzi yapo kwenu nyinyi wajumbe, msipoteze malengo, ukweli mnaujua lakini mnaupotezea, hovyooooooooooo!!! Wake wawili wamekushinda wakiwa watatu ndio utawamudu....... KAMA KAWAIDA YENU WAPINZANI, HEBU SUSIENI NA HILI, TUJIPANGIE MAMBO YETU KIULAIIIINIII!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kuna watu hawafikili kabisa JK alichotakiwa pale ni kuhutubia bunge na sio kunadi sela za msimamo wa chama chake na kusema serikali tatu ni majanga na kuanza kuponda kama rais hakupaswa kufanya ailipaswa asifungamane na uponde wote lakin alichofanya ni aibu tupu kuipinga tume ambayo umeiunda mwenyewe ni aibu alichofanya pale ni kuwahutubia ccm na si wananch ila naamin hz fikra za kidumu fikra za mwenyekit zitafika mwisho na Tanganyika yetu tutaipata

      Delete
  5. Lowasa we msenge sana unasaport anachosema mshua kwakuwa wote nyie ndo mnaosaini mikataba hewa, na kutuingiza kwenye hali ngumu ya kiuchumi, alafu bado unataka kugombea urais ili muendelee kutuumiza, muogope mungu we mzee, umekula vya kutosha sanaaaa

    ReplyDelete
  6. Mimi sio mwana ccm hata chembe but alichoongea mkuu wa kaya jana simple n clear ,yy ametoa maoni yake kwa jinsi aonavyo yy baada ya kuipitia rasimu mara kadhaa na kugundua mapungufu na ndo maana akawa anasisitiza kuwa wajumbe wao ndio waamuzi wa mwisho, thn rais kuunda tume ya katiba chini ya jaji warioba sio kwamba asiweze kuikosoa hyo ni tume imeundwa na wanadamu km wanadamu wengine so km wamekosea shm wacha mkuu wa kaya akosoe kwa kupitia maoni yake...big up mkuu wa kaya kazi ipo kwao wajumbe maalum wa bunge la katiba

    ReplyDelete
  7. warioba alianza kulivuruga bunge na kujifanya alichoandika yeye ndio hicho hicho na yeye ndo anojua kuliko wote kwa hiyo kakosolewa ndo mmenuna hivi mlitaka iweje? yaani kutengeneza Tanzania hewa ndio mnavyotaka, hongera kikwete kwa kuonyesha msimamo wa kutouvunja muungano. kwa hiyo tumeona hata hizo serikali tatu za warioba zina changamoto kabla hata hazijaanza.

    ReplyDelete
  8. Watu mnavichwa vigumu kama mawe rais hajatoa msimamo wa chama alikua anatoa maoni yake na kuwaelewesha wajumbe waelewe kitu ambacho watakipitisha kina changamoto gani mfano hyo serikali ya tatu ambayo itabeba wizara za muungano kama mambo ya ndani na ulinzi huku haina chanzo cha mapato hela ya bajeti inategemea kutoka tanganyika na zanzibar je hzo nchi zikisema hazima hela au zikichelewa kupeleka hela hyo serikali itawezaje kuzihudumia hzo wizara zake ambazo ni nyeti watu inabidi wawe wanafikiria na sio kufata mkumbo tu

    ReplyDelete
  9. Raisi wenu naye fala tu tena boya wa mwisho ndo maana alitakiwa kuzungumza kabla ya warioba na si baada!!! kazi yake kucheka cheka tu...aaaaah nimesahau kumbe ni mtoto wa pwani ile.

    ReplyDelete

Top Post Ad