ZIFAHAMU FAIDA 5 ZA KUNUNIANA NA MPENZI WAKO NDANI YA MAHUSIANO YAWE YA NDANI YA NDOA AMA UCHUMBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mapenzi yana wigo mpana mno ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili pembuzi kabla ya kuingia, namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina cha maji kabla ya kuzamia. Sasa basi, zifuatazo ni faida tano utakazozipata ukiwa umenuniana na mpenzi wako. 

HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO
Ni ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu fulani katika jamii unayoishi ni vigumu sana kujikuta umekwaruzana naye. Hii ni kwasababu utakuwa hauingiliani naye katika mizunguko yako, vivyo hivyo kwa wapenzi walionuniana. 

Hali hii hupunguza kabisa migogoro ya hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo ambalo huepusha maudhi ya kibinadamu. 

Mfano, yawezakana katika kipindi mlichonuniana na mpenzi wako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama ungelikuwa naye karibu. 

Kwa hiyo kuna baadhi ya maumivu na maudhi ambayo utaepukana nayo kwa kipindi cha kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba hupunguza migogoro na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi msomaji wangu? Haya twende kwenye faida ya pili. 

KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO
Hiki ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu hana ‘time’ na mwenzake. 

Kama kuna asili ya maisha yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na wewe, ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa kujiona kuwa hana mtu wa kumzuia na kumbana. 

Kama ni mlevi kupindukia, mchafu, muongo na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha katika kipindi ambacho mmenuniana. 

KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
Hapa naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazuri na mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari penzi lenu kwa ujumla. 

Ni kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa ni aina gani ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu, lakini pia katika kutafuta suluhu hiyo utapata fursa ya kutafakari kwa kina juu ya penzi lenu huku ukimpima mwezi wako kwa mtazamo chanya. 

KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
Si kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zake kuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata penzi lako. 

Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako. 

Hii si kwa msichana tu, hata kwa wanamume kwani huenda kati ya rafiki wa ‘girlfriend’ wako, kuna wanaokutamani, sasa wakiona huna uhusiano mzuri na mpenzi wako, watatumia nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu yake na kukuonesha kila dalili za kukutaka.

Hivyo utakuwa umefahamu ni aina gani ya rafiki ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba, marafiki wengi wana tabia zinazofanana. 

KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisia za dhati kabisa kwako, katika kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu. 

Pamoja na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha kukujali kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale yaani ilimradi tu asikie angalau sauti yako, lengo lake likiwa ni kutaka kurejesha ukaribu ambao sasa anaona kama akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake. 

Kwa mantiki hiyo basi, utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na ni aina gani ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika kuyajua kupitia kipindi cha kununiana kwenu. 

Hata hivyo, niwatahadharishe kwamba, kuandika haya isiwe ni tiketi ya wewe sasa kuanza kununiana na mpenzi wako eti kwa kigezo kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la hasha!
Siku zote katika uhusiano wako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa ya lazima.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huo no ukweli usiofichika wapendwa

    ReplyDelete
  2. Hivi wadau ni kweli kuwa pilipi inaweza kukuza uume?, emb naomben kila mmjo aweze kuingia google na kusearch wavuti inayoitwa swahilitz.info
    Alaf aweze kucoment pale kama ni kweli pilipili ndio dawa. Maana nina datito kama hilo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi wadau ni kweli kuwa pilipili inaweza kukuza uume? emb naombeni kila mmoja wenu aweze kuingia google na kusearch Swahilitz.info
      Na kusoma makalala iliyoandikwa kwamba pilipili ni mkombozi kwa wanaume. Kama itakuwa kweli basi soma na coment. Maana nina tatizo kama hilo.

      Delete
  3. Dah true say Admin....l ms you my lbraheem.....kissez

    ReplyDelete
  4. Changia mada habali za pilipili uko uko shenz

    ReplyDelete

Top Post Ad