JERR SILAA" YANGA HAKUNA KUJENGA UWANJA JAGWANI ..PALE NI MKONDO WA MAJI"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa amepigilia msumari wa mwisho kwa kuwataka Yanga kusahau kuhusu ongezeko la eneo la kujenga uwanja wake eneo la Jangwani kwa vile sehemu hiyo ni mkondo wa maji.

Akizungumza na gazeti hili, Dar es Salaam jana, Silaa alisema:

“Tumepata hasara kubwa (Serikali) hii yote imetokana na watu kujimegea maeneo na kujenga kwenye mkondo wa maji, mafuriko yote haya yanayotokea ni kwa vile maji yanakosa pa kwenda na kuishia kwenye maeneo mengine ndiyo maafa yote haya yanatokea.

“Hebu angalieni pale Jangwani sasa hivi kulivyo, maji yamefurika watu wengine wamepoteza maisha, halafu bado turuhusu watu waendelee kujenga kwenye mkondo wa bahari, waambieni wasahau hilo.”

Kauli hiyo ya Meya Silaa imekuja siku chache baada ya Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) kudai kuwa eneo ambalo wanaliomba Yanga ni hatarishi, hivyo watafute eneo lingine kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wao kama kweli uongozi uliopo chini ya Mwenyekiti wake, Yusuf Manji, una nia ya kuwajengea Wanayanga uwanja.

Eneo hilo la Jangwani, mbali ya kuwa ni bonde kubwa la Mto Msimbazi, ambalo ni mkondo wa upumuaji wa bahari, lakini pia kuna bomba kubwa linalopeleka maji Hospitali ya Taifa Muhimbili na lingine linalopeleka maji taka baharini.

Hata hivyo, licha ya Yanga kushauri kuondoka eneo hilo ambalo ni hatarishi, uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake wa

Ujenzi wa Uwanja, Francis Kifukwe, umezidi kusisitiza kuwa kuna masharti ambayo NEMC wamewapa na wakiyatimiza eneo hilo watapewa ikiwemo kubeba fidia za kuwalipa wakazi wa eneo hilo.

“Kuna masharti ambayo wametupa na sisi tupo tayari kuyatekeleza hawajatuambia chochote, huyo aliyekwambia tumenyimwa kujenga uwanja ni nani? Nitajie huyo mtu wa NEMC, ninachoweza kusema kuna masharti na maelekezo ambayo wametupa,” alisema Kifukwe huku akigoma kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kueleza masharti na mapendekezo waliyopewa.

Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Manispaa ya Ilala ilikutana hivi karibuni kujadili suala hilo ambalo hata hivyo wameliacha  mikononi mwa NEMC.

Nayo Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Manispaa ya Ilala ilifanya  ziara ya ukaguzi wa Jangwani hivi karibuni

Wakati huohuo; Mvua hizo zinazoendelea kunyesha zimesababisha ukuta mkubwa wa uzio wa uwanja wa Yanga, ambao umejaa maji kwa sasa kubomoka. Ukuta huo ni ule ambao upo upande wa bonde la Msimbazi chini ya uwanja huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haka kakatuni kinatuambia nini sisi? hata bahari watu wanajenga viwanja itakuwa kwenye mkondo wa maji!!

    ReplyDelete

Top Post Ad