WAISLAMU WAUNGANA NA MAASKOFU KUMTETEA WARIOBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeungana na maaskofu mbalimbali kuwataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuheshimu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwa mujibu wa sheria na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Pia, taasisi hiyo imemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi kutokana na kauli waliyodai ya kichochezi, aliyoitoa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma kuwa ukipitishwa muundo wa serikali tatu, jeshi litachukua nchi kwa sababu itashindwa kuwalipa mishahara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Jumuiya na Taasisi hizo, Sheikh Rajab Katimba alilaani kauli kuhusu jeshi na kuwa makanisa yote yatafungwa na nchi itakosa amani kutokana na kupitisha muundo huo wa serikali.

Sheikh Katimba alisema Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba imetokana na utafiti na uchambuzi wa maoni ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani ili kuboresha Muungano kutatua kero zilizodumu kwa miaka 50 sasa.

Msimamo

Jumuiya hiyo iliweka wazi msimamo wake wa kutaka serikali tatu na kutaka maoni ya makundi mbalimbali ndani ya Bunge la Katiba kuheshimiwa.

Mjumbe wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ramadhan Sanze pia alisema si ustaarabu kwa kundi moja kuhodhi mchakato kwa masilahi binafsi.

Alisema kukosoa maoni ya waasisi wa Taifa si dhambi kwa sababu wao hawakuwa Mungu kwamba hawakosei, badala yake alipendekeza watu waachwe wazungumze kwa utashi wa matakwa yao juu ya kile kilichowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

“Nchi hii haithamini mchango wa wataalamu, tumeona Tume ilivyofanya kazi nzuri, leo hii wanatukanwa hadharani, nawashangaa sana viongozi wa nchi hii,” alisema.

Sheikh Sanze alisema miiko na misingi waliyoiweka waasisi wa Taifa inavunjwa na viongozi wenyewe ambao leo wanasema waasisi wanatukanwa kwa kuwa wamependekeza serikali tatu badala ya mbili walizounda waasisi.

“Kulikuwa na utaratibu wa kubadilishana awamu za uongozi katika Serikali ya Muungano, awamu hii rais akitoka Tanzania Bara, ijayo atatoka Zanzibar; hii ndiyo misingi waliyoiweka waasisi, mbona leo haifuatwi? Huu ni unafiki...” alifafanua Sheikh Sanze.

Jumuiya hiyo imewataka wananchi wote kuendelea na mshikamano katika kutengeneza Katiba Mpya yenye maridhiano na itakayoondoa kero zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad