Aibu Kubwa:Wabongo Wafumaniana China, Wazichapa Bara barani na Kuvuana Nguo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja

Ni aibu kubwa kwa taifa! Huku Waislamu wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja mkazi wa Sinza, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana, wanadaiwa kufumaniana laivu nchini China na kugeuka kituko cha aina yake, Ijumaa Wikienda ndilo lenye uthubutu wa kuripoti tukio hilo.

Habari za awali zilidai kuwa Glory ndiye aliyemfuma mwenzake na bwana’ke, raia wa Nigeria kisha kumshushia kipigo kabla ya kutoana nje na kwenda kuchaniana nguo barabarani, mchana kweupe.

OFM KUTOKA GUANGZHOU, CHINA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, mwakilishi wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers nchini China (jina kapuni), alisema kuwa akiwa katika pitapita zake za kukusanya matukio ili kuyatuma Bongo kuonesha jinsi gani Wabongo wanavyoidhalilisha nchi yao ughaibuni, wikiendi iliyopita alitembelea eneo la Guangzhou Rujing Lu Sky Coffee nchini humo ambalo Watanzania wengi hufanyia ‘biashara’ zao.

Mwakilishi huyo wa OFM alisema akiwa eneo hilo linalosifika kwa matukio na starehe za kichumbani ndipo alipokumbana na timbwili hilo ambalo linaichafua taswira ya Wabongo ambao wanakwenda China kuchukua biashara mbalimbali.

NI AIBU KUBWA
“Dah! Hii ni aibu kubwa ambayo sijawahi kutegemea kuwa nitakutana nayo, yaani Wabongo kwa Wabongo wanapigana, wanachaniana nguo na kuumizana kisa bwana wa Kinigeria, tena ughaibuni!” Alisema kwa masikitiko mwakilishi huyo wa OFM nchini China.

Akiendelea kufunguka, OFM alisema kwamba ilisemekana kuwa Mnigeria huyo aliwahi kuwa na uhusiano na Glory hivyo siku ya tukio, jamaa alimtosa Glory na ‘kuchepuka’ na mwenziye.

KIPIGO CHA MBWA MWIZI
Ilielezwa kwamba Glory hakukubali ndipo akamuanzishia timbwili mwezake na kumpa kipigo cha mbwa mwizi akimtuhumu kwa nini amemchukulia bwana’ke.

WASABABISHA FOLENI
Katika timbwili hilo, warembo hao walijikuta wakichaniana nguo na kubaki nusu utupu huku wakirushiana matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini kimaadili).
Wakati wakipigana waliingia barabarani na kusababisha bonge la foleni huku wakinusurika kukanyagwa na magari hasa walipoangushana katikati ya barabara.

POLISI WAITWA
Kuna wakati Glory alimkaba mwenzake hadi mashuhuda wa sinema hiyo ya bure wakahisi anamuua mwenzake hivyo kulazimika kuita polisi wa usalama barabarani ambaye alifika mara moja na kuwaamulia.
Ilisemekana kwamba, askari huyo alipoona hawaelewani lugha ndipo akawaachia huku kila mmoja akichukua hamsini zake.

GLORY ANASEMAJE?
Baada ya kupata taarifa hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumtafuta Glory kwa njia ya simu yake ya kiganjani lakini hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kuhusiana na tukio hilo, licha ya kuonekana umemfikia (delivered) hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.



YATOKANAYO
Kumekuwa na wimbi la warembo ambao huenda nchini China kwa kisingizio cha kwenda kuchukua biashara lakini ukweli ni kwamba huenda kufanya mambo mengine mabaya (hasa biashara haramu ya kuuza miili).

Mbali na ukahaba, wapo wanaodaiwa kufanywa punda wa kubeba madawa ya kulevya na matokeo yake ni kuishia kunyongwa mara wanapokamatwa.
Hata hivyo, baadhi ya Wabongo waliozungumza na gazeti hili kutoka China, waliziomba mamlaka husika kushughulikia suala hilo hasa wanapotoa vibali vya kutoka nje ya nchi wajue mhusika anakwenda kufanya nini.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mi nahamu kuwadhalilisha ...na .....ambao mara kwa mara wanakuja china,usiku unawakuta madangulo wanajiuza.siku hizi hawapewi dili la kuuza sembe sasa wamebakia kuuza miili yao huku china,baada ya two weeks wanarudi bongo wakavuuuu kutishia watu mavai,laiti wazazi wao wangejua wanafuata nini huku China wasingewaruhuhusu,hivi visa za china mbona rahisi hivi,yaani wasichana wanakuja kila sampuli.hawana hata elimu.wanasingizia wanafanya handbags.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni balaaaa. Kama China inawasumbua hivyo vipi kuhusu Nchi nyingine kama za Ulaya na Marekani dah. Na jinsi soko lilivyokuwa gumu kwa wakati huu. Angalia sasa Uingereza jinsi mademu wa East Europe walivyojazana sijui Lithuania, Poland, Chezk Republic, Russia na kwingineko. Achilia mbali mademu wa French, Italians, Germans halafu ni wazuri na pia wanayo ile sense of humour. Sasa kwa mpango huo mademu wa Kibongo watafurukuta wapi???? Kama ni kazi sasa wanataka uwe na additional language zaidi ya Kiingereza. Ni lazima ujue French au Germany. Sasa angalia ni jinsi gani mademu wa Kibongo wasivyokuwa na wakati mgumu. Matokeo yake wanaishia kuaibishana kwa hivyo viNigeria feki. Jamani rudini Tanzania mkalime. Nendeni mkazuie mashamba mlime. Acheni mteremko dah

      Delete
  2. Jamani mademu wa Kibongo Ulaya hawana dili. Asikudanganye Mtu mademu wa Kibongo yaani ni njaa mpaka basi tena. Hawaliwezi Soko la Ulaya. Elimu hawana lugha hawajui basi ni matatizo matupu. Usione wanatupia picha kwenye Instagram ukawaona kama ni wa maana. Hawana lolote ni kujishaua tu. Ukiwakuta mitaani mpaka wanatia na huruma. Halafu wanavyojua kutembea kwa mafungu utafikiria swala. Niulizeni niwaeleze mademu wa Kibongo jinsi walivyo rosti huku Ulaya dah.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usidanganye watu labda Hao waliolosti huku Ni wale waliozamia meli,karatasi hawana,mtu umekuja kihalali na visa yako utalosti vipi,wenzio tuko ulaya na mahorofa twajenga.

      Delete
  3. Hata wale mademu walio olewa na wazungu ni shida. Wako hapo wamewekwa kama ma house girl. Na majamaaa zao hata hawajali wanawaacha waishi maisha ambayo ni miserable. Wakati huo wao wanaendelea kujirusha na wazungu wenzao. Hawa mind sana kama wanajiendeleza kimaisha ama la. Wanawazalisha vijitoto na kuwaacha hapo.

    ReplyDelete
  4. Na mademu wa Kibongo overseas walivyokuwa wajinga they never want to learn Foreign language. Wamekalia mambo yao yale yale ya kiswahiliiii. Hawana jipya.

    ReplyDelete
  5. dah! kwel tabia haina dawa

    ReplyDelete

Top Post Ad