google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html YASEMAKEANA LULU AMEANZA KURUDIA MAMBO YA MCHARUKO YALIO MPOTEZEA DIRA KABLA | UDAKU SPECIAL

YASEMAKEANA LULU AMEANZA KURUDIA MAMBO YA MCHARUKO YALIO MPOTEZEA DIRA KABLA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KWAKO Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi, juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.

Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu. Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi zako walianza kukutupa.


Walikupotezea kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo, ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana, Januari mwaka jana.

Baada ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali, uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako, ulikuwa mwema sana aisee!. Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu, unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita, nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa. Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa kuvumilia mengi. Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu, kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa. Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa leo ni hayo tu!
Wasalam.
Ni mimi Anko Erick Evarist. 
-GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mtoto Lulu kwa tukio alilopiga ni bora angetulia,na amuuombe sana mungu wake....!!!

    ReplyDelete
  2. Huyu ni mpumbavu wa hakir anauhaba wa hekima ajikague

    ReplyDelete
  3. Mwambie huyo kumaaaaaaaaa!!!!

    ReplyDelete
  4. Toto senge sana hiloooo...!!..

    ReplyDelete
  5. Anadanganyika na uzuri wakat unachuja huo

    ReplyDelete
  6. ivi jamani tangu lini mja asili akaacha asili yake huyu alikua anazuga kwa mda ili watu wamuonee huruma kabadilika bt ukweli hawezi acha mcharuko hata akizeeka alikuja na maneno ya MUngu kibao kiko wapi now

    ReplyDelete
  7. kasahau kabisa mwenzie kaoza huko yeye anatanua, ninahasira ujue

    ReplyDelete
  8. muacheni lulu wa watu.. fanyeni yenu

    ReplyDelete
  9. Huyo kanumba alikufa kwa ufreemason wake mumuache lulu wa watu.

    ReplyDelete
  10. Ulijuaje Kama frermason Kama sio nawewe freemason na mbona siku aliyoanguka na kufa hao freemason awakuonekana kaonekana huyo mbilikimo aliedumazwa na wanaume, pumbavu mkubwa Kama huyo emolo

    ReplyDelete
  11. Yani mtu akiwa na ela freemason , ni jinsi gani usivyo na akili na ulivyo na dhana potofu mbweha mkubwa kazi kumchafua marehem wa watu lione kwanza fukara wa mawazo

    ReplyDelete
  12. wanasema yupo proin promotions sababu moja tu anatoka na huyo Mwenye kampuni ya proin promotions ndugu

    ReplyDelete

Top Post Ad