google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Baada ya Miaka Miwili ya Ndoa, Aunt Ezekiel aanza kusaka Mtoto | UDAKU SPECIAL

Baada ya Miaka Miwili ya Ndoa, Aunt Ezekiel aanza kusaka Mtoto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwigizaji nguli katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) anadaiwa kuanza kusaka mtoto ikiwa ni miaka miwili tangu afunge ndoa na Sunday Dimonte.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Aunt, siku si nyingi staa huyo atakwenda kuweka makazi ya muda kwa mumewe Dubai hadi atakapopata ujauzito.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, rafiki huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ‘matarumbeta’, alisema wengi wanadai mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu hicho hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa ujauzito.

Kama mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo. Lakini baadaye ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai,” alisema rafiki huyo.

Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai, muda si mrefu ataondoka.

Nadhani unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia afya njema ni muhimu ndoa ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai ndiyo mipango yangu.

“Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume wangu amefungwa! Sitaki kuwajibu kwa maneno, nataka kuwajibu kwa vitendo,” alitamba Aunt.

Chanzo: Amani/Gpl
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ujinga sasa hiyo mimba itakuwa na nembo ya mmeo! Mmeo Ni bushoke tu. Bora angekosea kujenga nyumba kuliko kosa alilofanya kukuoa wewe.

    ReplyDelete
  2. kuropoka sio kitu kizuri jifundisheni midomonyenu kua na break......we si ulisema hujaona bado mwanaume wa kuzaa nae ss nani kakuonesha?mastaa wa bongo acheni midomo michafu.kukua sio kukua miguu na kurefuka kukua na akili pia muwe nazo........lol

    ReplyDelete

Top Post Ad