Alex Massawe Awatoroka Polisi, Ala Kona Dubai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

UONGOZZI mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania chini ya IGP Ernest Mangu umesema unafuatilia kwa karibu nyendo za mfanyabiashara, Alex Massawe ili akamatwe na kumrejesha Bongo kukabiliana na kesi ya mauaji inayomkabili yeye na mfanyabishara mwingine, Marijani Abubakar Msofe ‘Papa Msofe’.

Taarifa kutoka vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo zinadai kwamba, viongozi wa juu wa polisi walisema Massawe alifuatiliwa kwa karibu na Jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol) akiwa Dubai lakini alipogundua yuko mtegoni alitoroka na kwenda Afrika Kusini ambako anaishi hadi sasa.

Chanzo kikasema kuwa, IGP Mangu amesema haoni sababu ya mfanyabiashara huyo kukamatwa na kuletwa nchini kuwe ni hadithi ya muda mrefu wakati uwezo wa kumnasa upo.
Massawe anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi, Novemba 6, 2011 nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ilitoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini kwa Massawe ili kukabiliana na kesi mbili ikiwemo ya kughushi nyaraka mbalimbali.

Massawe anakabiliwa na kesi hiyo ya mauaji namba 150/2013 ambapo mtuhumiwa wa kwanza Papaa Msofe na mwenzake Makongoro Joseph Nyerere wapo Gereza la Keko, Dar wakisubiri kesi hiyo.
Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita lilimtafuta IGP Mangu kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hili ambapo alisema Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCI)  anaweza kusema yote.

Uwazi likamtafuta DCI Isaya Mngulu ofisini kwake, Dar na alipoulizwa juu ya suala hilo alisema ofisi yake kwa kushirikiana na Interpol linamsaka kwa udi na uvumba mtuhumiwa huyo.
“Ni kweli tunamtafuta Massawe, naamini  tutamkamata muda si mrefu na kurejeshwa nchini kukabiliana na kesi yake.

“Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa amewahi kukamatwa Dubai, hiyo si kweli. Inasemekana alikuwa huko na aliposikia anatafutwa akakimbilia Afrika Kusini, tutamkamata tu,” alisema DCI Mngulu. 
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yuko sauz msituzuge

    ReplyDelete
  2. ingekua dereva wa bodaboda fastaaa!!polisi jamani!!ni shiiida!!

    ReplyDelete
  3. Wadau huyo makongoro Ni mtoto WA nyerere huyu mwalimu jk nyerere?? Baba WA taifa??

    ReplyDelete
  4. Hlf nyie police wa nchi hii haki na ramadhani hii nawaambia mtalipia matendoyenu mnakula rushwa hamumkamati.nanyie niwahalifu vilevile.mnamnasa tu amekuwa samaki.mbona anakula bata S.A halafu mnatuletea hadithi hapa kamavipi endeleeni Kula rushwa tu namnyamaze milele sio mnaandika uzushi hapa tumewachoka

    ReplyDelete
  5. Mdau 1:03 umeshaona jina lenyewe ni MAKONGORO JOSEPH NYERERE na baba wa Taifa ni JULIUS NYERERE sasa hapo mtoto wake au mtoto wa kaka/mdogo wake?

    ReplyDelete

Top Post Ad